• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

MAELFU WAFURIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM DAR

admin by admin
August 28, 2025
in Habari, Uchaguzi
0
MAELFU WAFURIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM DAR
0
SHARES
15
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MUSSA YUSUPH

DAR ES SALAAM imeitika. Maelfu ya wakazi wa jiji hili walifurika katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, kushuhudia uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uzinduzi huo wa kihistoria ulitikisa jiji la kibiashara na vitongoji vyake, ukidhihirisha namna CCM inavyoendelea kukubalika, ikiwa ni matokeo ya utekelezaji bora wa Ilani ya Chama chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye ndiye mgombea urais kupitia CCM.

Wananchi walianza kumiminika viwanjani hapo kuanzia saa mbili asubuhi, huku eneo lote likipambwa na mabango makubwa yaliyobeba ujumbe wa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, ikiwemo miradi ya afya, elimu, kilimo na miundombinu.

Hadi kufikia saa nane mchana, viwanja vyote vilifurika, shangwe, nderemo na vifijo vikitawala kutoka kwa wanachama, wakereketwa na wapenzi wa chama hicho kikongwe.

Katika kunogesha tukio hilo, wasanii wa muziki na vikundi mbalimbali vya burudani walitumbuiza, akiwemo Mbosso aliyetikisa jukwaa kwa kibao chake cha Pawa, pamoja na Marioo, AY, Chege, Madee, Missomsindo, Vajana Jazz, vikundi vya dansi, singeli na tamthilia.

Kadhalika, viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walihudhuria akiwemo Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wassira, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asharose Migiro.

Ilipotimu saa 14:18, mgombea mwenza Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi aliwasili, akifuatiwa na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Shangwe ziliendelea pale Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Kenan Kihongosi, alipompandisha jukwaani Diamond Platnumz na bendi ya TOT kuimba wimbo maalum wa kumkaribisha mgombea urais wa CCM, Dk. Samia.

Msafara wa Dk. Samia ulisindikizwa na vijana wa UVCCM waliopanda pikipiki za kijani, huku tukio hilo likioneshwa mubashara kupitia runinga kubwa. Saa 14:43, Rais Dk. Samia aliingia uwanjani ndani ya gari la kijani, akishangiliwa kwa wimbo maarufu Namleta Rais na miamvuli ya kijani yenye nembo za CCM.

Baada ya kuwasili, alielekea moja kwa moja katika jukwaa kuu, ambapo alisalimu maelfu ya wananchi waliompokea kwa shangwe kubwa. Burudani iliendelea, Diamond akiendelea kulitawala jukwaa kwa kibao chake cha Iyenaiyena CCM Namba Moja.

Previous Post

SIRI YA AZAM FC HADHARANI

Next Post

DK. SAMIA AELEZA VIPAUMBELE SIKU 100 ZA KWANZA AKIWA RAIS

Next Post
DK. SAMIA AELEZA VIPAUMBELE SIKU 100 ZA KWANZA AKIWA RAIS

DK. SAMIA AELEZA VIPAUMBELE SIKU 100 ZA KWANZA AKIWA RAIS

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI IMEIMARISHA BARABARA – DK. SAMIA

SERIKALI IMEIMARISHA BARABARA – DK. SAMIA

1 month ago
DIAMOND, HARMONIZE, MISO MISONDO WATIKISA UZINDUZI KAMPENI CCM

DIAMOND, HARMONIZE, MISO MISONDO WATIKISA UZINDUZI KAMPENI CCM

2 months ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.