• ePaper
Saturday, November 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA UADILIFU, UTATUZI MIGOGORO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 3, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA AHIMIZA UADILIFU, UTATUZI MIGOGORO
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa maagizo kwa viongozi wapya aliowaapisha, akiwasisitiza kutekeleza majukumu kwa uadilifu, kusimamia haki na kuwajibika katika nafasi walizokabidhiwa.

Pia, amesisitiza umuhimu wa usimamizi mzuri wa fedha za serikali, kushughulikia malalamiko ya wananchi kuhusu ukiukwaji haki za binadamu na kuhakikisha migogoro ya wafanyakazi, inatatuliwa kwa kuzingatia sheria bila chuki, hila au upendeleo.

Rais Dk. Saia alitoa kauli hiyo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, ambao ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Angeline Mabula, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dunford Mpelumbe.

Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Omar Ali Omar na Jaji Mstaafu Peter Dyansobera, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi  na Usimamizi na makamishna wa tume hiyo.

MAAGIZO YAKE KWA ANGELINE MABULA

Rais Dk. Samia, alimtaka Angeline, kuhakikisha fedha za serikali zinazotolewa kwa maendeleo, zinasimamiwa vizuri na kutumika kutatua changamoto za wananchi.

Alisema Angeline ana uzoefu mkubwa katika utumishi wa umma kutokana na nafasi mbalimbali alizowahi kushika, ikiwemo ya mkuu wa wilaya, naibu waziri, waziri na mbunge.

Alisema uzoefu huo, unampa uelewa wa kutosha kuhusu mahitaji ya wananchi, namna serikali inavyotoa fedha na changamoto zinazopaswa kushughulikiwa katika maeneo mbalimbali.

Alimtaka ashirikiane na viongozi na watendaji atakaowakuta mkoani Tabora, kuhakikisha fedha zinazotolewa na serikali, zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Ukasisimamie fedha tunazozileta, zikaondoshe shida za watu,” alisema Rais Samia.

TUME YA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Rais Samia, aliitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kusimamia ipasavyo majukumu yake kwa kupokea malalamiko ya wananchi wanaodai kuvunjiwa haki na kuyafanyia kazi.

Akiwaapisha viongozi Mpelumbe na Omar, aliwaambia kuwa, tume hiyo inapaswa kufuatilia masuala ya utawala bora na kujibu haraka shutuma zinazotolewa dhidi ya Tanzania kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu.

Alisema katika dunia ya sasa, kuna nchi zinazofanya vizuri, lakini bado zinakabiliwa na shutuma kuhusu masuala ya haki za binadamu, hivyo wajumbe wa tume wanapaswa kuelewa yanayotokea duniani na hali halisi ya ndani ya nchi.

“Katika dunia ya leo, nchi zinazofanya vizuri, zinaweza kushutumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, hivyo nawaomba mchunguze mitandao ya kijamii, mfahamu yanayotokea duniani na mjibu kwa haraka shutuma zinazoelekezwa Tanzania, huku mkihakikisha malalamiko ya wananchi kuhusu ukiukwaji wa haki zao yanapokelewa na kufanyiwa kazi,” alisema.

Pia, aliwataka viongozi wa tume hiyo kutumia uwezo wao katika kusimamia  haki za binadamu na utawala bora.

Alisema ni muhimu tume hiyo ihakikishe malalamiko yanayowasilishwa, yanashughulikiwa na kufikishwa katika sekta husika pindi yanapobainika kuwepo ukiukwaji wa haki au utawala bora.

TUME YA USULUHISHI  NA UAMUZI WA MIGOGORO

Aidha, Rais Samia, alimtaka Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Wafanyakazi, Jaji Mstaafu Dyansobera na makamishna, kutekeleza majukumu yao kwa haki bila chuki, hila au upendeleo.

Alisema uamuzi unaotolewa, unapaswa kuzingatia sheria za kazi na makosa yaliyofanywa na mfanyakazi, bila kujali jina, nafasi au mahusiano ya mtu anayehusika.

“Mfanyakazi amekosa, sheria za kazi zinasemaje. Hukumu yake ni hii. Hiyo ndiyo kazi yenu, hata kama likija jina la mtu unayemfahamu, sheria na makosa aliyoyafanya  ndiyo yaamue bila upendeleo waka chuki,” alisema.

Alieleza tume hiyo inapaswa kufanya kazi kwa umakini kwa kuwa, baadhi ya wahusika hawaridhiki na uamuzi unaotolewa na wengine hukata rufaa, hivyo kila uamuzi lazima uzingatie hoja na sheria zilizopo.

Alisema kufunguka nchi na kuongezeka uwekezaji katika sekta binafsi, kunaweza kuongeza migogoro ya wafanyakazi, hivyo aliwataka kusimamia sheria na kulinda haki za waajiri na waajiriwa.

Pia, aliwapongeza viongozi wote waliopatiwa dhamana hizo, aliwataka kuitumikia nchi kwa uadilifu, akisisitiza kuwa serikali ina matarajio makubwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Previous Post

SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA KUONGEZA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI – WAZIRI KAPINGA

Next Post

KOCHA YANGA ‘FULL’ MZUKA

Next Post
KOCHA YANGA ‘FULL’ MZUKA

KOCHA YANGA ‘FULL’ MZUKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MCHAKATO WA MABADILIKO SIMBA MBIONI KUKAMILIKA

MCHAKATO WA MABADILIKO SIMBA MBIONI KUKAMILIKA

11 months ago
SABABU SARE AZAM, YANGA SC IKO HAPA

SABABU SARE AZAM, YANGA SC IKO HAPA

8 months ago

Popular News

  • PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANADANA UCHAGUZI SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UFAULU WALIOMALIZA ELIMU MSINGI WAPAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?