Na MWANDISHI WETU,
ARUSHA
MKUU wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kuwa, hali ya ulinzi na usalama ni shwari na shughuli za kijamii na kiuchumi zimerejea katika hali ya kawaida.
Makalla ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
Aidha, katika kutekeleza maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa jana, CPA Makalla amewataka wamiliki wa vituo vya mafuta kufungua vituo vyao pamoja na maeneo mengine ya biashara, huku akiwataka viongozi wa serikali za mitaa na vijiji kuendelea kutimiza jukumu lao la kuhakikisha usalama unakuwepo wa kutosha katika maeneo yao, sambamba na kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria kwa mamlaka husika.
Katika hatua nyingine, CPA Makalla amewaagiza wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote mkoani humo chini ya usimamizi wa Katibu Tawala wa Mkoa, kuhakikisha huduma za usafi wa mazingira zinasimamiwa kikamilifu.




