• ePaper
Thursday, August 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

PROF. KABUDI AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TAHADHARI ZA MAAFA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 20, 2026
in Habari, Kitaifa
0
PROF. KABUDI AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TAHADHARI ZA MAAFA
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na, Mwandishi wetu – Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, amewataka wananchi kuzingatia tahadhari na maelekezo yanayotolewa na wataalamu na mamlaka husika ili kupunguza madhara yanayotokana na majanga na maafa.

Prof. Kabudi ametoa wito huo Agosti 19, 2026, akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Watoa Huduma za Misaada ya Kibinadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kuimarisha ustahimilivu wa jamii dhidi ya majanga, huku akiwataka kuendelea kufuata taarifa na maelekezo rasmi kutoka kwa wataalamu na mamlaka zinazohusika na masuala ya maafa.” alisema

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema na kujenga ustahimilivu wa jamii ili kuongeza uwezo wa wananchi kukabiliana na majanga na kupunguza madhara yanayotokana na matukio hayo.

Amesema uwezo wa nchi katika kukabiliana na majanga kwa ufanisi unategemea uwepo wa mifumo madhubuti, uratibu na ushirikiano wa karibu na wenye tija kati ya Serikali na wadau wa huduma za kibinadamu.

Prof. Kabudi pia amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika kusimamia masuala ya kibinadamu na ustawi wa wananchi.

“Kupitia uongozi wa Rais Dkt. Samia, Serikali imeendelea kuhakikisha wananchi wanaokumbwa na changamoto za majanga wanapata msaada na faraja wakati wa dharura.”

Prof. Kabudi amewataka watoa huduma za kibinadamu kuwekeza zaidi katika kuwawezesha wananchi kwa elimu na taarifa sahihi kuhusu vihatarishi vinavyowazunguka, pamoja na hatua za kuchukua kabla, wakati na baada ya janga.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dk. James Kilabuko, amesema maadhimisho ya siku hiyo yanatoa fursa ya kutambua na kuthamini mchango wa watoa huduma za kibinadamu ambao hujitolea kwa moyo wa huruma, ujasiri na mshikamano katika kuokoa maisha na kupunguza madhara.

Amesema ni muhimu kuendelea kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa Serikali, wadau wa huduma za kibinadamu na jamii katika kuhakikisha kuwa msaada unapatikana kwa wakati na unawafikia wale wanaouhitaji.

“Ni muhimu kuhakikisha kuwa katika kila hatua ya utoaji wa huduma za kibinadamu, maisha, usalama na utu wa mwanadamu vinaendelea kuwa kiini cha hatua tunazochukua.”

Previous Post

WASIRA ATAKA WANA CCM WAKUTANE, WASIINGIE MKENGE KWA MANENO YA MITANDAONI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

ILANI MPYA YA CCM IMEZINGATIA  AMANI, USALAMA – DK. NCHIMBI

ILANI MPYA YA CCM IMEZINGATIA AMANI, USALAMA – DK. NCHIMBI

12 months ago
TUME ILIYOUNDWA NA RAIS DK. SAMIA ILIVYOBEBA MATUMAINI YA AMANI

TUME ILIYOUNDWA NA RAIS DK. SAMIA ILIVYOBEBA MATUMAINI YA AMANI

4 months ago

Popular News

  • PROF. KABUDI AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TAHADHARI ZA MAAFA

    PROF. KABUDI AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TAHADHARI ZA MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WASIRA ATAKA WANA CCM WAKUTANE, WASIINGIE MKENGE KWA MANENO YA MITANDAONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUTAENDELEA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA UKIMWI – YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KETE NGUMU SIMBA, PAMBA JIJI  

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MIAKA 50 YA UPUNGUFU WA MAFUTA YA KULA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?