• ePaper
Thursday, September 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KETE NGUMU SIMBA, PAMBA JIJI  

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 19, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
KETE NGUMU SIMBA, PAMBA JIJI  
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

KIKOSI cha Simba leo kinashuka dimbani katika mchezo namba mbili, kumenyana na Pamba Jiji katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba itakuwa ugenini kupepetana na Pamba Jiji katika mechi itakayopigwa   dimba la CCM Kirumba, Mwanza kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.

Timu hiyo yenye maskani yake Mtaa Msimbazi, Dar es Salaam, itajiuliza kwa Pamba huku ikiwa na kumbukumbu nzuri baada ya kuanza ligi msimu huu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, wakati Pamba Jiji ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Dodoma Jiji.

Katika msimamo, Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama tatu wakati Singida Black Stars inaongoza kwa pointi tatu sawa na Yanga, inayoshika nafasi ya pili zikitofautiana uwiano wa mabao ya kufunga.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Simba, Steve Barker, alisema timu yake inahitaji ushindi wa hali na mali kwa lengo la kutengeneza mazingira ya kuwa katika nafasi nzuri katika msimamo.

Barker alisema anaamini kikosi chake kitaingia dimbani kusaka pointi tatu kwa kucheza kwa utulivu huku kikisawazisha makosa madogo madogo yaliyojitokeza katika mechi ya awali.

“Pamba ina kikosi ambacho kimekuwa kikitoa upinzani mkali kinapocheza nyumbani, itailazimu kupambana, kucheza kwa kujihami na kutengeneza nafasi za kupata mabao,” alisema Barker.

Nyota wa timu hiyo, Kevin Nashon,  alisema maandalizi waliyofanya yanawapa sababu ya kujiamini kuwa wana uwezo wa kupata ushindi katika mchezo huo.

Alisema  kila mchezaji anamorari ya kutosha, kuhakikisha timu yao inaendeleza wimbi la ushindi.

 Kocha Msaidizi wa Pamba Jiji, John Waw, alisema timu yake imefanya maandalizi kwa ajili ya michezo yote ya ligi na si kuikabili Simba pekee.

 Waw alisema anajua Simba ina timu bora, yenye uchu wa ushindi lakini   atahakikisha anawaongoza wachezaji wake kupambana dakika zote 90. 

 Pamoja na Simba, Pamba kutoshana nguvu, michezo mingine ya ligi itazikutanisha Mbeya City na Dodoma Jiji zikipepetana Uwanja wa Sokoine, Mbeya wakati Kagera Sugar itacheza na Singida zitacheza Kaitaba.

Ligi Kuu msimu wa 2026/27, ilianza kutimua vumbi wiki iliyopita ambapo  Yanga ilianza kwa kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC huku  Singida Black Stars ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate FC huku Polisi Tanzania ikipata sare ya bao 1-1 ilipocheza na Azam FC.

Geita Gold yenye maskani mjini Geita ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City wakati Mashujaa FC ikipata ushindi wa bao 1-0 ilipoumana na Coastal Union huku JKT Tanzania ikipata sare ya bao 1-1 dhidi ya TRA United.

Previous Post

MIAKA 50 YA UPUNGUFU WA MAFUTA YA KULA

Next Post

TUTAENDELEA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA UKIMWI – YONAZI

Next Post
TUTAENDELEA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA UKIMWI – YONAZI

TUTAENDELEA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA UKIMWI - YONAZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA ANAVYOTAFSIRI ‘KAZI NA UTU’ KWA VITENDO

DK. SAMIA ANAVYOTAFSIRI ‘KAZI NA UTU’ KWA VITENDO

12 months ago
DK. SAMIA AFUNDA VIJANA

DK. SAMIA AFUNDA VIJANA

11 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?