• ePaper
Saturday, November 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

TANZANIA YAMOTO ‘MISS AFRICA’

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 3, 2026
in Burudani, Kimataifa, Michezo
0
TANZANIA YAMOTO ‘MISS AFRICA’
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

TANZANIA imeendelea kuwa ya moto katika mashindano  ya urembo, baada ya Eva Godwin kushinda taji la Miss Africa International.

Mrembo huyo, aliibuka mshindi wa shindano  hilo, lililofanyika nchini Nigeria na kuiwezesha Tanzania kuendelea kung’ara katika mashindano ya urembo ya Kimataifa.

Ushindi wa Eva, umetangazwa usiku wa kuamkia, huku pongezi mbalimbali zikitolewa kwa Eve Godwin pamoja na timu iliyokuwa nyuma ya ushiriki wake, ikiongozwa na Nazimizye Adam Mdolo, Mkurugenzi wa Miss Grand Tanzania.

Mafanikio ya Eva, yamezidi kuitangaza Tanzania katika mashindano ya kimataifa mwaka huu, baada ya hivi karibuni,  Jihan Dimack kutwaa taji la Miss Grand International 2026 nchini Thailand.

Kufuatia ushindi huo, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limempongeza Eva Godwin kwa kutwaa taji la Miss Africa International 2026, ushindi umeonesha uwezo, vipaji na ubora wa Watanzania katika majukwaa ya kimataifa ya urembo.

Pongezi hizo, zilitolewa jana kupitia ukurasa wa BASATA wa mtandao wa kijamii ‘Instagram’, ambapo baraza hilo limeeleza kuwa, mafanikio hayo ni fahari kwa taifa.

Aidha, baraza hilo, limetoa pongezi kwa wadau wote wanaoendelea kuunga mkono, kuhamasisha na kutoa nguvu kwa vipaji vya Watanzania vinavyooneshwa katika majukwaa mbalimbali.

“Ushirikiano huu ni muhimu katika kukuza sanaa, kuinua vipaji na kuitangaza Tanzania kimataifa, tutaendelea kushirikiana, kuviunga mkono vipaji vyetu na kuifanya Tanzania iendelee kung’ara duniani kwani, anaa ni aAjira, biashara na uchumi,’ilieleza taarifa hiyo

Kutokana na mafanikio hayo, baadhi ya wasanii walipozungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana, walimpongeza Eva kwa ushindi huo, huku wakiwasihi wasichana wengine kujitokeza kushiriki mashindano mbalimbali ya urembo ili kuonesha vipaji vyao na kuitangaza nchi kimataifa.

Msanii wa filamu na tamthilia, Kelly Collins ‘Fifi’, alimpongeza Eva kwa ushindi huo kwani  ni mafanikio yanayopaswa kuwa chachu kwa wasichana wengine kuamini uwezo wao na kuthubutu kushiriki mashindano ya kimataifa.

Alisema ushindi huo unaonesha kuwa Watanzania wana uwezo wa kushindana na kufanya vizuri katika majukwaa ya kimataifa iwapo wataendelea kupata maandalizi mazuri, ushauri na ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali.

Pia, aliwasihi wasichana wenye ndoto za kushiriki mashindano hayo kujitokeza kwa wingi, kujiamini na kutumia fursa zinazopatikana kukuza uwezo wao.

 “Niwasihi wadau wa sanaa na sekta ya urembo kuendelea kutoa mafunzo na kuwaandaa wasichana ili waweze kushindana kwa viwango vya kimataifa,”alisema.

Msanii wa tasnia ya uigizaji Asha Jumbe, ‘White Maria’, aliwasihi wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa watoto wao katika kukuza vipaji walivyonavyo badala ya kuwakatisha tamaa.

Pia, Rossie Uisso alifanikiwa kuingia 12 bora ya Miss Global International na Sharon Julius kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Miss Elite World yaliyofanyika nchini Misri.

Previous Post

KOCHA YANGA ‘FULL’ MZUKA

Next Post

WACHIMBAJI WADOGO KUNUFAIKA NA VIWANDA VYA UONGEZAJI THAMANI

Next Post
WACHIMBAJI WADOGO KUNUFAIKA NA VIWANDA VYA UONGEZAJI THAMANI

WACHIMBAJI WADOGO KUNUFAIKA NA VIWANDA VYA UONGEZAJI THAMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KAPOMBE, DUCHU WATOA MSIMAMO SIMBA

KAPOMBE, DUCHU WATOA MSIMAMO SIMBA

10 months ago
YANGA, AL AHLY MECHI YA MAAMUZI

YANGA, AL AHLY MECHI YA MAAMUZI

9 months ago

Popular News

  • PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANADANA UCHAGUZI SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UFAULU WALIOMALIZA ELIMU MSINGI WAPAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?