Na NASRA KITANA
BAADA ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi Kagera Sugar, kaimu kocha wa Yanga, Simon Dladla mzuka upmepanda baada ya kufurahishwa na kiwango kinachooneshwa na wachezaji wake.
Yanga, ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wake wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Dladla alisema kuwa malengo yake ni kuona timu hiyo inapata ushindi katika kila mchezo.
Dladla alisema wameendelea kufanyia kazi kasoro zote zilizojitokeza katika mechi zilizopita.
“Nimefurahishwa na matokeo ya kushinda magoli mengi, kikosi changu kinaendelea kuimarika na kuwa bora zaidi ili kupata ushindi katika kila mchezo,” alisema Dladla.
Nyota wa Yanga Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ alisema ushindi walioupata umewaongezea morari zaidi kuelekea katika mchezo ujao.
“Tumefurahi kupata ushindi mkubwa na tutahakikisha tunapambana mwanzo mwisho ili kushinda katika kila mchezo ujao,” alisema Tshabalala.
Kocha wa Kagera Sugar, Cedric Kaze alisema wamepoteza mchezo huo lakini wanaenda kujipanga upya kuhakikisha wanapata ushindi.
Kaze alisema kuwa kutokana na makosa waliyoyafanya wachezaji wake ndio yamesababiosha kushindwa kufanya vizuri.
“Tumepoteza mchezo wetu lakini hatujakata tamaa tunaenda kupambana na kufanya marekebisho yaliojitokeza ili kufanya vizuri katika mechi zinazofuata,” alisema Kaze.
Kaze alisema wamepoteza na timu bora lakini hawajakata tamaa wanaenda kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo.
Katika msimamo wa ligi Yanga inaendelea kusalia nafasi ya pili ikiwa na pointi 25 huku Kagera Sugar ikisalia mkiani ikiwa na pointi sita




