• ePaper
Saturday, November 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WACHIMBAJI WADOGO KUNUFAIKA NA VIWANDA VYA UONGEZAJI THAMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 4, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WACHIMBAJI WADOGO KUNUFAIKA NA VIWANDA VYA UONGEZAJI THAMANI
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, amewataka wamiliki wa viwanda vya uongezaji thamani madini ya metali nchini kuwa soko la uhakika la madini yanayozalishwa na wachimbaji wadogo ili kuimarisha mnyororo wa thamani wa madini, kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa Taifa.

Waziri Mavunde ametoa wito huo wakati wa kikao chake na wamiliki wa viwanda hivyo katika Ofisi za Tume ya Madini jijini Dodoma Waziri ambapo amesisitiza umuhimu wa wamiliki wa viwanda kuingia katika makubaliano ya kibiashara yenye tija na wachimbaji wadogo, ili kuhakikisha wachimbaji wanapata soko la uhakika la madini yao na viwanda vinapata malighafi zinazohitajika kwa ajili ya uzalishaji.

Amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuimarisha mnyororo wa thamani wa madini ya metali nchini, kuongeza uzalishaji na kuhakikisha manufaa ya uwekezaji katika viwanda vya uongezaji thamani yanawafikia pia wachimbaji wadogo.

Waziri Mavunde amepongeza muitikio wa Watanzania katika kuanzisha viwanda vya uongezaji thamani madini, akieleza kuwa uamuzi wa Serikali kuzuia usafirishaji wa madini ghafi ambayo hayajachakatwa nje ya nchi umechochea uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo.

Amesema uwekezaji huo umewezesha kujifunza na kutumia teknolojia mpya, kuongeza ajira kwa Watanzania na kukuza mapato ya Serikali, sambamba na kujenga msingi wa uchumi unaotegemea uzalishaji wa bidhaa zenye thamani kubwa.

Aidha, amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini, akieleza kuwa hatua zinazochukuliwa na Serikali zimekuwa chachu ya ukuaji wa sekta ya madini na kuvutia uwekezaji katika shughuli za uchakataji na uongezaji thamani.

“Ni jukumu la Serikali kuhakikisha wawekezaji hawa hawakwami. Wizara ya Madini itaendelea kutoa miongozo na ushirikiano unaohitajika ili kuhakikisha viwanda hivi vinafikia malengo ya kuanzishwa kwake,” amesema Mavunde.

Katika hatua nyingine, Waziri Mavunde amemuagiza Kamishna wa Madini na Tume ya Madini kutembelea viwanda vya Zamahero na Haneti vilivyoanza uzalishaji wa madini ya nikeli na shaba ili kubaini changamoto na kuwasilisha mapendekezo ya kuboresha mazingira ya uzalishaji.

Amesisitiza umuhimu wa wamiliki wa viwanda na wachimbaji wadogo kuweka makubaliano madhubuti ya kibiashara, akibainisha kuwa changamoto ya baadhi ya wachimbaji kushindwa kuwasilisha madini baada ya kupokea fedha za awali imeathiri uaminifu na upatikanaji wa malighafi na kwamba Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji ili kuhakikisha viwanda vinafanya kazi kwa tija, kuongeza ajira na kukuza matumizi ya teknolojia mpya.

Kwa upande wao, Wamiliki wa viwanda wameishukuru Serikali kwa kutatua changamoto ya muda mrefu ya umeme katika maeneo ya uzalishaji, huku Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini ya Metali Tanzania (TBMA), Tobias Kente, akimshukuru Waziri Mavunde kwa kuendelea kushughulikia changamoto za wadau wa sekta hiyo.

Previous Post

TANZANIA YAMOTO ‘MISS AFRICA’

Next Post

NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Next Post
NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

BODABODA WAKINGIWA KIFUA

BODABODA WAKINGIWA KIFUA

5 months ago
TUME YA JAJI CHANDE KUIMARISHA DEMOKRASIA

TUME YA JAJI CHANDE KUIMARISHA DEMOKRASIA

8 months ago

Popular News

  • PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANADANA UCHAGUZI SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UFAULU WALIOMALIZA ELIMU MSINGI WAPAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?