• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Biashara

BILIONI 499/- ZAPATIKANA KUPITIA UTALII

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 12, 2025
in Biashara, Habari, Kitaifa
0
BILIONI 499/- ZAPATIKANA KUPITIA UTALII
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu 

IDADI ya watalii wanaotembelea vivutio mbalimbali Tanzania imeongezeka kutoka 786,710 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hadi kufikia 1,493,135 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kuchangia zaidi ya sh. bilioni 499 katika pato la Taifa.

Kamishna Msaidizi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), July Lyimo, alisema hayo jijini Arusha alipowasilisha mada katika Kikao Kazi cha Wadau wa Haki Jinai katika uhifadhi wa Wanyamapori.

Alisema mwaka wa fedha 2016/2017, watalii waliingizia Taifa jumla ya sh. 187,889,184,373, huku mapato hayo yakiongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikia sh. 499,895,848,371.95 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

“Kwa mwaka wa fedha 2023/2024, ukusanyaji wa mapato ulikuwa sh. 410,665,187,391.96 na makadirio ya mapato kwa mwaka wa fedha 2024/2025 yalikuwa sh. 430,556,220,982.99, mapato yaliyopatikana yalikuwa sh. 499,075,308,953.63. Makadirio ya mapato kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ni sh. 600,181,999,994,” alisema.

Lyimo alisema mapato hayo, yamepatikana kutokana na vivutio mbalimbali, huku Mbuga ya Serengeti ikiongoza kwa asilimia 53.47, ikifuatiwa na Mlima Kilimanjaro wenye asilimia 20.80 na mbuga ya Tarangire ikishika nafasi ya tatu kwa asilimia 11.90.

Alisema vivutio vingine na namna vilivyochangia mapato ni Lake Manyara asilimia 4.10, Nyerere asilimia 2.79, Arusha asilimia 2.10, Mikumi asilimia 1.97, Ruaha asilimia 1.10, Saadani asilimia 0.50, Mkomazi asilimia 0.27 na hifadhi nyingine asilimia moja.

Alisema TANAPA wana mikakati mbalimbali ambayo itasaidia kuvutia watalii na kuongeza mapato, ikiwemo kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara za utalii na viwanja vya ndege, malazi, madaraja na kuboresha malazi ya bei nafuu ya soko la ndani na nje.

Alitaja mikakati mingine ni kuvutia wawekezaji katika sekta ya utalii ndani ya Hifadhi za Taifa kukidhi mahitaji ya watalii wa hadhi zote (malazi, mazao ya utalii) na kutangaza vivutio vya utalii katika masoko ya ndani na nje ya nchi kwa kutumia njia mbalimbali, yakiwemo maonesho, matamasha, kampeni maalumu, mikutano mikubwa, shuleni, Taasisi mbalimbali, watu maarufu na michezo (Marathon).

Pia, kuendelea kubuni mazao mapya ya utalii kuongeza mapato, kuongeza idadi na aina ya wanyamapori na kufanya upembuzi yakinifu na kubaini hifadhi za kuongeza idadi na aina ya wanyamapori kuvutia watalii zaidi katika hifadhi zenye upungufu.

Alisema kuna aina mbalimbali za vivutio vya utalii Tanzania, ikiwemo aina mbalimbali za wanyama, wingi wa wanyama, upekee wa wanyama katika eneo, wanyama wakubwa watano, uhamaji wa nyumbu kwa kuvuka mto Mara na Grumet na kuzaa kwa wakati mmoja (Zebra, Thomson Gazell Eland).

Vivutio vingine ni milima kama Mlima Kilimanjaro, Meru, Fukwe za Bahari na Maziwa, Wanyama adimu na hatarini kutoweka (Mkomazi na Serengeti) na uwanda wa kuvutia ndege mbalimbali na maua.

Previous Post

NLD KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

Next Post

SIKUKUU YA BURUDANI

Next Post
SIKUKUU YA BURUDANI

SIKUKUU YA BURUDANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

Uchumi wa Tanzania unaendelea kukua kwa asilimia 6.8

2 months ago
DK. SAMIA AACHA GUMZO SONGEA AKIAHIDI NEEMA TELE

DK. SAMIA AACHA GUMZO SONGEA AKIAHIDI NEEMA TELE

3 weeks ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.