• ePaper
Saturday, November 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA YAJIPANGA KUVUTIA UWEKEZAJI MKUBWA WA NISHATI DUNIANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 3, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA YAJIPANGA KUVUTIA UWEKEZAJI MKUBWA WA NISHATI DUNIANI
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nishati, Dk. Juma Homera, amesema Tanzania imejipanga kutumia fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati duniani kwa kuvutia mitaji ya ndani na nje.

Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Nishati (ADIPEC 2026) unaofanyika Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Dkt. Homera amesema Tanzania imeweka mikakati ya kuvutia wawekezaji katika kipindi ambacho usalama wa nishati umekuwa kipaumbele cha kimataifa kutokana na changamoto za minyororo ya ugavi zinazosababishwa na migogoro ya kijiografia na kisiasa.

Amesema Tanzania ina fursa kubwa za uwekezaji kutokana na kuwa na takribani futi za ujazo trilioni 57.54 za gesi asilia zinazoweza kuendelezwa kupitia miradi ya LNG na Mini-LNG, pamoja na miradi ya uzalishaji umeme ikiwemo Bwawa la Julius Nyerere (MW 2,115), mradi wa umeme wa jua Kishapu (MW 150), nishati ya upepo mkoani Singida na jotoardhi katika mikoa ya Mbeya na Songwe.

Aidha, Dkt. Homera amesema nafasi ya kijiografia ya Tanzania inaipa fursa ya kuwa kitovu cha biashara ya nishati kikanda kupitia masoko ya umeme ya Afrika Mashariki na Kusini, huku akisisitiza umuhimu wa sera zinazotabirika, mifumo imara ya kisheria, kupunguza urasimu na kuandaa miradi yenye tafiti za kina ili kuongeza ushindani katika kuvutia mitaji ya kimataifa.

Ameeleza kuwa Serikali, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, inaendelea kutekeleza Mkataba wa Kitaifa wa Nishati (National Energy Compact) unaolenga kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi wa takribani dola za Marekani bilioni 4.039, huku vipaumbele vikiwa ni uwekezaji katika nishati jadidifu, uimarishaji wa miundombinu ya usafirishaji umeme na ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP).

Dkt. Homera amesisitiza kuwa utekelezaji wa mikakati hiyo utaiwezesha Tanzania kubadilisha utajiri wa rasilimali za nishati kuwa miradi halisi yenye tija kiuchumi, kuvutia wawekezaji wa kimataifa na kuimarisha nafasi ya nchi katika soko la nishati duniani.

Previous Post

MAELFU YA MIRADI YASAJILIWA TISEZA

Next Post

SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA KUONGEZA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI – WAZIRI KAPINGA

Next Post
SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA KUONGEZA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI – WAZIRI KAPINGA

SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA KUONGEZA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI - WAZIRI KAPINGA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA, SIMBA ZAPEWA MBINU KULIPA KISASI 

YANGA, SIMBA ZAPEWA MBINU KULIPA KISASI 

9 months ago
SIMBA, YANGA MZIGONI LEO

SIMBA, YANGA MZIGONI LEO

8 months ago

Popular News

  • PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANADANA UCHAGUZI SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UFAULU WALIOMALIZA ELIMU MSINGI WAPAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?