• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MZEE KIMITI, HAMAD WAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU TUME YA JAJI CHANDE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 28, 2025
in Habari, Kitaifa
0
MZEE KIMITI, HAMAD WAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU TUME YA JAJI CHANDE
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

MWANASIASA mkongwe Mzee Paul Kimiti na Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha ADC, Hamad Rashid, wametoa rai kwa Watanzania kuwapuuza baadhi ya watu wanaochochea wananchi wasitoe maoni katika Tume ya Rais ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani Oktoba 29.

Wamesema kuundwa kwa tume hiyo ni wajibu wa kikatiba, hivyo wanaohamasisha wananchi wasitoe ushirikiano kwa tume hiyo hawalitakii mema Taifa.

Kauli hizo zimekuja ikiwa imepita siku moja tangu Tume ya Rais ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi, kubaini uwepo wa watu wanaoshawishi wananchi kutotoa ushirikiano.

Akizungumza na UHURU, Hamad Rashid alisema ni wajibu wa Watanzania kutoa ushirikiano kwa tume hiyo, kwani si mara ya kwanza serikali kuunda tume, ambapo  mwaka 2001 Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa aliunda kwa ajili ya kuchunguza vurugu Zanzibar.

“Matukio ya Oktoba 29 hakuna aliyefurahia, hivyo  kuundwa kwa tume ni wajibu wa kikatiba, niwaombe Watanzania wawapuuze watu ambao halitakii mema Taifa letu, wawapuuze wale wote wanaochochea wananchi wasishiriki kutoa maoni,” alisema.

Kwa mujibu wa Rashid, watu wanaoshawishi wananchi wasishiriki kutoa maoni wanaweza kuwa wanahusika na vurugu hizo na wanapaswa kufuatiliwa.

Mwanasiasa mkongwe na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kimiti, aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu kutoa maoni kwa tume hiyo ili iweze kukamilisha uchunguzi wake.

Kauli ya Tume

Desema 26 mwaka huu Tume ya Rais ya kuchunguza matukio ya vurugu wakati na baada ya uchaguzi, ilisema imebaini kuwepo kwa watu au makundi ya watu yanayoshawishi wananchi kutotoa ushirikiano, ikiwemo kutoa maoni, ushahidi au taarifa kwa namna yoyote ile.

Taarifa hiyo ilisema ushawishi huo hausaidii jitihada za kitaifa za kutafuta ukweli, haki, kujifunza kutokana na yaliyopita na kuweka misingi ya suluhu ya kudumu.

Iliwashauri wananchi kupuuza ushawishi wowote unaolenga kuwazuia kushiriki, badala yake watoe maoni.

“Kupitia sauti za wananchi, Taifa linaweza kutambua changamoto zilizojitokeza, kuzitatua na kuchukua hatua za kuhakikisha matukio kama haya hayajirudii siku zijazo,” ilisema taarifa hiyo.

Pia taarifa hiyo ilifafanua kwamba tume hiyo ipo kwa ajili ya Watanzania wote na mafanikio ya kazi yake yanategemea ushiriki mpana, wa hiyari na wenye uwazi kwa wananchi.

Novemba 18 mwaka huu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliunda tume hiyo baada ya kutokea kwa vurugu na uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 29.

Hatua hiyo ilikuwa ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa wakati akihutubia Bunge la 13 Jijini Dodoma, ambapo aliahidi kuunda tume huru ya kuchunguza tukio hilo.

Tume hiyo inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Othuman Chande, wajumbe wa tume hiyo ni aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Balozi Dk.Tergomena Tax, Jaji Mkuu Mstaafu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue.

Wengine ni Balozi Paul Meela, Balozi David Kapya, Mwanadiplomasia Balozi Radhia Msuya, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Said Mwema.

Previous Post

DK. GWAJIMA AONYA ‘WATU WAZIMA OVYO’ MITANDAONI

Next Post

 WAZIRI GWAJIMA AANIKA MIZIZI YA UKATILI NCHINI

Next Post
 WAZIRI GWAJIMA AANIKA MIZIZI YA UKATILI NCHINI

 WAZIRI GWAJIMA AANIKA MIZIZI YA UKATILI NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

‘BODA BODA KWANGU NI ZAIDI YA KAZI INAYONIWEKA MJINI’

2 months ago
KIBANO WALIOHARIBU SARUJI MIFUKO 1,262

KIBANO WALIOHARIBU SARUJI MIFUKO 1,262

1 month ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?