• ePaper
Saturday, November 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 5, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

TANZANIA inatarajia kupata Chuo Mahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (DTI) jijini Dodoma, ambacho ujenzi wake unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 441, kupitia mkopo nafuu kutoka Serikali ya Korea Kusini, kwa ajili ya kuimarisha uzalishaji wa wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu katika teknolojia za kidijiti, ikiwemo Akili Unde.

Mradi huo utaanza kutekelezwa baada ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Exim ya Korea Kusini, Novemba 3 mwaka huu, kutia saini mkataba wa mkopo wenye riba nafuu wa dola za Marekani milioni 167.4, sawa na sh. bilioni 441.12, utakaotolewa kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea (EDCF).

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo, Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, alisema chuo hicho kitakuwa na mchango mkubwa katika kuandaa na kukuza wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu katika fani za kiufundi na kuimarisha sekta ya tehama nchini.

Amesema chuo hicho kitakuwa na vituo vya kisasa vya mafunzo, maabara, miundombinu ya kidijiti na tafiti, huku kikiimarisha uhusiano kati ya taasisi za elimu na sekta ya viwanda ili kupunguza pengo la ujuzi na kuchochea maendeleo ya teknolojia.

“Mradi huu umekuja wakati mwafaka ambapo Tanzania inaendelea kutekeleza ajenda ya mageuzi ya kidijiti na kujenga rasilimali watu pamoja na uwezo wa kitaasisi unaohitajika kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijiti’ Alisema Dkt. Mwamba.

Amesema Wizara ya Fedha itashirikiana kwa karibu na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na taasisi zote zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo, ikiwemo kutoa mchango wa ndani unaohitajika ili kuhakikisha unatekelezwa kwaufanisi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Exim ya Korea, Bw. Dong-Hoon Lee, alisema mradi huo una umuhimu mkubwa kwa nchi hizo mbili kwa kuwa ni mradi wa kwanza wa EDCF kuidhinishwa mwaka huu na wa kwanza unaohusisha usaidizi katika eneo la Akili Unde.

Amesema majadiliano ya kuidhinisha mradi huo yalianza Aprili mwaka huu kisha ikatolewa sera ya usaidizi wa serikali Agosti mwaka huu na kufikia hatua hiyo ya utiaji saini mkataba huo Novemba mwaka huu.

Amesema kasi hiyo imetokana na ushirikiano thabiti kutoka Serikali ya Tanzania na kusisitiza kuwa Korea itaendelea kuwa mshirika wa kuaminika katika kusaidia maendeleo ya Tanzania kupitia miradi mbalimbali ya ushirikiano katika sekta za barabara, nishati na afya.

“Ushirikiano huu utaimarisha ukuaji wa pande zote mbili na urafiki wa nchi hizi mbili” alisisitiza Bw. Lee.

Mradi huo wa Chuo Mahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-Dodoma, unaongezwa katika orodha ya miradi inayoendelea kutekelezwa kwa ushirikiano na Benki ya Exim ya Korea, yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.12, inayohusisha sekta za nishati, kilimo, maji safi na maji taka, reli na sekta nyinginezo.

Previous Post

UFAULU WALIOMALIZA ELIMU MSINGI WAPAA

Next Post

DANADANA UCHAGUZI SIMBA

Next Post
DANADANA UCHAGUZI SIMBA

DANADANA UCHAGUZI SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

TANZANIA, SINGAPORE KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

5 months ago
KIPIGO, KUNYIMWA UNYUMBA UKATILI MPYA KWA WANAUME

KIPIGO, KUNYIMWA UNYUMBA UKATILI MPYA KWA WANAUME

10 months ago

Popular News

  • PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANADANA UCHAGUZI SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UFAULU WALIOMALIZA ELIMU MSINGI WAPAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?