• ePaper
Saturday, November 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAELFU YA MIRADI YASAJILIWA TISEZA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 3, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MAELFU YA MIRADI YASAJILIWA TISEZA
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), imesema kipindi cha Julai, 2025 hadi Septemba 30, 2026,imesajili miradi 1,148 ya uwekezaji, yenye thamani dola za Marekani bilioni 15.32 ambayo inatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 344,031.

Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gilead Teri, ameeleza hayo Novemba 2, 2026, katika mkutano na wahariri na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.

Amesema katika miradi hiyo,  uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi umefikia dola za Marekani bilioni 9.60 na uwekezaji wa

ndani ukiwa ni dola bilioni 5.72.

Akielezea uendelezaji wa maeneo maalumu ya kiuchumi, Teri amesema mamlaka imezidi kuendeleza maeneo hayo  kuvutia wawekezaji

katika shughuli za viwanda, uzalishaji, uchakataji mazao, biashara na huduma za usafirishaji, huku maeneo yaliyopewa kipaumbele ni Bagamoyo, Kwala na Nala.

Amesema kupitia juhudi za kutangaza maeneo hayo na kushirikiana na wawekezaji, mamlaka imepokea maombi zaidi ya 80 ya matumizi ya ardhi ndani ya maeneo maalumu ya uwekezaji kiuchumi. Kati ya hayo, maombi 43 yamefikia hatua ya kusainiwa mikataba ya upangishaji au haki za upangaji wa ardhi.

Teri amesema matarijio ya TISEZA kuvutia uwekezaji wa zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.5 na kuzalisha ajira zaidi ya 15,844.

Kuhusu uwekezaji, Teri alisema sekta za viwanda, uchukuzi, utalii, kilimo na madini zimekuwa miongoni mwa maeneo yanayovutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Aidha, ameeleza mwenendo huo umeonesha namna shughuli za uzalishaji, usafirishaji na huduma zinavyoendelea kuwa sehemu muhimu ya uwekezaji, huku ushirikiano kati ya Watanzania na wawekezaji wa kigeni ukizidi ‘kupaa’.

“Sekta ya viwanda inaongoza kwa idadi ya miradi ya uwekezaji, ikifuatiwa na uchukuzi, majengo ya kibiashara, utalii na kilimo,” amesema.

Teri amefafanua sekta ya viwanda ina miradi 1,660, uchukuzi 525, majengo ya kibiashara 361, utalii 338 na kilimo miradi 308, sekta nyingine zinazovutia uwekezaji ni madini, huku kilimo, viwanda na bidhaa za misitu zikiwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa mauzo ya bidhaa za Tanzania katika masoko ya nje.

Pia, Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na miradi 1,339, ukifuatiwa na Pwani wenye miradi 680, Arusha 232, Mwanza 164 na Dodoma miradi 157.

Previous Post

WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

Next Post

TANZANIA YAJIPANGA KUVUTIA UWEKEZAJI MKUBWA WA NISHATI DUNIANI

Next Post
TANZANIA YAJIPANGA KUVUTIA UWEKEZAJI MKUBWA WA NISHATI DUNIANI

TANZANIA YAJIPANGA KUVUTIA UWEKEZAJI MKUBWA WA NISHATI DUNIANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AVUNJA NGOME YA UPINZANI MKOANI LINDI

DK. SAMIA AVUNJA NGOME YA UPINZANI MKOANI LINDI

1 year ago
SIFA KEMKEMU ZA LUKUVI

SIFA KEMKEMU ZA LUKUVI

7 months ago

Popular News

  • PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANADANA UCHAGUZI SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UFAULU WALIOMALIZA ELIMU MSINGI WAPAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?