• ePaper
Wednesday, August 19, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WASIRA ATAKA WANA CCM WAKUTANE, WASIINGIE MKENGE KWA MANENO YA MITANDAONI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 19, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WASIRA ATAKA WANA CCM WAKUTANE, WASIINGIE MKENGE KWA MANENO YA MITANDAONI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu – Singida

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amewataka wanachama wa CCM kukutana mara kwa mara katika vikao rasmi vya chama ili kujadili masuala muhimu na kuepuka kupotoswa na taarifa zisizo na ukweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza leo Agosti 19, 2026 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wakati wa kuanza ziara rasmi ya kikazi ya kukagua uhai wa chama, Wasira amesema vikao hivyo vinawapa wanachama fursa ya kupata taarifa sahihi na kuambizana ukweli.

“Wanachama wetu nchi nzima, kwa mujibu wa Katiba mna vikao vya wanachama. Mkutane muambizane. Siku hizi kwenye mitandao kuna uongo mwingi sana. Usipoangalia unaweza hata wewe kushirikishwa kusema uongo,” amesema.

Amesisitiza kuwa ni muhimu wanachama kukutana na kujadili madai yanayosambaa, kisha kumtafuta mtu mwenye ujuzi awasaidie kuyafafanua.

“Kwa hiyo ni vizuri kukutana mkasema hili jambo limesemwa sana, maana yake ni nini? Mkamwita mtu anayejua akawasaidia kufafanua,” ameeleza.

Makamu Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa mikutano ya wanachama ni fursa muhimu ya kujadili masuala yanayoendelea nchini ili waweze kukitetea chama ipasavyo.

Kuhusu uhuru na umoja wa nchi, Wasira amesema CCM itaendelea kulinda urithi huo uliopatikana kwa kazi kubwa.

“Hii ndiyo CCM. Kazi ya kwanza tulipewa ni uhuru na tunalinda. Ya pili ni umoja na tunahakikisha unabaki. Yeyote anayetaka kuubomoa anabomoa msingi ambao hawezi. Anaweza kutikisa matawi lakini mizizi itabaki chini,” amesema.

Ameongeza kuwa wapo wanaodai CCM haijatekeleza chochote tangu uhuru, jambo ambalo amelisema ni kinyume na ukweli.

“Wanasema hatujafanya chochote tangu uhuru. Lakini uhuru wa kusema ndio huo walionao. Mdomo una kazi mbili: kusema na kula. Mtu akisema hakuna chochote tangu uhuru, muache tu. Huyo ana matatizo anahitaji msaada,” amehitimisha.

Previous Post

TUTAENDELEA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA UKIMWI – YONAZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MIGOGORO ARDHI MFUPA MGUMU

MIGOGORO ARDHI MFUPA MGUMU

5 months ago
DK. SAMIA ASEMA MIAKA MITANO IJAYO, SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YAO

DK. SAMIA ASEMA MIAKA MITANO IJAYO, SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YAO

11 months ago

Popular News

  • WASIRA ATAKA WANA CCM WAKUTANE, WASIINGIE MKENGE KWA MANENO YA MITANDAONI

    WASIRA ATAKA WANA CCM WAKUTANE, WASIINGIE MKENGE KWA MANENO YA MITANDAONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUTAENDELEA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA UKIMWI – YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KETE NGUMU SIMBA, PAMBA JIJI  

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MIAKA 50 YA UPUNGUFU WA MAFUTA YA KULA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA BWAWA LA JULIUS NYERERE YA CHALINZE – DODOMA IMEKAMILIKA: MRAMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?