LONDON, England
TIMU za soka za Liverpool na Arsenal, leo zinatarajiwa kupambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Pambano hilo, limepangwa kufanyika katika Uwanja wa Anfield ambapo Liverpool itakuwa mwenyeji wa mchezo huo.
Hadi leo, Arsenal inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi sita baada ya kushuka dimbani mara mbili katika michuano hiyo.
Liverpool katika ligi hiyo, ipo nafasi ya tatu katika msimamo huo, ikiwa na pointi zake sita baada ya kucheza mechi mbili tangu msimu huu wa 2025/26 ulipoanza hivi karibuni.
Katika msimamo huo, timu ya Tottenham ipo nafasi ya pili ikiwa na alama sita baada ya kushuka dimbani mara mbili katika ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.
Hata hivyo, baadhi ya mechi ambazo Liverpool imecheza imeonesha udhaifu katika safu ya ulinzi licha ya kupachika mabao saba katika mechi zao mbili za kwanza katika ligi.
Katika pambano la leo kati ya Liverpool na Arsenal, macho ya mashabiki yatakuwa kwa
Timu ya Arsenal ipo katika hali tete ya kuwakosa Kai Havertz ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti.
Pia, kocha wa Arsenal, Arteta yupo katika muda mgumu kufuatia Bukayo Saka na Martin Odegaard kuwa na majereha huenda wasiwepo katika mchezo dhidi ya Liverpool.
Viktor Gyokeres anastahili kupata nafasi nyingine ya kuanza mchezo huo dhidi ya Liverpol huku Jeremie Frimpong, atakosa pambano hilo la leo.
Mechi nyingine zitakazo fanyika leo ni Brighton & Hove Albion itapambana na Manchester City, Nottingham Forest itacheza na West Ham.
Pambano jingine litakuwa kati ya timu za Aston Villa dhidi ya Crystal Palace.
Liverpool huenda ikawakilishwa na Alisson, Bradley, Konate, Van Dijk, Kerkez, Szoboszlai, Gravenberch, Salah, Wirtz, Gakpo na Ekitike.
Arsenal: Raya, Timber, Saliba, Gabriel, Calafiori, Eze, Zubimendi, Rice, Madueke, Gyokeres na Martinelli.