• ePaper
Saturday, November 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

WATANZANIA 37,647,235 KUPIGA KURA LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 28, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
WATANZANIA 37,647,235 KUPIGA KURA LEO

Upigaji Kura

0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WAANDISHI WETU

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza maandalizi yote muhimu ya Uchaguzi Mkuu wa wa Rais, Wabunge na Madiwani, yamekamilika.
Jumla ya wapigakura 37,647,235, wamethibitishwa kushiriki uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa INEC, Jaji Jacobs Mwambegele, amesema hayo kupitia taarifa ya tume hiyo na kusisitiza, uchaguzi huo, unafanyika kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 38(2)(a), 65 na 74(6)(b) na (d) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, zikisomwa pamoja na vifungu vya 49 na 58 (2) vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024.

Amesema upigaji kura, utafanyika kwa utaratibu wa kawaida, isipokuwa katika majimbo na kata zenye wagombea pekee wa ubunge au udiwani, ambapo wapigakura, watapiga kura ya ‘ndiyo’ au ‘hapana’.

Ameongeza karatasi za kura maeneo hayo, zimeandaliwa maalumu zikionesha jina na picha ya mgombea, nembo ya chama chake na visanduku viwili vya kuchagua ‘ndiyo’ au ‘hapana’.

Kuhusu kampeni za uchaguzi, Jaji Mwambegele alieleza vyama vya siasa, wagombea na wananchi kwa ujumla wameendesha kampeni kwa amani na ustaarabu, kasoro chache zilizojitokeza zimeshughulikiwa kwa mafanikio na kamati za maadili ngazi mbalimbali.

“Kwa mwaka huu wa uchaguzi, jumla ya wapiga kura 37,647,235 wamethibitishwa kushiriki, kati yao 36,650,932 wako Tanzania Bara na 996,303 Zanzibar. Wapigakura wanawake ni 18,950,801 sawa na asilimia 50.34 na wanaume 18,696,434 sawa na asilimia 49.66.

“Jumla ya majimbo ya uchaguzi ni 272, ambapo Tanzania Bara ina majimbo 222 na Zanzibar 50.

Majimbo 270 yatafanya uchaguzi wa wabunge leo, huku majimbo mawili ya Siha (Bara) na Fuoni (Zanzibar) yakipangiwa Desemba 30, mwaka huu kutokana na vifo vya wagombea,” alisema.

Kwa upande wa madiwani, Jaji Mwambegele amesema kata 3,945 kati ya 3,950 ndizo zitakazoshiriki uchaguzi leo, huku tano zikifanya

uchaguzi Desemba 30, mwaka huu na Januari 5, mwakani kutokana na sababu maalumu.

Amesema kwa mara ya kwanza katika historia ya uchaguzi wa Tanzania, Tume imeruhusu wapigakura 8,277 kupiga kura ya Rais katika vituo tofauti na walivyojiandikisha, hatua iliyotokana na mabadiliko ya kikatiba na kisheria.

Pia, Tume imeruhusu wafungwa wanaotumikia vifungo visivyozidi miezi sita, wanafunzi wa Vyuo vya Mafunzo Zanzibar na mahabusu kupiga kura ya Rais katika vituo maalumu vya magereza na vyuo vya mafunzo.

“Kwa ujumla, vituo 99,895 vitatumika kote nchini, ambapo 97,348 vipo Tanzania Bara na 2,547 Zanzibar. Vyama 17 vimesimamisha wagombea wa urais na makamu wa rais, huku 18 vikiwa na wagombea wa ubunge na udiwani.

“Takwimu zinaonesha kuwa wagombea wa urais ni 17, wakiwemo wanawake watatu sawa na asilimia 17.65 na wanaume 14 sawa na asilimia 82.35.

Kwa wagombea wa makamu wa rais, wanawake ni tisa na wanaume wanane,” alisema.

Aidha, amesema wagombea wa ubunge ni 1,729 wakiwemo wanawake 558 (sawa na asilimia 32) na wanaume 1,171 (68%). wagombea wenye ulemavu ni 27 sawa na asilimia 1.56. Kwa udiwani, wapo wagombea 7,239, wakiwemo wanawake 718 (10%) na wanaume 6,521 (90%).

Jaji huyo amesema wapigakura watakaokuwa na vitambulisho vya NIDA, leseni ya udereva au pasi ya kusafiria wataruhusiwa kupiga kura endapo taarifa zao zitapatikana katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Amesema vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi alasiri, huku vituo vya magereza na vyuo vya mafunzo vikifunguliwa saa mbili na kufungwa saa tisa.

Amesisitiza wapigakura walioko mstari muda wa kufunga vituo wataruhusiwa kupiga kura.

Mwenyekiti huyo amesema mpiga kura asivae sare za vyama, kufanya kampeni au kukaa ndani ya mita 300 kutoka kituo cha kupigia kura siku ya uchaguzi na kusisitiza upigaji kura ni wa siri kwa mujibu wa sheria.

Amesema baada ya kupiga kura, wapiga kura wanapaswa kuondoka vituoni kuepuka msongamano, huku mawakala wa vyama wakisimamia maslahi ya wagombea wao.

Amewataka Watanzania kudumisha amani, uzalendo na utulivu wakati wa uchaguzi, akisisitiza kila mmoja ana wajibu wa kulinda heshima na amani ya Taifa.

ULINZI UMEIMARISHWA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, amewahakikishia Watanzania wote kuwa, ulinzi na usalama, umeimarishwa nchi nzima,

hivyo wajitokeze kwa wingi kushiriki kupiga kura kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.

Bashungwa aliyasema hayo mkoani, Mwanza jana na kuwahakikishia wananchi kuwa, hakutakuwa na shida yoyote.

“Kesho (leo) Oktoba 29, hakutakuwa na shida yoyote. Vyombo vya usalama, vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi, vipo timamu nchi nzima.

“Usalama umeimarishwa, kwa hiyo, Watanzania twende tukapige kura bila kuwa na wasiwasi, yeyote atakayethubutu kuvuruga amani, atakutana na kisiki,” alisisitiza Bashungwa.

Pia, alitoa wito kwa vijana, kujitokeza kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo na kuwataka kujiepusha na vitendo au vishawishi vyovyote,

vinavyoweza kuvuruga amani na kuwahakikishia kuwa, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imebainisha fursa nyingi mahsusi kwa vijana.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoani wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, aliwataka wananchi wa mkoa huo, kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani.

Alisema wamejipanga vizuri, kuhakikisha amani, utulivu na usalama, vinatawala muda wote kipindi cha kupiga kura hadi utangazaji matokeo.

Akizungumza jana baada ya kufanya doria za magari, miguu na mbwa wa Polisi kuzunguka maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya, Kamanda Kuzaga, aliwataka wananchi kujitokeza kupiga kura.

Kuzaga alisisitiza kuwa, wananchi wapuuze maneno ya uongo, upotoshaji, taarifa zisizo sahihi zinazotolewa kupitia mitandao ya kijamii kuhamasisha vurugu na vitendo vya uvunjifu wa amani, hivyo aliwahakikishia usalama.

Alisema jeshi hilo, halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani, utulivu na usalama.

MSEMAJI WA JESHI LA POLISI

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi nchini, limewahakikishia wananchi kuwa kuna usalama wa kutosha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa leo.

Aidha, limesema hakuna tishio lolote la kiusalama kama taarifa za awali zilivyotolewa Oktoba 26, mwaka haku.

Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alisema hayo, kupitia taarifa ya jeshi hilo na kuwatahadharisha wananchi kuwa, kuna kikundi cha watu baada ya kuona wameshindwa kuvuruga amani ya nchi, wameunda kikundi cha vijana ambao wanaandaa picha mjongeo na taarifa mbalimbali za matukio yaliyotokea siku za nyuma, ambayo yalishashughulikiwa na mengine ya kutunga wayasambaze katika mitandao ya kijamii yaonekane yametokea kipindi hiki au muda mfupi uliopita.

Alisema wananchi wakiona taarifa kama hizo katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vingine vya habari vilivyoandaliwa na watu hao wenye nia ovu na amani ya taifa, watambue ni za uongo, uzushi na za kutaka kutuchonganisha na kugombanisha.

Aliongeza pia wapo walioandaliwa kama ambavyo baadh wameshajitokeza kuzungumza na kutoa taarifa zenye tungo tata, zenye kutaka kuleta taharuki.

“Pia wanakusanya matukio ambayo yalitokea nchi zingine na kuyatengeneza kwa kuyawekea sauti zenye lafudhi ya Kiswahili yaonekane yametokea nchini mwetu na wakati huu muhimu tunapoelekea kupiga kura kesho (leo).

“Wamepanga kuchukuwa picha za baadhi ya viongozi na kuziwekea maneno na sauti zenye matamko ya upotoshaji ionekane wao ndiyo. wanayazungumza au wanayatamka wakati siyo kweli; alisema.

Alisema taarifa kama hizo au vipeperushi na mengine yanayofanana na hayo Watanzania wanatakiwa kuyapuuza kwani yameandaliwa kwa nia ovu ya kihalifu kwa lengo la kutaka kuleta taharuki kwa wananchi.

Alisisitiza atakayetumiwa taarifa kama hizo, asisambaze kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya makosa ya kimtandao badala yake zifutwe.

“Tarifa sahihi zinazohusu jambo lolote zitatolewa na mamlaka zenye wajibu wa kufanya hivyo,” alisema.

Previous Post

KISHINDO SIKU 60 ZA DK. SAMIA

Next Post

RAIS DK. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA NCHINI

Next Post
RAIS DK. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA NCHINI

RAIS DK. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AAHIDI NEEMA TANGA AKIPEWA RIDHAA YA KUONGOZA NCHINI

DK. SAMIA AAHIDI NEEMA TANGA AKIPEWA RIDHAA YA KUONGOZA NCHINI

2 months ago
ILANI MPYA YA CCM IMEZINGATIA  AMANI, USALAMA – DK. NCHIMBI

ILANI MPYA YA CCM IMEZINGATIA AMANI, USALAMA – DK. NCHIMBI

2 months ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KETE YA KWANZA KWA GAMONDI STARS LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAGIZO MATATU KWA DK. NCHEMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI MARIDHIANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.