• ePaper
Saturday, November 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 4, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na, MWANDISHI WETU – NAIROBI, KENYA

NCHI wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimetakiwa kuimarisha ushirikiano na kuchukua hatua za haraka kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño, zikiwemo mafuriko, maporomoko ya ardhi, uharibifu wa miundombinu na kuathirika kwa biashara na maisha ya kawaida ya wananchi.

Wito huo umetolewa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Dharura wa Wataalamu wa Sekta Mbalimbali kuhusu Maandalizi na Mwitikio wa Kikanda dhidi ya Mvua Zinazotarajiwa za El Niño Kali, unaofanyika Nairobi, Kenya, kuanzia Novemba 4 hadi 6, 2026.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa wataalamu  umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Brigedia Jenerali Hosea Ndagala.

Akifungua mkutano huo Mratibu wa Mradi wa Pamoja wa Sekta Mbalimbali wa Usalama wa Chakula na Lishe wa Uganda, Bw.Julius Twinamatsiko amesema utabiri unaonesha uwezekano wa mvua kunyesha kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026, hali inayohitaji maandalizi ya haraka na hatua za pamoja.

Amezitaka nchi wanachama kubaini maeneo hatarishi katika miundombinu ya usafirishaji, kuandaa njia mbadala, kuhakikisha upatikanaji wa chakula na malisho ya mifugo, pamoja na kuimarisha huduma za afya na ufuatiliaji wa magonjwa yanayoweza kuenea kutokana na mafuriko.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Sekretarieti ya EAC amesisitiza kuwa athari za El Niño zinaweza kuhatarisha amani, usalama na maendeleo ya kiuchumi, hivyo juhudi za kila nchi zinapaswa kuunganishwa kupitia mpango wa pamoja wa kikanda.

Mkutano huo unalenga kutathmini uwezo wa nchi wanachama kukabiliana na athari zinazotarajiwa, kubaini mapungufu na kuandaa mpango wa uratibu wa kikanda utakaosaidia kulinda maisha ya wananchi, huduma muhimu na shughuli za biashara katika Afrika Mashariki.

Previous Post

WACHIMBAJI WADOGO KUNUFAIKA NA VIWANDA VYA UONGEZAJI THAMANI

Next Post

TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

Next Post
TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWINYI APANIA KUPAISHA UCHUMI

DK. MWINYI APANIA KUPAISHA UCHUMI

1 year ago
BIMA YA AFYA YAHITAJI UANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI

BIMA YA AFYA YAHITAJI UANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI

9 months ago

Popular News

  • PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANADANA UCHAGUZI SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UFAULU WALIOMALIZA ELIMU MSINGI WAPAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?