• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MIAKA 64 YA UHURU YAWAIBUA BAYI, RAGE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 9, 2025
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
MIAKA 64 YA UHURU YAWAIBUA BAYI, RAGE

MZEE RAGE

0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na VICTOR MKUMBO

WAKATI leo ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 64, tangu Tanzania ilipopata Uhuru, wadau wa michezo nchini Filbert Bayi na Ismail Aden Rage wamefunguka mambo mbalimbali kuhusu mafanikio ya sekta hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao walisisitiza kwamba kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta ya michezo nchini tangu Tanzania ilipopata Uhuru wake.

Mwanariadha mkongwe Bayi, amesema sekta ya michezo imepiga hatua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka 64 ya Uhuru hadi hivi sasa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Amesema kwa upande wa riadha mafanikio yapo kwa wachezaji binafsi huku katika mpira wa soka klabu na timu za taifa zimepiga hatua zaidi kwani serikali iliyopo madarakani imafamya kazi kubwa kuendeleza michezo.

“Ndani ya miaka 64 ya Uhuru, michezo imepiga hatua kwa upande wa riadha mchezo huo unaendelea kufanya vizuri kutokana na serikali kutoa sapoti ya kutosha kwa wachezaji mmoja mmoja.

“Katika soka pia tumeona klabu na timu za taifa zikituwakilisha vyema katika michuano mbalimbali, kitu ambacho kinatia moyo japokuwa kuna baadhi ya vyama wameshindwa kufanya vyema kutokana na viongozi wao kutokuwa na mikakati mizuri,” alisema Bayi.

Bayi ambaye aliwahi kuwika katika mchezo wa riadha mwaka 1974 kwa kushinda mashindano ya dunia kwa mbio za mita 1,500 huku mwaka uliofuata akitikisa katika Michezo ya Jumuiya ya Madola, alisema kuna kipindi kulikuwa na wachezaji wengi wakishiriki michuano mikubwa ikiwemo Olimpiki lakini walishindwa kufanya vizuri.

Hata hivyo, Bayi aliiomba serikali kuendelea kutoa sapoti katika michezo ili kutanua wigo wa kusaidia vyama kuhakikisha fedha zinaendelea kutolewa za kutosha ili timu ziendelee kufanya vyema.

“Angalia mchezo wa riadha, kwani tumeona hivi karibuni Alphonce Simbu alifanya vyema na kurejea nchini akiwa na medali ya dhahabu, hiyo ni historia kubwa kwani ni juhudi binafsi za mchezaji lakini serikali iliweka nguvu zake, naamini vipaji vilivyopo hivi sasa vikizingatiwa vizuri, vitaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika michuano mbalimbali ya kimataifa,” alisema Bayi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Rage alisema kuna mafanikio makubwa katika sekta ya michezo.

Alisema kipindi anacheza soka, mwaka 1974, Simba ilipata mafanikio makubwa baada ya kutinga nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika, hivi sasa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), mafanikio ambayo hayajawahi kufikiwa na timu nyingine zaidi ya Simba.

Alisema katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imekuja na mafanikio zaidi katika mchezo wa soka ikiwemo kuutengea bajeti ya kutosha.

Alisema hivi sasa serikali imeufanya mchezo wa soka kuonekana ni moja ya ajira kwa kutengeneza miundombinu bora ikiwemo kujenga viwanja na hamasa ya ‘Goli la Mama’ imekuwa chachu kwa wachezaji kujituma zaidi.

“Tumeona serikali chini ya Rais Dk. Samia ilivyofanya mambo makubwa ikiwemo ujenzi na ukarabati wa viwanja kuhakikisha mchezo wa soka unachezwa katika sehemu zenye viwango bora.

“Klabu na timu za Taifa zinazocheza michuano ya kimataifa zimekuwa zikinufaika na ‘Goli la Mama’ kimsingi ni hamasa kubwa inayowafanya wachezaji wazidi kujituma zaidi tofauti na sisi tulikuwa tukiingia uwanjani tunaangalia umati wa watu ndiyo tunahamasishana kutafuta ushindi,” alisema Rage.

Previous Post

CHAMBUA: DUBE KAMA MAYELE

Next Post

TASAF KIELELEZO CHA MAFANIKIO MIAKA 64 YA UHURU

Next Post
TASAF KIELELEZO CHA MAFANIKIO MIAKA 64 YA UHURU

TASAF KIELELEZO CHA MAFANIKIO MIAKA 64 YA UHURU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

BONDIA MWAKYEMBE AMKUBALI MMALAWI

BONDIA MWAKYEMBE AMKUBALI MMALAWI

3 months ago
TRA IMEANZA KUTEKELEZA  MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KARATU

TRA IMEANZA KUTEKELEZA  MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KARATU

1 month ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?