LONDON,
England
TOTTENHAM Hotspur inaendelea na kazi kubwa ya kutaka kumsajili beki wa Manchester City, Manuel Akanji.
Imeeleza kuwa timu hiyo ya England, imepania kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
Hata hivyo, Tottenham inaweza kukutana na upinzani kutoka kwa klabu za AC Milan na Crystal Palace kupata sahihi yake.
Timu zote zinawania saini ya mchezaji huyo kwa ajili ya kumsajili aweze kuichezea timu moja wapo kati ya hizo.
Manuel Akanji hivi karibuni alikataa ofa ya kujiunga na timu ya Galatasaray.
Alikanusha taarifa hizo zilizokuwa zimeenea kuwa yupo mbioni kutua nchini Uturuki.
Hata hivyo, nyota huyo ameweka wazi kwamba bado anatafakari mustakabali wake na Manchester City.
Manuel Obafemi Akanji ni mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Uswisi ana mkataba na klabu ya Man City.
Mlinzi huyo alizaliwa Neftenbach nchini Uswisi,Julai 19, mwaka 1995 amefikisha miaka 30.
Alijiunga na Manchester City, mwaka 2022 amewahi kuichezea timu ya Borussia Dortmund.
Akanji alitua katika kikosi cha B orussia mwaka 2018 akitokea Uswisi.
(Gazetta Dello Sport)
CHELSEA KUIBOMOA BARCA
CHELSEA ipo tayari kutoa ofa nono kunasa saini ya Fermin Lopez.
Timu hiyo ya England inamtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 mwenye thamani pauni milioni 78 ndani ya klabu ya Barcelona FC.
(Mundo Deportivo)
WEST HAM YAINGIA VITANI
KLABU ya West Ham imeingia vita ya kusaka saini ya Fabio Vieira kutoka Arsenal.
Hata hivyo, West Ham itakutana na upinzani kutoka kwa timu ya Stuttgart na klabu nyingine zinazoshiriki Bundesliga kumnasa kiungo huyo Mreno mwenye miaka 25.
(Sky Sports Germany)
RB LEIPZIG YAVAMIA LIVERPOOL
TIMU ya RB Leipzig imevamia klabu ya Liverpool kutaka kumsajili kiungo na England, Harvey Elliott.
Mchezaji huyo anaichezea timu ya Taifa ya England U21, huenda akaziba nfasi ya Xavi Simons, hata hivyo RB Leipzig bado inasita kutoa uamuzi juu ya dau linalotakiwa na Liverpool.
(ESPN)
BOYOMO HUYOO ASTON VILLA
ASTON Villa inatarajiwa kukamilisha uhamisho wa beki wa Osasuna,Enzo Boyomo.
Mlinzi huyo ana miaka 23 ni raia wa Cameroon huenda akanunuliwa na Aston Villa kwa pauni milioni 21.25. (The Telegraph)