• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. NCHIMBI ATAJA SULUHU FOLENI DAR

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 2, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. NCHIMBI ATAJA SULUHU FOLENI DAR

MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi

0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SUPERIUS ERNEST 

MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema kama CCM itapewa ridhaa katika miaka mitano ijayo, itaondoa foleni katika Jiji la Dar es Salaam kwa kujenga makutano ya barabara (Fly Over), inayosababisha msongamano katikati ya jiji.

Pia, amepongeza utendaji kazi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha zaidi ya miaka minne, ambayo imeweka alama kila sekta, kikiwa ni kigezo cha kuwaomba wananchi kumchagua tena.

Dk. Nchimbi aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, katika mwendelezo wa kampeni za kunadi sera na kuomba kura kwa wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.

“Katika miaka mitano ijayo, kama tutapata ridhaa, ilani yetu ya uchaguzi, imeeleza namna tulivyojipanga kuchochea maendeleo ndani ya Jiji la Dar es Salaam, ikiwemo Kinodnoni.

“Tumekusudia kuanza ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Mwenge, Kinondoni, Magomeni na zingine, lengo ni kuondoa changamoto ya foleni,”alisema.

Alieleza mipango mingine ya utekelezaji ilani Kinondoni ni kujenga Barabara ya Mwai Kibaki, Bagamoyo, kujenga kilometa 97 zenye vumbi na barabara zingine kuweza kupitika muda wote.

Katika kuboresha huduma ya maji, Dk. Nchimbi, alisema wamekusudia kutanua mtandao wa maji kupitia mradi mkubwa wa Ruvu, usaidie Dar es Salaam wakiwemo wananchi wa Kinondoni.

Katika huduma za afya, alisema wataongeza zahanati nyingine Kinondoni zifikie 31 na vituo vya afya, kuongeza nyumba za watumishi wa afya.

Katika hatua nyingine, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema kipindi cha miaka mitano ijayo, kama Chama kitapewa ridhaa na wananchi, kitaweka mifumo rafiki ya ulipaji kodi kwa wafanyabiashara itakayowawezesha kulipa bila shuruti kuondoa changamoto zilizopo sasa.

Hivyo, aliwataka wanaCCM wote na wananchi kwa ujumla, ifikapo Oktoba 29, mwaka huu, kujitokeza kwa wingi kupiga kura, wapate ushindi wa asilimia 100 kwa sababu ya kazi kubwa iliyofanywa na Dk. Samia Suluhu Hassan kote nchini.

Akizungumza na wafanyabiashara wa Ilala, Dk. Nchimbi, alisema: “Katika miaka mitano ijayo kama mtatupa ridhaa, tumekusudia kuimarisha mfumo wa kodi rafiki ambao si shurutishi, kufanya mfanyabiashara kutambulika na serikali na sio adui wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Mfumo ambao TRA itashauriana na mfanyabiashara ikiwa ni msisitizo wa Rais Dk. Samia wa kuboresha maisha ya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.”

Aliwahakikishia wafanyabiashara wadogo, mama ntilie, waendesha bajaji, bodaboda, kuthamini mchango wao, hivyo katika miaka mitano ijayo watatengeneza mazingira mazuri zaidi ya kufanya shughuli zao.

Alisema katika kufikia hayo ndiyo maana serikali imekusudia kutenga sh. bilioni 200 za wafanyabiashara wadogo watekeleze majukumu yao.

Pia, alisema wataboresha mfumo wa mikopo ya asilimia 10 ambao miaka iliyopita ulikuwa haieleweki umejaa upendeleo, hivyo wataweka mfumo mzuri utakaosaidia kila mlengwa kuomba na kufikiwa.

Alieleza kuwa, mfumo huo ulitumika kwa upendeleo ukiwanufaisha baadhi ya maofisa, hivyo wataweka utaratibu mzuri wa kuwafikia walengwa.

Akieleza kuhusu uboreshaji wa miundombinu, Dk. Nchimbi, alisema katika miaka mitano ijayo, wamekusudia kuimarisha baadhi ya miundombinu zikiwemo barabara za mabasi yaendayo haraka ya Nyerere, Uhuru, Bibi Titi, ujenzi wa barabara ya juu eneo la Fire na kwingineko.

Kuhusu sekta ya Afya, Dk. Nchimbi alisema wataboresha zaidi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mnazi Mmoja, kujenga kituo cha afya Mchikichini na vinginevyo.

Pia, alisema Dk. Samia amefanya utafiti na kugundua kuwa, wananchi wanapata changamoto kubwa katika sekta afya, hivyo wamekusudia kila Mtanzania kupata bima ya Afya.

“Katika siku 100 za kwanza, kipaumbele ya bima Afya kitakuwa kwa wajawazito, watoto na watu wenye ulemavu,” alisema.

Dk. Nchimbi alisema katika elimu, watajenga sekondari eneo la Azania, kukarabati sekondari zote za zamani, kusimamia maendeleo ya viwanda na kutoa ajira milioni nane katika sekta rasmi na isiyo rasmi.

Alisema Dk. Samia ameonesha uwezo mkubwa katika uongozi wake,  akichochea  mabadiliko makubwa katika afya mambo makubwa yamefanyika upandikizaji moyo, upasuaji wa moyo kupitia tundi dogo na huduma nyingine za kibingwa.

Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM, UWT Taifa, Mary Chatanda, aliwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kuwapigia kura wagombea wa CCM kwa kazi kubwa waliyoifanya.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu, aliwataka wananchi kumpigia kura nyingi Dk. Samia na wagombea wengine wa Chama wa Mkoa huo wakiwemo wabunge na madiwani.

Naye, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu, alimshukuru Dk. Nchimbi kwa kufanya mkutano huo jimboni humo na kuwaomba wananchi kujitokeza kupiga kura kwani mambo mengi yamefanyika na ipo mipango mingi katika ilani itakayotekelezwa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM, UWT Taifa, Mary Chatanda aliwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kuwapigia kura wagombea wa CCM kwa kazi kubwa waliyoifanya.

Leo, Balozi Dk. Nchimbi anatarajiwa kuanza mikutano yake ya hadhara ya kampeni za Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu mkoani Mtwara.

Previous Post

DK. SAMIA ATANGAZA HATUA ZA MWISHO UTEKELEZAJI MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Next Post

DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA BARABARA ZA NDANI KWA KIWANGO CHA LAMI PANGAWE

Next Post
DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA BARABARA ZA NDANI KWA KIWANGO CHA LAMI PANGAWE

DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA BARABARA ZA NDANI KWA KIWANGO CHA LAMI PANGAWE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KOCHA TAIFA STARS UHAKIKA KWA NIGER

KOCHA TAIFA STARS UHAKIKA KWA NIGER

1 month ago
DK. SAMIA AELEZA VIPAUMBELE SIKU 100 ZA KWANZA AKIWA RAIS

DK. SAMIA AELEZA VIPAUMBELE SIKU 100 ZA KWANZA AKIWA RAIS

2 months ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.