• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

NCHIMBI : NIDHAMU NGUZO KUIMARISHA DEMOKRASIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 15, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Toleo Maalumu
0
NCHIMBI : NIDHAMU NGUZO KUIMARISHA DEMOKRASIA

Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA,

Tanga


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimevunja ukimya na kusema nidhamu ndani ya Chama ni nguzo muhimu ya kuimarisha demokrasia.

Amesisitiza kuwa, uteuzi wa wagombea ndani ya CCM, huzingatia vigezo vya uongozi, uaminifu na muda mwafaka, siyo matokeo ya kura za maoni.

Hayo yalielezwa Soni, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga, jana na Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

Alikuwa akiwahutubia mamia ya wananchi waJimbo la Bumbuli katika mkutano wa kampeni kumwombea kura za urais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Dk. Nchimbi alisema CCM inaendelea kuimarika kwa kufuata misingi imara ya uongozi na siasa.

“Uongozi ni kupeana kijiti. Unaweza usiteuliwe leo, ukapewa nafasi kubwa zaidi baadaye. Mimi mwenyewe niligombea uspika mwaka 2015, sikuteuliwa, leo hii ni miaka 10 baadaye, nimeteuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM.

“Hii ndiyo maana ya nidhamu ndani ya demokrasia,”alisema Dk. Nchimbi.

Alisema kila mwanachama wa CCM, anapaswa kuelewa kuwa, nafasi za uongozi siyo haki ya mtu,bali dhamana, hivyo ni muhimu kila mwanachama akajenga moyo wa kukubali uamuzi kwa heshima na unyenyekevu.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu utakaofanyikaOktoba 29, mwaka huu, Dk. Nchimbi, alisema mfumo wa vyama vingi na uchaguzi huru nchini,unatoa fursa kwa vyama kuwasimamisha wagombea,baadae kumteua mtu kwa kila nafasi.

“CCM ina wanachama zaidi ya milioni 13.4 waliosajiliwa kielektroniki, kila mmoja ana haki ya kugombea.

“Nafasi ni moja kila kata, jimbo au taifa. Tunapofanya uteuzi, siyo kwamba wengine hawafai, inakuwa safari hii ni zamu ya mwingine,” alisema.

“Katika nchi yetu, tuna utaratibu wa demokrasia ya vyama vingi na demokrasia ya uchaguzi, kila baada ya miaka mitano, tunafanya uchaguzi, mwaka huu ni miaka mitano inayokuja lazima tufanye uchaguzi.

“Kwa hiyo, katika ngazi ya umma, kila chama cha siasa, kinapeleka wagombea wakajinadi, wakajieleze na wakaeleze yaliyotokea nyuma wanayotaka kufanya baadaye,” alisema.

WAPONGEZWA KWA UZALISHAJI

Balozi Dk. Nchimbi aliwapongeza wananchi wa Lushoto kwa kuleta maendeleo kupitia kilimo huku zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa eneo hilo, akitegemea kulima.

“Viungo, matunda, mboga, misitu, uvuvi, biashara ndogondogo na madini vinapatikana hapa. Hongereni, mnatupa heshima kubwa,” alisema.

Alisema Lushoto ni sehemu muhimu kwa uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara nchini.

Pia, alitumia fursa hiyo kuwapelekea salamu kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama, Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Mgombea Urais wa CCM.

“Dk. Samia amenituma niwape salamu za upendo na mshikamano na kuwashukuru kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kipindi chote cha uongozi wake,” alisema.

MAJIMBO YOTE TANGA CCM

Alisema viongozi wa CCM mkoani Tanga akiwemo Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa, Rajabu Abdulrahman na Katibu Mkuu mstaafu wa Chama, Yusuf Makamba kuwa, majimbo yote ya mkoa huo yatachukuliwa na CCM.

“Tumeungana kujenga Chama chetu na nchi yetu. Na matarajio yangu ni kwamba, hapa kwa wakwe zangu, tutapata kura zote za Dk. Samia, mbunge na diwani,” alisema.

MAKAMBA ANENA

Balozi Dk. Nchimbi alimpigia simu Katibu Mkuu mstaafu, Makamba akiwa jukwaani na kuwaombawananchi wa Jimbo la  Bumbuli mkoani Tanga, kumchagua Dk. Samia, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Mhandisi Ramadhani Singano na madiwani wote wa Chama.

Makamba alisema anaimani na wagombea wote wa CCM na alipenda kuhudhuria mkutano huo, kutokana na changamoto ya afya hakuhudhuria na kuwataka wakazi wa wa Mkoa wa Tanga, wasimwangushe katika uchaguzi huo.

MOMBO

Akiwa katika mkutano wa kampeni Mombo, Korogwe Vijijini, Dk. Nchimbi, aliwasisitiza wananchi wa maeneo hayo hawana deni kwa Dk. Samia bali anawadai kutokana na maendeleo makubwa aliyowafikishia.

“Rais wetu amegusa kila eneo elimu, afya, kilimo, uvuvi, umeme, biashara na miundombinu.

“Hili halihitaji mjadala, ni kazi kubwa inayozungumza yenyewe,” alisema.
Kwa mujibu wa Dk. Nchimbi, kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM itaongezwa mara dufu endapo Chama kitaendelea kuaminiwa kuongoza dola.

Alisema katika kipindi kijacho iwapo watapewa ridhaa ya kuongoza nchini, watatekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Korogwe Vijijini ikiwemo uboreshaji wa hospitali ya wilaya kufikia hadhi ya wilaya kwa majengo, vifaa, madaktari na wauguzi.

MNZAVA

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia CCM, Timotheo Mnzava, alisema serikali ya CCM imefanya kazi kubwa na hivi sasa ni muda wa kurudisha heshima kwa kupiga kura kwa wingi.

“Watu wa Korogwe Vijijini na Mombo tumejipanga. Hatuna deni, serikali ya CCM imefanya kazi  katikaelimu, afya, umeme, barabara. Tumejiandaa kutoa kura za heshima kwa Rais Samia, mbunge na diwani,” alisema.

AWESO

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, aliwahakikishia wananchi kuwa, serikali imepeleka sh. bilioni 900 kwa mradi wa maji, ambao utekelezaji wake ulichelewa na hivi sasa utakamilika.

“Baada ya dhiki huja faraja. Faraja ni CCM, Samia, Nchimbi na serikali yetu. Nawahakikishia kazi hii itakamilika haraka,” alisema.

Previous Post

MSIGWA : DK. SAMIA AMETHIBITISHA UWEZO WAKE WA UONGOZI

Next Post

KISHINDO CHA DK. SAMIA MIKOA 10

Next Post
KISHINDO CHA DK. SAMIA MIKOA 10

KISHINDO CHA DK. SAMIA MIKOA 10

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI ITAIMARISHA TIBA ZA KITALII – DK. MPANGO

SERIKALI ITAIMARISHA TIBA ZA KITALII – DK. MPANGO

1 month ago
DK. MWINYI ATANGAZA NEEMA WAZEE ZANZIBAR

DK. MWINYI ATANGAZA NEEMA WAZEE ZANZIBAR

4 weeks ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.