• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. SAMIA AACHA GUMZO SONGEA AKIAHIDI NEEMA TELE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 22, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA AACHA GUMZO SONGEA AKIAHIDI NEEMA TELE

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.

0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH, 

Ruvuma

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuifungua mikoa ya kusini kuwa eneo la kimkakati kibiashara litakalofungua fursa za uwekezaji na ajira nchini.

Amesema katika kutimiza azma hiyo, tayari serikali imeanza kutekeleza miradi mikubwa kuimarisha miundombinu ya usafirishaji kwa njia ya anga, majini, barabara na reli.

Akizungumza na maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa VETA mjini Songea mkoani Ruvuma, Dk. Samia amesema wananchi wa mikoa hiyo watarajie neema kubwa.

“Tunataka kuufungua mkoa huu wa Ruvuma kuwa kitovu, pia ukanda mzima wa kusini (Ruvuma, Mtwara na Lindi) kuwa eneo la kibiashara. 

“Mkoa huu (Ruvuma) tumekamilisha upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege Songea. Nimetua juzi, nimeona njia ya kurukia haipungui kilometa tatu inayoruhusu ndege kubwa kutua hapa Songea.

“Njia hiyo ya ndege imeongeza idadi ya miruko ya ndege kutoka 276 hadi miruko 463 kwa mwaka. Na idadi ya abiria kutoka 3,971 hadi 20,667 kwa mwaka,” alisema.

Amesema awamu ya pili ya marekebisho ya kiwanja hicho ni kujenga jengo la abiria ambalo limefikia asilimia 70 pia, ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay umefikia asilimia 35 itakayoongeza kasi ya biashara katika ukanda wa Ziwa Nyasa.

Amesema serikali imekamilisha ujenzi wa Bandari ya Ndumbi ambayo imechochea biashara baina ya Tanzania na Malawi kupitia Nkatabay, hivyo kuongeza fursa za kiuchumi Ziwa Nyasa.

Dk. Samia amesema mwaka jana alizindua barabara ya Mbinga- Mbamba Bay inayounganisha Bandari ya Mtwara na Mbamba Bay.

“Tunafungua ukanda huu biashara zifanyike kwa anga, barabara au maji Ruvuma iwe kitovu kikubwa cha biashara. Tunakwenda kukamilisha barabara ya Kidatu – Ifakara – Malinyi hadi Lumecha inayounganisha Ruvuma na mkoa wa Morogoro,” alisisitiza.

Ameutaja mradi mwingine ni reli ya kisasa (SGR) ambayo itaunganisha Mtwara hadi Mbamba Bay.

Amesema reli hiyo yenye urefu wa kilometa 1,000 itaunganisha mikoa ya Mtwara na Ruvuma, kurahisisha usafirishaji madini yatakayochimbwa Mchuchuma na Liganga.

UUNGANISHAJI UMEME

Akizungumzia mkakati wa nishati safi, Dk. Samia alisema serikali imetekeleza mkakati huo zaidi ya ilivyotarajiwa katika ilani ya uchaguzi.

“Ilani ilituambia tukifika 2025 vijiji vyote viwe na umeme, serikali ipo katika vitongoji kuunganisha umeme. Takriban vitongoji nusu vya Tanzania vimeshaunganishwa umeme.

“Tunafanya hivyo kwa sababu tuliahidi kila wilaya kuwa na kongani za viwanda na tunataka tutakapoanza kuweka kongani, umeme uwe umeshafika na ndiyo maana tunakwenda kwa kasi,” alisema.

Alisema uwepo wa umeme utavutia wawekezaji wengi zaidi kuwekeza katika maeneo hayo.

Vilevile, serikali inakusudia kuweka viwanda vya kuongeza thamani zao la kahawa na parachichi.

“Kule Peramiho tumepata mwekezaji mkubwa wa kiwanda cha sukari na shamba kubwa la miwa. Hii pia ni fursa nyingine kutengeneza ajira kwa vijana wetu,” alisema.

Alisema Halmashauri ya Songea imeongeza uzalishaji mazao ya chakula kutoka tani 200,000 hadi 455,500 huku uzalishaji mazao ya kilimo kwa Madaba umepanda kutoka tani 141.7 hadi 160,000.

Kuhusu Mbinga, alisema uzalishaji kahawa umepanda, pia ruzuku ya miche na pembejeo za kilimo zinatolewa na serikali.

Alieleza uzalishaji kahawa umeongezeka kutoka tani zaidi ya 100 hadi 300 na kubainisha alitembelea shamba la mwekezaji lililoajiri watu 3,000 hali inayoonesha mkoa huo ni kinara kwa kilimo.

Aliwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kuchangia vyema usalama wa chakula nchini na mataifa jirani yanakouzwa mahindi.

Alisema Januari mwaka huu, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi 25 za Afrika zinazozalisha kahawa, ambapo

katika mkutano huo liliwekwa lengo la ndani ya miaka 10 ijayo (2025-2035) asilimia 50 ya kahawa bora inayozalishwa Afrika iwe inasindikwa kabla ya kuuzwa nje ya bara hilo.

Alibainisha lengo la serikali inayotokana na CCM ni kutekeleza azimio hilo kwa kufunga mitambo ya kukoboa kahawa kabla haijauzwa.

Vilevile, alisema serikali imetekeleza mradi wa ujenzi maghala 28 ya kuhifadhia mazao mkoani Ruvuma akiainisha Halmashauri ya Wilaya ya Songea ina maghala 11, Madaba (tisa), Namtumbo (saba) na ghala moja kwa Manispaa ya Songea.

Aidha, alisema katika Manispaa ya Songea, serikali itakamilisha ujenzi wa soko la kisasa Manzese A na B.

“Mkoa huu umebarikiwa kuwa na madini mengi kuanzia dhahabu, shaba, makaa ya mawe, madini ujenzi na vito hadi urani yanapatikana ndani ya mkoa huu,” alieleza.

Dk. Samia alisema endapo CCM ikipatiwa ridhaa, serikali yake itaanzisha na kuendeleza kongani za viwanda zinazohusiana na madini.

Alisema hatua hiyo itaongeza thamani ya madini kabla ya kuuzwa huku kipaumbele kikiwa katika uchimbaji na wachimbaji wadogo.

Mgombea huyo urais huyo wa CCM alisema mwaka huu alifika wilayani Namtumbo kuzindua mradi wa madini ya urani pamoja na kuchimba madini hayo azma ya serikali yachakatwe, yasafirishwe kisha uwepo mtambo wa kuzalisha umeme nchini upatikane kwa uhakika.

Pia, alisema duniani madini hayo yanakubalika kama nishati safi kwa taifa kuyatumia.

Dk. Samia alisema katika sekta za maendeleo ya jamii ambazo ni maji, elimu, afya na umeme serikali imetekeleza miradi hiyo kwa kasi kubwa.

Alieleza katika maji kuna miradi mingi inayoendelea kutekelezwa mkoani humo na itakapokamilika itapita kiwango cha upatikanaji maji kilichoelekezwa na ilani ya uchaguzi (2020-2025).

“Kwa hiyo bado miradi inaendelea, maji yatapatikana niwaombe tuwe wastahimilivu wakandarasi wafanye kazi zao vizuri na maji yapatikane,” alibainisha.

Kuhusu elimu, alisema ujenzi wa madarasa, shule umefanyika huku serikali ikiendelea kutoa elimu bila malipo.

Aligusia pia ujenzi wa Chuo Kikuu cha Uhasibu Arusha tawi la Songea na kusisitiza kitakamilika na kitachukua wanafunzi 10,000 kwa mkupuo.

Dk. Samia alisema ni fursa nzuri kwa wananchi wa mkoa huo, kuhamasika kusoma fani zitakazotolewa chuoni hapo.

Vilevile, alisema serikali itatekeleza ujenzi wa chuo cha wenye ulemavu eneo la Liganga, Jimbo la Peramiho kitakachotoa mafunzo yaliyokusudiwa.

Vilevile, alisema pamoja na serikali kujenga barabara ya lami kilometa 10 ndani ya mji wa Songea, bado kuna msongamano wa magari.

Hivyo, alisema ombi la mgombea ubunge wa jimbo la Songea Mjini, Dk. Damas Ndumbaro kujenga barabara ya mchepuko kupunguza msongamano, linakwenda kufanyiwa kazi.

“Natambua kuna maeneo ambayo mawasiliano ya simu siyo mazuri. Hilo nalo tunakwenda kulifanyia kazi kuhakikisha mawasiliano yawe mazuri kwa sababu ukanda wa biashara lazima uwe na urahisi wa mawasiliano,” aliongeza.

MWENYEKITI WA CCM MKOA

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho, alisema tangu Dk. Samia alipoanza mikutano yake ya kampeni kazi kubwa ya kuomba kura kwa wananchi imefanyika.

Alisema wagombea ubunge wameendelea kutoa ushuhuda kwa mafanikio yaliyofanyika katika miaka minne ya uongozi wa Dk. Samia.

WAGOMBEA UBUNGE

Kwa upande wake, mgombea ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama, alisema umeme umefika katika vijiji vyote vya jimbo hilo.

Alisema mwaka 2021 wananchi wa Ruvuma, walinunua mfuko wa mbolea kwa sh. 150,000 hivi sasa bei imeshuka hadi sh. 70,000.

Naye, mgombea ubunge Jimbo la Songea Mjini, Dk. Ndumbaro alisema jimbo hilo limenufaika kupitia ruzuku ya mbolea na soko la mahindi.

Alisema ujenzi wa hospitali ya rufani, ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, mradi mkubwa wa maji wenye thamani zaidi ya sh. bilioni 100, vimelifungua zaidi jimbo hilo kwa maendeleo.

Mgombea ubunge Jimbo la Madaba, Omari Msigwa, alisema kupitia uongozi wa Dk. Samia wananchi wameondokana na adha ya kusafiri umbali wa kilometa 100 kufuata huduma za afya kufuatia serikali kujenga hospitali ya wilaya.

Wagombea ubunge wateule wa viti maalumu, Mariam Nyoka na Jaqueline Msongosi walisema Dk. Samia amefanya kazi nzuri yenye kupigiwa mfano ndani na nje ya nchi. 

Previous Post

DK. NCHIMBI : TUTAJENGA BARABARA WILAYANI LUDEWA

Next Post

DK. MWINYI : YAJAYO YANAFURAHISHA KASKAZINI UNGUJA

Next Post
DK. MWINYI : YAJAYO YANAFURAHISHA KASKAZINI UNGUJA

DK. MWINYI : YAJAYO YANAFURAHISHA KASKAZINI UNGUJA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

VYAMA 18 Z’BAR VYASAINI FOMU KUELEKEA UCHAGUZI

VYAMA 18 Z’BAR VYASAINI FOMU KUELEKEA UCHAGUZI

2 months ago
MOROCCO ATAJA KILICHOIPONZA STARS

MOROCCO ATAJA KILICHOIPONZA STARS

5 days ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.