• ePaper
Saturday, November 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 5, 2026
in Habari, Kitaifa
0
PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MCHANGO  wa Watanzania katika kuendeleza sekta ya bahari kimataifa umezidi kutambuliwa baada ya Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Prof Tumaini Shabani Gurumo kutunukiwa tuzo ya heshima ya Mwanafunzi wa Zamani Mashuhuri (Outstanding Alumna Award) kutoka  Chuo Kikuu cha World Maritime University (WMU) kilichopo nchini Sweden.

Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha uongozi, elimu na mafunzo ya sekta ya bahari pamoja na kuchochea maendeleo ya taasisi zinazohusika na sekta hiyo barani Afrika.

Katibu Mkuu wa Shirika la Bahari Duniani Bwana Arsenio Dominguez alimkabishi Prof  Gurumo tuzo hiyo Oktoba 31 Mwaka huu katika mahafali ya 43 ya (WMU) yaliyofanyika nchini Sweden  mbele ya Mgeni Rasmi ,Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya chuo hicho na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Jiji la Malmo.

Aidha  Prof  Gurumo amekuwa na mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya bahari hususani  katika uongozi, utafiti katika  kuimarisha uwezo wa wataalamu wa sekta hiyo.

Prof  Gurumo  Amefanya kazi katika sekta ya bahari kwa zaidi ya miaka 20 ambapo miaka 10 ameitumikia katika nafasi mbalimbali za usimamizi na uongozi Katika kipindi hicho huku  akijihusisha na ufundishaji wa sheria za bahari kwa wataalamu wenye uzoefu na wanaoanza taaluma katika maeneo ya bandari, usafirishaji wa majini na masuala ya bahari.

Akizungumzia mchango wake   Rais wa (WMU) Profesa Maximo Mejia Jr amesema kuwa  Prof Gurumo ametumia sehemu kubwa ya maisha yake ya kitaaluma kuendeleza sekta ya bahari kupitia ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu.

Hata hivyo  Prof Gurumo  ni mtafiti na mwandishi wa machapisho mbalimbali ikiwemo kitabu kinachohusu Uchumi wa Buluu, Fursa, na Chachu ya Maendeleo huku  akifanya kazi kama  mshauri wa kitaalamu katika masuala ya uchumi wa buluu na usafirishaji wa majini kwa Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) na TradeMark East Africa (TMEA).

“Kupitia Mchango wake  ameboresha elimu na mafunzo ya sekta ya bahari ikiwa ni  hatua iliyosaidia kuimarisha viwango vya ubora na kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi wa kutekeleza majukumu yao katika meli, bandari,  na mamlaka za usimamizi wa bahari na usafirishaji wa mizigo.” Amesema Prof Mejia Jr.”

Katika hatua nyingine Prof  Gurumo alihitimu Shahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Tumaini, Kampasi ya Iringa mwaka 2004, kabla ya kupata Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Masuala ya Bahari na kubobea Sheria na Sera  kutoka (WMU) mwaka 2007 Mwaka 2012 alipata Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kimataifa za Bahari kutoka Dalian Maritime University nchini China.

Katika  mahafali  hayo Watanzania wengine wanne walitunukiwa vyeti vya kuhitimu shahada ya uzamili na stashahada katika fani mbalimbali za sekta ya bahari.

Mafanikio hayo yanatarajiwa kuongeza nguvu katika upatikanaji wa wataalamu wenye ujuzi wa kimataifa na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika maendeleo ya sekta ya bahari na uchumi wa buluu barani Afrika.

Previous Post

DANADANA UCHAGUZI SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WANASIASA WAGUSIA USHINDI WA RAIS DK. SAMIA

WANASIASA WAGUSIA USHINDI WA RAIS DK. SAMIA

12 months ago
WADAU WA SOKA WAMPONGEZA ZUNGU 

WADAU WA SOKA WAMPONGEZA ZUNGU 

12 months ago

Popular News

  • PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    PROF. GURUMO AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KUPITIA SEKTA YA BAHARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANADANA UCHAGUZI SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOREA YAIPATIA TANZANIA BILIONI  441 KUJENGA CHUO CHA TEHAMA DODOMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UFAULU WALIOMALIZA ELIMU MSINGI WAPAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA NISHATI JUA NCHINI INDIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?