Na MWANDISHI WETU
DODOMA
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza wake, Dk. Emmanuel Nchimbi, wameapishwa jijini Dodoma, kuanza rasmi safari ya uongozi katika kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Sita.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi mbalimbali, wageni waalikwa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Dk. Samia ameapishwa baada ya kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29 mwaka huu, ambapo alijitwalia asilimia 97.6 ya kura zote zilizopigwa, huku akiwashinda wagombea 16 wa vyama vya upinzani.












