• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIHONGOSI: TANZANIA HAIWEZI KURUDI UKOLONI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 7, 2025
in Habari, Kitaifa
0
KIHONGOSI: TANZANIA HAIWEZI KURUDI UKOLONI

KATIBU wa Halmadhauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi

0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesisitiza kuwa Tanzania haitarudi katika ukoloni.

Pia, kimewahimiza Watanzania kulinda amani ya taifa na kudhibiti nguvu za uchochezi unaoenezwa mitandaoni.

Vilevile, kimesema hakitasita kuwachukua hatua dhidi ya watu waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi iwapo watashindwa kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya wananchi wa Watanzania.

Kauli hiyo, ilitolewa na Katibu wa Halmadhauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi katika kikao chake na viongozi wa Chama na jumuiya zake wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofurika kumsikiliza.

“Wazee walipigania uhuru kwa gharama kubwa hivyo, jukumu la kizazi cha sasa ni kuendelea kuulinda na kuuthamini uhuru huo bila kuyumba.

“Amani iliyopo nchini siyo ya kubahatisha bali ni matokeo ya nidhamu, mshikamano na kazi ya kizalendo iliyoimarishwa kwa miongo mingi,” alisema uliohudhuriwa na maelefu ya wanachama.

Akizungumzia hali ya sasa ya siasa na usalama, Kihongosi alionya kuhusu juhudi za makusudi za baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii kupandikiza chuki, kutengeneza taharuki na kuchochea vurugu kwa maslahi binafsi.

Alisema wapo watu nje ya nchi, wakiwa salama na familia zao, lakini wanawashawishi Watanzania kuingia mitaani kufanya fujo na machafuko ambayo hatimaye yangewaumiza wananchi wa kawaida.

Kihongosi alisema tabia hiyo ni sawa na jaribio la kurudisha nchi katika mfumo wa kikoloni kwa njia za uchochezi, hivyo alisisitiza amani kwa taifa ni msingi mkuu wa uhuru.

Alisema kupotea kwa amani ni sawa na kupotea kwa uhuru, hivyo Watanzania hawapaswi kuruhusu mtu yeyote wa ndani au nje kuyumbisha misingi ya amani kwa visingizio vya kisiasa.

Aliwahimiza viongozi na wananchi kuendelea kuwaelimisha vijana na jamii kwa ujumla kuhusu thamani ya utulivu, umoja na mshikamano wa kitaifa.

“Tanzania ni nchi huru na itaendelea kubaki huru, hakuna nguvu ya nje wala ya ndani itakayoweza kuirudisha nchi kwenye enzi za ukoloni kwa jina lolote au kwa mbinu zozote,” alisisitiza.

Alisisitiza kuwa kulinda amani na uhuru ni wajibu wa kila Mtanzania, siyo serikali pekee, kila mmoja akatae kutumiwa kama chombo cha watu wenye ajenda zisizolenga maslahi ya taifa.

Kihongosi aliwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali, kutunza misingi ya amani na kuheshimu juhudi zinazofanywa na viongozi wa taifa katika kulinda umoja wa nchi.

Alisema Tanzania ni nchi ya watu huru na haitarudi katika mikono ya ukoloni, iwe kwa mabavu ya kisiasa, itikadi za kupandikizwa au propaganda za mitandaoni.

Alisema CCM ni baba wa demokrasia nchini kwa kuwa, ndicho Chama kilichoridhia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, hivyo alionya kuwa demokrasia hiyo kisiwe kigezo cha kuhatarisha amani.

WATUMISHI WABABAISHAJI

Kihongosi aliongeza kuwa CCM ni Chama cha watu wote na uthibitisho wa hilo ni uwepo wa viongozi kutoka makundi yote ya vijana, wazee, wanawake na watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Katibu huyo wa Itikadi aliwaeleza viongozi kuwa, hawana budi kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba Chama kitashirikiana na serikali kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ubora na thamani halisi ya fedha.

“Watumishi wa umma wanaokwamisha huduma watakumbana na nguvu ya Chama, sisi ni waajiri, hatutaacha mradi uuziwe kwa maneno, tutafuatilia hadi ngazi ya kata.

“Kuna baadhi ya watumishi wa umma wanasema Chama kinawafatafata, waambieni tuna wajibu wa kuwafuata kwa kuwa ilani inayotekelezwa ni yetu na tutawafuata kila wakati kuhakikisha wanafanya kazi iliyokusudiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Ikiletwa fedha ya kituo cha afya basi Chama kitakuja kukagua matumizi sahihi ya fedha hizo, hatutaacha kufanya hivyo kwa kuwa watumishi wazembe ndiyo wenye kusababisha CCM ionekane haifanyi kazi,” alieleza Kihongosi.

UCHOCHEZI MITANDAONI

Akizungumzia makundi ya uchochezi mitandaoni, Kihongosi alisema baadhi ya watu wameamua kugeuza majukwaa ya ‘internet’ kuwa chanzo cha chuki dhidi ya serikali, huku wakidanganya wananchi.

Alisema wachochezi hao wanawaita wahanga wa vurugu kuwa mashujaa, lakini wao hawajawahi kujitokeza kokote kuwaongoza moja kwa moja.

Kihongosi aliwataka viongozi wa vijana wa CCM, UWT, Wazazi na jumuia zote kutumia nguvu zao kueneza elimu ya uzalendo katika jamii, vijiweni na mitandaoni.

“Kama sisi wote humu ndani tukiamua kuingia mtandaoni kwa wakati mmoja, hakuna mtu atakayetupiku, tatizo tumeteleza, tumewaacha wachache wafanye kelele,” alisema.

Kihongosi alisema maendeleo hayawezi kumalizika siku moja kwa sababu idadi ya watu inaongezeka kila mwaka, hivyo alimpongeza Rais Dk. Samia kwa ustahimilivu hata kwa waliotenda makosa.

“Wengine wangekuwa jela milele, lakini Mama Samia amewasamehe, amewaruhusu warudi nyumbani, huo ni uthibitisho kwamba Rais anaongoza kwa utu, uzalendo na hekima,” alisema.

Kihongosi alisema CCM itaendelea kuwa nyumba ya Watanzania wapendao amani, haitasita kukemea, kuonya na kupambana na juhudi za kuvuruga utulivu wa nchi.

VIONGOZI WA CCM MKOA

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ alisema CCM haitafanya fujo bali itakuwa daraja kati ya serikali na wananchi na itasimamia umoja na mshikamano.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile, alimpongeza Dk. Samia kwa kauli za kishujaa za kuimarisha utulivu wa taifa, kuhimiza maadili ya kisiasa na kuwahakikishia wananchi amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo na ustawi wa taifa.

Alisema kauli hizo zimeleta hamasa kubwa kwa wanachama na wananchi, zikiwapa ujasiri wa kuendelea kulitumikia na kulilinda taifa kwa misingi ya upendo na nidhamu.

Previous Post

MATOLA AWAFUNGIA KAZI WASHAMBULIAJI SIMBA SC

Next Post

AZAM FC YAIZAMISHA SIMBASC

Next Post
AZAM FC YAIZAMISHA SIMBASC

AZAM FC YAIZAMISHA SIMBASC

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWIGULU AWAONYA MADEREVA WA SERIKALI

DK. MWIGULU AWAONYA MADEREVA WA SERIKALI

5 months ago
BARKER, IBENGE VITA YA MBINU ‘MZIZIMA DERBY’

BARKER, IBENGE VITA YA MBINU ‘MZIZIMA DERBY’

3 months ago

Popular News

  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AFICHUA KUWA NA KIPAJI CHA SOKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?