• ePaper
Friday, January 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Biashara

TRA INAVYOIMARISHA USHIRIKIANO NA WAFANYABIASHARA KUKUZA UCHUMI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 6, 2026
in Biashara, Makala
0
TRA INAVYOIMARISHA USHIRIKIANO NA WAFANYABIASHARA KUKUZA UCHUMI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

TANGU kuingia madarakani kwa serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imesaidia kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hakika kazi kubwa imefanyika ya kuongeza makusanyo ya kodi kupitia TRA, hivyo kufanikisha dhima ya serikali ya utekelezaji wa maendeleo kwa wananchi na taifa. 

Hayo yanatokana na usikivu wa TRA, kwa maagizo ya Rais Dk. Samia aliyoyatoa wakati akimwapisha Kamishina Mkuu wa Mamlaka hiyo, Yusuph Mwenda.

Wakati huo, Rais Dk. Samia alimwelekeza Mwenda kuboresha ukusanyaji wa mapato uwe kwa hiari siyo kwa mashinikizo ya nguvu.

Hatua hiyo, iliwezesha ongezeko la ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ndani ya mwezi na hadi mwaka.   

Hali hiyo, imejidhihirisha katika taarifa za TRA, ambazo wanazitoa mara kwa mara, ikiwemo ile ya Mwezi Oktoba hadi Desemba ambayo ilitolewa hivi karibuni.

Katika taarifa hiyo ya TRA, ilieleza kuwa katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana, ilikusanya jumla ya sh. trilioni 9.8, huku mwezi Desemba pekee, ikikusanya sh. trilioni 4.13, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Kamishna Mkuu, Mwenda alieleza kwamba mafanikio hayo yanatokana na utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk. Samia ya kukusanya kwa njia shirikishi ya kuimarisha mahusiano mazuri na wafanyabiashara kote nchini.

Pia, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi, jambo ambalo limeendelea kutoa tija ya ongezeko la ukusanyaji kodi.

 WAFANYABIASHARA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Hamis Livembe, alitaja siri ya kuongeza kasi ya ulipaji kodi, kuwa ni uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji iliyopo na kutotozwa kodi kwa mabavu.

Alisema chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia wafanyabiashara wanafanya shughuli zao bila bughudha na TRA inakusanya kodi kistaarabu bila kutumia nguvu.

Pia, Livembe alisema hatua ya TRA kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato imechangiwa na sera nzuri zilizopo na uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji.

“Hatua hii inatokana na sera nzuri na ustaarabu unaoendelea katika ukusanyaji kodi tofauti na awali,”alisema.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema sababu nyingine iliyowafanya wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi kwa hiyari ni uwepo wa mazingira bora ya kufanya biashara yaliyowekwa na serikali.

Hata hivyo, Livembe aliomba serikali kuendelea kupanua zaidi bandari ili kuongeza zaidi fursa za kukua kwa biashara.

Aliomba serikali kuendelea kusaidia urahisishaji wa upatikanaji wa mikopo kwa wafanyabiashara, hatua ambayo itasaidia kukuza mitaji na kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi.

TRA

Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Yusuph Mwenda, alisema katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka jana mamlaka imefanikiwa kukusanya sh. trilioni 4.13.

Alisema mapato hayo yamepanda ikilinganishwa na sh. trilioni 3.5 zilizokunywa kipindi kama hicho mwaka 2024.

Alieleza katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desema mwaka jana mamlaka imekusanya jumla ya sh. trilioni 9.8

Mwenda anasema ukusanyaji huo wa sh. trilioni 9.8 umevuka lengo lililokusudiwa ambalo lilikuwa sh. trilioni 9.6.

“Kiasi hiki ni kikubwa na ni mara ya kwanza hakijawahi kukusanywa na TRA kwa mwezi mmoja, mwaka jana mwezi kama huo (Desemba 2024) tulikusanya  shilingi trilioni 3 na bilioni 500,”alisema.

Vilevile Kamishina Mkuu wa TRA alisema wastani wa ukusanyaji kodi kwa mwezi umepanda kutoka sh. trilioni 2.7, hadi kufikia sh.trilioni 3.130 kwa mwezi.

Kamishina Mwenda, alisema sababu za mafanikio hayo ni uhimilivu wa uchumi uliyopo nchini, sera za uchumi, ulipaji kodi kwa hiyari na mfumo mzuri wa kodi uliyojengwa.

“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais (Dk. Samia Suluhu Hassan) kwa kujenga uchumi himilivu, mwezi Oktoba pamoja na changamoto hatukushuka  kiwango tulichotakiwa kukusanya na mwezi Novemba hatukushuka,”aliongeza.

Hata hivyo, Kamishna Mwenda alisema katika kipindi cha mwaka huu TRA imejipanga kusimamia sheria za kodi, kupambana na wakwepa kodi wote, na kuendelea kusimamia uadilifu kwa watendaji wa mamlaka hiyo.

Pia, Kamishna Mwenda alitaja sababu nyingine zilizochangia mafanikio hayo ni jitihada za utendaji kazi mzuri wa watumishi wa TRA.

“Tutaimarisha sana watumishi wetu na kusimamia uadilifu katika utendaji kazi.”aliongeza

Aidha, Kamishna Mwenda alisema TRA imejipanga kuboresha huduma zake, ambapo inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa kodi za ndani utakao anza Januari mwaka huu.

“Kupitia mfumo huo mambo mengi yatafanyika online ule usumbufu wa walipa kodi kwenda kwenye ofisi zetu utapungua sana.

“Tutakuwa na maamuzi ya kikodi ambayo ni data base tofauti na awali,”alisema Kamishna Mwenda.

Alisema mfumo huo utafanywa zaidi kidijitali hatua ambayo itarahisisha utendaji kazi, kuboresha huduma kwa walipa kodi na kuondoa malalamiko.

Kamishna Mwenda aliongeza kuwa TRA itaendelea kushirikiana na walipa kodi kwa kuwezesha katika shughuli zao za biashara na kuendelea kuwasikiliza.

Mwenda alito rai kwa wananchi kuendelea kulipa kodi kwa hiyari, kwa mustakbali wa maendeleo ya taifa.

WACHUMI

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Profesa Haji Semboja, alisema ongezeko la makusanyo hayo linaashiria uwepo wa sheria na sera nzuri na kupanuka kwa uchumi wa nchi.

“Hii ni ishara kwamba uchumi wetu unakuwa na umepanuka, tuna sheria nzuri na mfumo wa kitaasisi wa TRA ni mzuri na miundombinu inayohitajika kwa sababu ya hiyo TRA hawakuwa wazembe,”alisema

Vilevile Profesa Semboja, alishauri serikali kuendelea kuwa na matumizi sahihi ya kodi ikiwemo, kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu.

Naye Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), Profesa Abel Kinyondo alisema ongezeko la mapato hayo yanaashiria uwepo wa ufanisi ndani ya TRA.

“Uchumi wetu umekuwa vizuri na kuna ufanisi ndani ya TRA, lakini lazima tujue kukusanya fedha ni jambo moja na fedha hizo kutumika maeneo sahihi kubadilisha maisha ya watu ni jambo lingine, kwa hiyo tuongeze ufanisi wa matumizi ya fedha hizo,”alisema.

Pia, Profesa Kinyondo alishauri serikali kuendelea kuongeza ufanisi katika matumizi ya kodi hizo, ikiwemo maeneo yanayogusa moja kwa moja wananchi, walipe kodi zaidi na kukuza uchumi.

“Mwananchi akitoa kodi na akiona inatumika katika maeneo yanayomgusa zaidi atatoa zaidi kodi, kuongeza mnyororo waendelee kuvunja rekodi kodi zitumike vizuri,”alisema.

Naye Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) Dk. Timothy Lyanga alisema ongezeko la makusanyo hayo unaonesha namna serikal ilivyofanikiwa kudhibiti ukwepaji kodi.

Dk. Lyanga alishauri serikali kuendelea kubuni miradi mbalimbali itakayochangia mzunguko wa fedha kuwa mkubwa zaidi, ikiwemo ujenzi wa viwanda.

Alisema ongezeko hilo la trilioni 4 katika kipindi cha mwezi mmoja unaonesha sekta mbalimbali za uchumi zimeanza kuchangia kikamilifu katika utoaji kodi

Aidha Dk. Lyanga alisema kupaa kwa makusanyo hayo kunaleta faida katika utekelezaji wa miradi kirahisi, ikiwemo ya miundombinu.

Aidha Julai 31 mwaka 2024, Rais Dk. Samia, aliunda tume ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini, ambayo iliongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue.

Rais Dk. Samia alizindua tume hiyo Oktoba 4 mwaka 2024, Ikulu Dar es Salaam huku akiwataka TRA kuhakikisha kila anayepaswa kulipa kodi alipe kodi stahiki, kwani hakuna aliye juu ya sheria.

Aidha, Juni 16 mwaka 2025 wakati akifungua jengo la TRA Mkoa wa Simiyu, Rais Dk. Samia aliwataka TRA kukusanya kodi kirafiki bila kutumia nguvu au kufunga akaunti za wafanyabiashara

“Nilimwambia Yusuph (Kamishna wa TRA) na kupeleka TRA, mfanyabiashara asiwe adui yako awe rafiki yako, ameweza kulipa alipe hajaweza ana madeni muite zungumza naye kirafiki…lakini ile ya kumnyang’anya kompyuta kufunga vitabu hapana,”alisema.

Previous Post

SERIKALI ZANZIBAR YAONGEZA TEKNOLOJIA KUDHIBITI MAKOSA YA BARABARANI

Next Post

BILIONI 1/- KUWAPANDISHA ULINGONI MWAKINYO, KIDUKU

Next Post
BILIONI 1/- KUWAPANDISHA ULINGONI MWAKINYO, KIDUKU

BILIONI 1/- KUWAPANDISHA ULINGONI MWAKINYO, KIDUKU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI AITEKA RORYA | WANANCHI WATHIBITISHA KUTIKI OKTOBA  29 KWA KISHINDO

DK. NCHIMBI AITEKA RORYA | WANANCHI WATHIBITISHA KUTIKI OKTOBA  29 KWA KISHINDO

4 months ago
DK. SAMIA : TUNATAKA USHINDI WA HESHIMA

DK. SAMIA : TUNATAKA USHINDI WA HESHIMA

4 months ago

Popular News

  • MRADI WA UMEMEJUA KISHAPU KULETA MAPINDUZI SEKTA YA NISHATI – MAKAMBA

    MRADI WA UMEMEJUA KISHAPU KULETA MAPINDUZI SEKTA YA NISHATI – MAKAMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KATIBU MKUU CCM AWATAKA WANACHAMA KUSHIRIKI KIKAMILIFU VIKAO VYA MASHINA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TASAF ILIVYOCHOCHEA KILIMO, KUBADILI MAISHA YA WANANCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA ATEUA, ATENGUA VIGOGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MIGIRO AJA KIVINGINE CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?