• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. SAMIA : UTAKUWA UCHAGUZI WA AMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 20, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA : UTAKUWA UCHAGUZI WA AMANI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Pemba 

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa wananchi kutokubali kuhatarisha amani ya nchi kwa sababu ya uchaguzi.

Dk. Samia ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, amesisitiza wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, mwaka huu, kwani vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kikamilifu kulinda amani.

Amesema katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, baadhi ya watu wanatamani kuvuruga amani, hivyo ametoa wito kwa wananchi kutokubali kuchokozeka.

Dk. Samia alisema hayo, alipohutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Gombani ya Kale, Mkoa wa Kusini Pemba na kubainisha Oktoba 29, mwaka huu, hakutakuwa na vurugu yoyote, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kutimiza takwa la kidemokrasia kwa kuchagua viongozi wanaowataka.

“Msichokozeke, kuweni kama mimi mama yenu, dada yenu na bibi yenu. Mimi ninachokozeka sana, lakini sikubali kuchokozeka. Tusiende kuvunja amani ya nchi, tutunze amani na utulivu. Tunapochokozwa tusichokozeke.

“Tarehe 29 Oktoba hakutakuwa na vurugu, vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vema kulinda nchi na ninayezungumza hapa ni Amiri Jeshi Mkuu,” alisisitiza.

Dk. Samia alisema serikali katika kipindi cha miaka mitano iliyopita imejitahidi kusimamia utulivu wa kisiasa na amani, ambapo hakuna vurugu zilizosikika.

“Wenzetu wanayolalamikia hakuna lisilozungumzika. Tutakaa tutazungumza, tusiende kuleta vurugu kuvunja amani kwa sababu hili halikufanyika. Tukapige kura, turudi nyumbani tusubiri matokeo,” alisema Dk. Samia huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi.

SERIKALI YA VITENDO

Katika hotuba yake, Dk. Samia alisisitiza serikali za CCM ni za vitendo na siyo maneno.

Alisema Pemba kila kukicha imekuwa ikibadilika, ikiwa ni matokeo ya miradi ya maendeleo inayopelekwa kisiwani humo.

“Serikali za CCM vinafanya kazi kwa vitendo na siyo blah..blah…kila nikija Pemba mambo yanaendelea kubadilika,” alieleza.

Alitaja baadhi ya miradi mikubwa inayotekelezwa ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege Pemba ambao utakuwa wenye hadhi ya kimataifa.

Dk. Samia alisema uwanja huo baada ya kukamilika ndege kubwa za abiria na mizigo zitatua, hivyo kufungua zaidi uchumi wa Pemba.

Alisema watalii na ndege za mizigo watafika moja kwa moja Pemba badala ya kutua Unguja.

Mgombea huyo wa urais alitaja miradi mingine ni ujenzi wa barabara ya Chake Chake-Mkoani ambao fedha zake zimeshapatikana.

Pia, alisema ujenzi wa Bandari ya Shumba utarahisisha shughuli za uchukuzi baina ya Pemba na Mombasa, hatua ambayo itaondoa changamoto ya usafiri.

Alisema wakazi wa maeneo hayo watatumia boti za kisasa badala ya usafiri wa vidau ambavyo usalama wake ni mdogo.

Vilevile, alisema kisiwa hicho kimenufaika kupitia ujenzi wa shule za ghorofa ikiwemo eneo la Kojani.

“Na ndiyo maana tunapata ujasiri kwa kujiamini kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena. Tunaamini tumefanya makubwa, tupeni mitano mingine tufanye makubwa zaidi.

“Tunafanya kazi kustawisha maisha ya wananchi. Mtu akifanya kazi ipasavyo atapata ujira kisha kufanya maendeleo. Kazi na utu maana yake ni kusonga mbele,” alisisitiza.

NISHATI SAFI

Dk. Samia alisema Serikali ya Muungano na ya Zanzibar zinafanya kazi pamoja kukabiliana na changamoto za kidunia.

Alitaja baadhi ya miradi ni wa kulinda maeneo ya ardhi yasiharibiwe na bahari hali inayochangiwa na uharibifu wa mazingira duniani.

Kutokana na hilo, alisema serikali imekuwa ikisisitiza matumizi ya nishati safi ikiwa ni mkakati ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanapikia kwa nishati safi.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Hemed Suleiman Abdullah, alisema miradi yote iliyotekelezwa Pemba ni sehemu ya utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

“Kama kuna jambo kubwa la kuliheshimu nchini ambalo Dk. Samia anaendelea kusimamia ni umoja na mshikamano nchini. Zamani Pemba haikuwa hivi lakini hivi sasa ni kwa sababu ya umoja, mshikamano na upendo ikiwa ni sehemu ya falsafa ya 4R.

“Pemba mtandao wake unaweza kuunganishwa hadi Mombasa kupitia Bandari ya Shumba na Tanga. Uimarishaji wa miundombinu unalenga kuimarisha ustawi wa familia,” alisema.

Alisema wananchi wa kisiwa hicho wana imani kubwa na Dk. Samia kutokana na kukifungua kiuchumi.

Hemed alibainisha Dk. Samia amekuwa msimamizi mzuri wa fedha za serikali, kwani kila eneo la nchi kuna wakandarasi wanaotekeleza miradi.

MRATIBU WA KAMPENI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Mratibu wa kampeni kisiwani Pemba, Mohammed Aboud, alieleza wana-CCM wanaposema miaka mitano tena wanamaanisha.

“Umetufanyia mengi mazuri katika miaka minne, tumeona maono, utu, uvumilivu na umakini katika kufanya uamuzi kwa nchi yetu,” alisema.

Aliongeza: “Umelinda misingi ya uhai wa taifa, umelinda mapinduzi na mafanikio yake, umeulinda muungano wetu. Tunakushukuru ulivyotimiza wajibu wako, Watanzania wanaishi pande zote bila bughudha.”

Alisema kubwa zaidi ni falsafa ya maridhiano ambayo wananchi wameona namna Dk. Samia alivyosimamia amani na utulivu, ambapo wananchi wanapata nafasi ya kujitafutia riziki kuendesha maisha yao kutokana na utulivu uliopo.

“Leo Watanzania tunaheshima kubwa kila tunapokwenda duniani wanatuuliza unatoka kwa Samia. Hii ni kwa sababu ya juhudi zako kutuunganisha kimataifa,” alieleza.

Alisisitiza utalii umekua Zanzibar kupitia filamu ya Royal Tour jitihada ambazo zimeleta manufaa makubwa na kuwasisitiza Watanzania kumpigia kura Dk. Samia, Dk. Hussein Ali Mwinyi, wabunge, wawakilishi na madiwani wote wa CCM.

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA KUSINI PEMBA

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba, Yusuph Ali Juma, alisema mengi kuhusu mafanikio ya uongozi wa Dk. Samia yameelezwa.

Hata hivyo, alisema katika mkoa huo wamepata hospitali ya mkoa yenye ghorofa mbili na ujenzi wa matenki matatu ya maji, ambayo yapo Chanjani, Dodo na Kiwani. Kila tenki lina uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja.

WAGOMBEA UBUNGE

Mgombea wa ubunge Jimbo la Mkoani, Profesa Makame Mbarawa, alieleza Dk. Samia amefanya kazi kubwa kwa maslahi ya wananchi kutoka pande zote za muungano.

Mbarawa alisema Dk. Samia alihakikisha upatikanaji fedha za ujenzi uwanja wa ndege Pemba ambao utakuwa na hadhi ya kimataifa, ukikamilika urefu wake itakuwa ni kilometa 2.5 na jengo lenye uwezo wa kuhudumia abiria 350,000 kwa mwaka.

“Maana yake Pemba itakwenda kufunguka kwa utalii na uwekezaji. Uwanja huu utagharimu shilingi bilioni 500. Hii ni historia,” alibainisha Profesa Mbarawa.

Pia, alisema serikali itaanza ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 43.5 kutoka Chakechake hadi Mkoani itakayokuwa na njia nne.

“Kutafungwa taa za barabarani na kujengwa njia ya watembea kwa miguu, miradi hiyo itagharimu sh. bilioni 800,” alisema.

Kwa upande wake, mgombea ubunge Jimbo la Kojani, Hamad Hassan Chande, alieleza kisiwa hicho kimenufaika na miradi mbalimbali, akitolea mfano ujenzi wa uwanja wa ndege Pemba na barabara ya Chakechake -Mkoani.

“Pia serikali imetenga zaidi ya bilioni 300 kugharimia ujenzi wa Bandari ya Mkoani itakayosaidia kuimarisha shughuli za uchukuzi Pemba… Oktoba 29 tutakwenda kutiki umetafsiri kwa vitendo ilani ya CCM,” alisema Chande.

Mgombea ubunge viti maalumu, Mariamu Mwinyi, alisema wananchi wa Pemba, hususan wanawake, wamenufaika kupitia mradi wa kuwezesha kaya maskini (TASAF).

Alisema mradi huo umewezesha uanzishwaji wa vikundi vya wajasiriamali, kusomesha watoto, kilimo na uvuvi ambavyo wanawake wamenufaika.

“Makundi yote tumenufaika kupitia mradi wa TASAF ambao umetokana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alieleza.

Naye, mgombea ubunge viti maalumu, Asia Omar, alisema CCM kimeendelea kupika viongozi wengi wanawake ambao wamefuata nyayo za Dk. Samia.

“Uwezeshaji hasa wanyonge wamenufaika na dhahiri umeona umati mkubwa umefika hapa kwa mapenzi yao. Umeonesha nia kwa vitendo hakuna mtu mwenye wasiwasi kusubiri ajira za serikali,” alisema.

Mgombea Uwakilishi, Jimbo la Chonga, Suleiman Makame, alisema fedha za Uviko-19 zaidi ya sh. bilioni 200 zilitumika kuimarisha huduma za afya na ustawi wa wananchi.

“Nilipata fursa kusimamia sh. bilioni 36 zilizotumika kuwanufaisha wananchi zaidi ya 200,000 kupitia uchumi wa buluu. Fedha hizi pia ziliwagusa kina mama na vijana ndiyo maana unaona wananchi wameitika kwa wingi. Tutaendelea kukuunga mkono,” aliongeza Makame.

Previous Post

DK. SAMIA ANAVYOTAFSIRI ‘KAZI NA UTU’ KWA VITENDO

Next Post

MGOMBEA URAIS CCM KURINDIMA RUVUMA LEO

Next Post
MGOMBEA URAIS CCM KURINDIMA RUVUMA LEO

MGOMBEA URAIS CCM KURINDIMA RUVUMA LEO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CCM INASHINDWAJE KIGOMA – DK. SAMIA

CCM INASHINDWAJE KIGOMA – DK. SAMIA

1 month ago
DK. MWINYI ATAKA KODI, TOZO NDOGO

DK. MWINYI ATAKA KODI, TOZO NDOGO

1 month ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.