• ePaper
Sunday, February 1, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Biashara

YANGA, AL AHLY MECHI YA MAAMUZI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 30, 2026
in Biashara, Habari, Kimataifa, Michezo
0
YANGA, AL AHLY MECHI YA MAAMUZI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAKATI timu ya Yanga ikitarajiwa kushuka dimbani kesho katika mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly, uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa huo ni mchezo wao wa maamuzi, hivyo hawatakubali kupoteza.

Yanga wanatarajiwa kushuka dimbani kesho katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL),  dhidi ya Al Ahly ya Misri, utakaochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni.

Timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Twiga na Jangwani, itashuka dimbani huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza 2-0 katika mechi iliyopita iliyofanyika Uwanja wa Al Salam, Cairo, Misri.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema mechi hiyo ndiyo itatoa maamuzi ya timu yao kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya CAFCL.

Alisema kuwa walipoteza ugenini, hivyo hawatakubali kupoteza nyumbani kwani watapambana kwa kila hali kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Kamwe alisema kuwa wachezaji wote wapo tayari na wana morari ya kutosha kuelekea katika mchezo huo na kila mmoja ameahidi kupambana na kutimiza majukumu yake uwanjani.

“Huu ni mchezo wetu wa maamuzi, tunahitaji kupata ushindi kwa namna yoyo ili kujihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali ya CAFCL msimu huu,” alisema Kamwe.

Kamwe alisema benchi la ufundi limeona makosa waliyofanya katika mechi iliyopita na kuyafanyia kazi kuhakikisha wanaibuka na ushindi wakiwa uwanja wa nyumbani na kuwapa raha mashabiki wao.

Alisema kikosi tayari kilishawasili Zanzibar kuhakikisha wanafanya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo huo.

Hata hivyo aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuhakikisha wanawapa sapoti wachezaji wao ili kuibuka na ushindi.

“Mashabiki ndio nguzo muhimu katika mchezo wetu na Al Ahly, kwani watawaongezea morari wachezaji ili kupata ushindi, tunawaomba wajitokeze kwa wingi,” alisema.

Katika msimamo wa kundi B, Yanga inashika nafasi ya pili kwa pointi nne Al Ahly ipo kileleni kwa pointi saba, AS FAR ikishika nafasi ya tatu kwa pointi mbili sawa na JS Kabylie inayoburuza mkia, timu zote zimeshashuka dimbani mara tatu.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

Next Post

NMB YAONGEZA  MAGARI MAALUMU YA HUDUMA ZA KIFEDHA

Next Post
NMB YAONGEZA  MAGARI MAALUMU YA HUDUMA ZA KIFEDHA

NMB YAONGEZA  MAGARI MAALUMU YA HUDUMA ZA KIFEDHA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

2 months ago
BOUANGA MATUMAINI KIBAO

BOUANGA MATUMAINI KIBAO

1 month ago

Popular News

  • MAKONDA ASISITIZA KUTOVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE AFCON

    MAKONDA ASISITIZA KUTOVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE AFCON

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NMB YAONGEZA  MAGARI MAALUMU YA HUDUMA ZA KIFEDHA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, AL AHLY MECHI YA MAAMUZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PAPA LEO XIV APOKEA UJUMBE WA RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?