• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

CCM YAELEZA KUONGEZEKA MBOLEA YA RUZUKU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 12, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
CCM YAELEZA KUONGEZEKA MBOLEA YA RUZUKU

Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi

0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA,

Katavi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, mbolea ya ruzuku imeongezeka maradufu kutoka tani 240 hadi kufikia tani 1,022 mwaka huu.


Hayo yalibainishwa Kata ya Inyonga, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi na Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, alipowahutubia mamia ya wananchi, waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Pia, Dk. Nchimbi, alitumia fursa hiyo, kueleza utekelezaji wa Ilani ya Chama na kuinadi mpya ya mwaka 2025-2030.

Aliwaomba wananchi wa eneo hilo, kumchagua Dk. Samia Suluhu Hassan nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Pia, aliwaomba zaidi kuwapigia kura wagombea wa ngazi ya Ubunge na Udiwani, wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi.


Alisema kuongezeka kwa mbolea ya ruzuku katika halmashauri hiyo, ni matokeo ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2026 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.Alisema mbolea ya ruzuku, imeongezeka maradufu kutoka tani 240 zilizokuwa zikipatikana miaka mitano iliyopita hadi kufikia tani 1,022 mwaka huu.


Pia, alisema katika sekta ya mifugo, majosho matano yamejengwa katika halmashauri hiyo na mawili ya kunyweshea, hatua inayolenga kuboresha afya ya mifugo na kuinua kipato cha wafugaji.


Aidha, mabwawa mawili ya ufugaji samaki, yamejengwa kuwawezesha wananchi wa Mlele kushiriki katika shughuli za uvuvi na ufugaji wa kisasa kwa kutumia teknolojia ya mabwawa, hivyo kusaidia kuongeza ajira na kipato cha familia.


Alisema katika kipindi hicho cha miaka mitano, huduma za afya, zimeimarishwa, Hospitali ya Wilaya ya Mlele, imejengwa na vifaa muhimu vimenunuliwa ikiwemo X ray ya dijital.


“Katika miaka mitano iliyopita, huduma za afya zimeboreshwa, Hospitali ya Mlele imejengwa, vilevile vifaa muhimu vya kisasa na digital x ray imenunuliwa,” alisema.
Kwa mujibu wa Balozi Dk. Nchimbi, katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Mlele, zahanati sita zimejengwa.


Akizungumzia sekta ya elimu, Dk. Nchimbi, alisema shule tano zimejengwa na idadi ya madarasa kuongezeka kutoka 135 hadi 322.
Alisema barabara za lami, zimeongezeka huku za changarawe zikifikia zaidi ya kilometa 2,000 kutoka kilometa 74.


Alisisitiza kuwa, katika miaka mitano ijayo, iwapo watapewa ridhaa ya kuongoza nchi, mipango zaidi imewekwa ikiwemo ya ujenzi wa vituo vya afya vipya viwili, zahanati tatu, sekondari 11 na madarasa 98.


Pia, miradi mipya ya maji, inatarajiwa kutekelezwa katika maeneo 16 na skimu za umwagiliaji kuimarisha kilimo cha kisasa.
Pia, kilimo cha umwagiliaji kitaimarishwa kwa kuendeleza skimu za umwagiliaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.

Previous Post

AHADI 5 ZA MGOMBEA URAIS WA CCM, IGUNGA

Next Post

NLD KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

Next Post
NLD KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

NLD KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI AGUSIA HISTORIA MPYA ILIYOANDIKWA NA DK. SAMIA

DK. NCHIMBI AGUSIA HISTORIA MPYA ILIYOANDIKWA NA DK. SAMIA

1 week ago
CCM YAAHIDI KILIMO CHA BIASHARA KWA WAKULIMA

CCM YAAHIDI KILIMO CHA BIASHARA KWA WAKULIMA

3 weeks ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.