• ePaper
Friday, January 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. NCHIMBI AELEZA MAFANIKIO YA KAMPENI ZA CCM NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 26, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. NCHIMBI AELEZA MAFANIKIO YA KAMPENI ZA CCM NCHINI

MGOMBEA Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi

0
SHARES
14
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA,
UKEREWE

MGOMBEA Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amefunga kampeni za Chama kwa kishindo huku akisema amezunguka takribani mikoa yote kwa mafanikio makubwa.

Katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Nchimbi, ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 na kumwombea kura za Urais, Dk. Samia Suluhu Hassan, wagombea ubunge na udiwani.

Dk. Nchimbi alisema hayo Nansio, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, alipohutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria ufungaji wa kampeni za Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

“Nimezunguka na wenzangu nchi nzima, mikoa takribani 27 kunadi Ilani ya Chama chetu, kumnadi Mgombea Urais wa Chama.

“Jambo ambalo tumelisema kwa mafanikio ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, ambayo imetekelezwa kwa miaka mitano ikiwa na utawala wa Dk. Samia ndani ya miaka minne na nusu.

“Tumeweza kulisema vizuri kwa sababu ya kazi kubwa ambayo Dk. Samia amefanya katika miaka hii minne na nusu,”alisema.

Alisema anajivunia kumalizia kampeni zake Ukerewe, sehemu aliyoitaja kuwa ngome muhimu na yenye historia kubwa ndani ya Chama.

“Nimefurahi kufanya mkutano wangu wa mwisho wa kampeni Ukerewe. Tulianza na kuzindua kampeni Agosti 28, mwaka huu, katika Uwanja wa Kawe, Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa mgombea wetu wa Urais, Dk. Samia na mamia walijitokeza kuunga mkono Chama Cha Mapinduzi,” alisema.

Alisema siku iliyofuata, Dk. Samia alikwenda mkoani Morogoro, naye alianzia kampeni zake jijini Mwanza,  Agosti 29, mwaka huu.

“Nilifurahi kuanzia Mwanza kwa sababu ni moja ya ngome zangu muhimu. Kwa hiyo, nimefurahi kuanzia kampeni Mwanza na kumalizia Mwanza, Ukerewe,” aliongeza huku akishangiliwa na mamia ya wananchi.

Alisema kwa kawaida, vitu visivyosahaulika katika kampeni ni mahali zilipoanzia na zilipomalizikia.

“Kila nitakapojiuliza kampeni za mwaka huu nilianzia wapi na kumalizia wapi, nitajibu nilianzia Mwanza na kumalizia Mwanza,” alisema.

UKEREWE WANAFANYA KAZI KWA BIDII

Akitoa shukrani kwa wananchi wa Ukerewe, Dk. Nchimbi, alisema rekodi zinaonesha kuwa, eneo hilo linaongoza kwa bidii ya kazi, asilimia 45 ya wananchi, wanajishughulisha na kilimo, asilimia 25 uvuvi na asilimia 10 ufugaji.

Alisisitiza historia ya kipekee ya Ukerewe ambayo imetoa viongozi wakubwa wa kitaifa, akiwemo Spika mstaafu, Pius Msekwa, ambaye alikuwa Katibu Mtendaji wa Kwanza wa CCM.

Alitaja viongozi wengine kutoka Ukerewe ni Getrude Mongella, aliyewahi kuwa Rais wa Bunge la Afrika na Mwenyekiti wa Mkutano wa Wanawake wa Beijing.

Anna Abdallah, licha ya kuwa mwenyeji wa Mkoa wa Mtwara, ni mke wa Mzee Msekwa na maskani yake ni Ukerewe.

“Nilipokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Mama Anna alinilea na kunifundisha namna ya kushiriki vikao vya juu vya Chama. Alinifundisha umuhimu wa kushirikiana kabla ya kupeleka hoja,” alisema.

APONGEZA KAZI ZA RAIS SAMIA

Dk. Nchimbi alisema Rais Dk. Samia, ameendelea kufanya kazi kubwa iliyotoa heshima kwake binafsi, Chama na wanawake wa Tanzania.

“Dk. Samia amesimamia miradi ya maendeleo, vilevile ameendesha vita iliyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere (Hayati Julius) ya kupambana na maadui wakuu watatu wa nchi yetu, maradhi, ujinga na umaskini.

“Amejenga miundombinu ya afya, elimu, mazingira ya biashara na kusimamia kukua kwa uchumi wetu,” alisema.

Alisema Dk. Samia, ametoa vibali na leseni za wafanyabiashara wapya nchini, kuliko wakati mwingine wowote.

Dk. Nchimbi, alisema wachimbaji wadogo waliopatikana ndiyo watakaokuwa wachimbaji wakubwa.

“Nataka kuwaambia tumepita tukiwa na nguvu ya kusema, wananchi wanatusikiliza na wanatambua kazi zilizofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya CCM, siyo kazi unazoweza kuzificha chini ya meza, kila mtu anaziona,” alisema.

Alisema kuwa, ndiyo maana kila walipokwenda wananchi walisema hawamdai Rais ila yeye ndiye anayewadai.

“Sisi ndiyo ametuahidi kila sehemu, nimesema Mwenyekiti wa Chama Wilaya na Mbunge wakumbushe watu wa Ukerewe hii habari ya kwamba, mtakuwa namba moja. Mjitahidi kwelikweli. Kwa sababu kila wilaya inataka kuongoza kwa kura za Rais Samia. Kura za mbunge na kura za madiwani wa CCM,”alisema.

AHADI ZA CCM UKEREWE

Aliahidi kuwa, Serikali ya CCM iwapo itapewa ridhaa ya kuongoza nchi miaka mitano ijayo, itaendelea kuimarisha amani na usalama, barabara, afya, elimu, kilimo na uvuvi.

“Tutaimarisha skimu za umwagiliaji, tutaendeleza ruzuku ya mbolea na mbegu, na kujenga skimu mbili mpya za kisasa Ukerewe,” alisema.

Kuhusu uvuvi, Dk. Nchimbi alisema serikali itajenga soko la kisasa la samaki na kiwanda cha kuchakata samaki na mazao yake pamoja kutoa mafunzo kwa wavuvi kutumia mbinu za kisasa.

Alisema serikali ya CCM itaboresha masoko ya Nansio, Katunguru, Sungura na Getrude Mongella huku ikihakikisha ndani ya miaka mitano kila kitongoji kinapata umeme.

“Tutaboresha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, kinamama wapike katika mazingira bora kwa afya zao,” alisema.

Aliahidi kuboresha Hospitali ya Nansio, kujenga vituo vya afya viwili katika Ngome na Bwiru, kukamilisha zahanati 16, kununua boti nne za wagonjwa na nyumba 10 za watumishi wa afya.

Aidha, sekta ya elimu nayo itanufaika kwa ujenzi wa shule za msingi sita, sekondari tatu, madarasa 320 na maabara za sayansi katika shule 43.

Pia, alisema upatikanaji wa maji safi na salama utaongezeka kutoka asilimia 70 hadi 85 ndani ya miaka mitano ijayo.

Vilevile, serikali itajenga zaidi ya kilometa 34 za barabara za lami katika maeneo ya Bukondo, Nansio, Katunguru, Bwisya na Kisiwa cha Ukara.

Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 29, mwaka huu na kukichagua Chama kwa ushindi wa kishindo.

Aliwaombea kura wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani.

SHANGWE NANSIO

Shughuli ya kufunga kampeni zilihudhuriwa na mamia ya wananchi waliovaa mavazi ya kijani na njano, wakiimba nyimbo za hamasa kuashiria utayari wa kupiga kura Oktoba 29, mwaka huu.

Msafara wa Dk. Nchimbi uliwasili Nansio saa tano asubuhi, ukipokelewa kwa shangwe na vijana wa bodaboda na viongozi wa Chama.

Kabla ya mkutano, Dk. Nchimbi alikwenda kumjulia hali Spika mstaafu, Mzee Msekwa, nyumbani kwake.

DK. SWITBERT MKAMA

Mgombea Ubunge Jimbo la Ukerewe kupitia CCM, Switbert Mkama, alimshukuru Dk. Samia kwa miradi mikubwa aliyoidhinisha wilayani humo zikiwemo sh. bilioni 25 kwa ujenzi wa Hospitali ya Rufani ngazi ya mkoa katika Wilaya ya Ukerewe, sh. bilioni 11 kwa vivuko viwili kati ya vine, hivi sasa viko tayari muda wote vitaanza kufanya kazi.

Previous Post

SIMBA, NSINGIZINI BALAA ZITO CAFCL

Next Post

DK. MWINYI AJAWA MATUMAINI KIBAO

Next Post
DK. MWINYI AJAWA MATUMAINI KIBAO

DK. MWINYI AJAWA MATUMAINI KIBAO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMULIZI YA RAIS DK. SAMIA ALIVYOWABEBA WANASIASA NJE 

SIMULIZI YA RAIS DK. SAMIA ALIVYOWABEBA WANASIASA NJE 

1 month ago
KIHONGOSI: TANZANIA HAIWEZI KURUDI UKOLONI

KIHONGOSI: TANZANIA HAIWEZI KURUDI UKOLONI

1 month ago

Popular News

  • MRADI WA UMEMEJUA KISHAPU KULETA MAPINDUZI SEKTA YA NISHATI – MAKAMBA

    MRADI WA UMEMEJUA KISHAPU KULETA MAPINDUZI SEKTA YA NISHATI – MAKAMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KATIBU MKUU CCM AWATAKA WANACHAMA KUSHIRIKI KIKAMILIFU VIKAO VYA MASHINA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TASAF ILIVYOCHOCHEA KILIMO, KUBADILI MAISHA YA WANANCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA ATEUA, ATENGUA VIGOGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MIGIRO AJA KIVINGINE CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?