Na HANIFA RAMADHANI,
Zanzibar
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kukamilika miradi mikubwa ya kimataifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, kutaufanya mkoa huo kutokuwa na tofauti na Mkoa wa Mjini.
Amesema hivi karibuni kutaanza ujenzi wa bandari kubwa ya kisasa ya kimataifa katika eneo la Mangapwani na ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nungwi, eneo la Kigunda.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni katika uwanja wa Shangani, Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
“Baada ya bandari ya Mangapwani na uwanja wa ndege Nungwi kukamilika, huu Mkoa wa Kaskazini Unguja hautakuwa na tofauti yoyote na mikoa ya mjini kwa maendeleo na jinsi utakavyofunguka,” alisema.
Alisema miradi hiyo ya kimataifa ambayo itaufanya Mkoa wa Kaskazini Unguja, kufunguka katika kila sekta kwa sababu kutakuwa na milango mikuu ya kuingia na kutoka katika visiwa vya Zanzibar.
Alisema serikali imejipanga kujenga barabara zote za Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwemo ya Mkwajuni hadi Matemwe, Mkwajuni-Kijini na Kinyasini-Kiwengwa.
Alisema lengo ni kuhakikisha kunakuwa na muunganiko baina ya mkoa mmoja kwenda mwingine.
“Mambo yatakuwa mazuri sana katika kipindi kinachokuja, tutahakikisha tunamaliza tuliyoanza pamoja na kuanza miradi mingine mipya,” alisema Dk. Mwinyi.
Alisema serikali imeimarisha huduma za kijamii za ujenzi wa skuli, hospitali za wilaya na mkoa ambazo zimeanza kujengwa eneo la Mahonda.
Alisema serikali imedhamiria kuanza mradi mkubwa wa upatikanaji wa maji safi na salama katika mkoa wa Kaskazini ambako hivi karibuni mradi huo unatarajiwa kuanza.
DK. DIMWA
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Mohammed Said Mohammed ‘Dimwa’, alisema Dk. Mwinyi ni kiongozi mtulivu, mnyenyekevu na madhubuti.
Alisema mgombea huyo ni miongoni mwa viongozi wachache waliobeba hekima na busara za wazee na mtu mwenye kufanya uamuzi sahihi.
Alisema katika kipindi cha m afya na miundombinu ya barabara, amefanya mambo makubwa, hivyo aliwaomba wananchi kumpigia kura nyingi sana Dk. Mwinyi aendeleze safari ya maendeleo.
Mgombea uwakilishi wa jimbo la Kijini, Badria Atai Masoud, alisema majiaka mitano Dk. Mwinyi hakutumia muda wake kujibu maneno ya mitaani, bali aliweka misingi madhubuti ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.
Alisema katika elimu,imbo yote ya Kaskazini wanatiki kwa CCM sababu wananchi hawana chama mbadala.
Naye, Mgombea ubunge wa jimbo la Donge, Sadifa Juma Khamis, alisema Dk. Mwinyi amefanya mambo makubwa katika jimbo hilo ambalo wananchi wameahidi kumpigia kura nyingi Oktoba 29.
DK.SAADA MKUYA
Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Dk. Saada Mkuya Salum, aliwaomba wana-Kaskazini kuacha kusikiliza upotoshaji unaofanywa na badhi ya wanasiasa wanaotaka umaarufu wakati hawana sera.
Alisema Serikali ya Awamu ya Nane imefanya maendeleo makubwa kwa wananchi wa Zanzibar, hasa ujenzi wa barabara mjini na vijijini za kiwango cha lami.