Wenger akufuru Arsenal

LONDON, UINGEREZA

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amelazimika kutenga kitita cha paundi milioni 40 kwenye dirisha dogo la usajili la Januari mwakani, ili kuiongezea nguvu safu ya kiungo.

Arsenal, inakabiliwa na majeruhi kwenye safu ya hiyo baada ya timu ya madaktari kubainisha kuwa viungo wa timu hiyo Saint Carzola na Francis Coquelin watarejea dimbani Machi, mwakani.

Pamoja na kutengwa fedha hizo bado mashabiki wa timu hiyo wanaamini kuwa Wenger hataweza kusajili wachezaji wenye uwezo kutokana na sifa yake ya ubahili.

COMMENTS

Leave a Comment