• ePaper
Sunday, November 16, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Burudani

GAMONDI AMPA MAJUKUMU KELVIN JOHN

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 7, 2025
in Burudani, Habari, Michezo
0
GAMONDI AMPA MAJUKUMU KELVIN JOHN
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Miguel Gamondi amemrejesha nyota wa Aalborg BK ya Denmark, Kelvin John, katika kikosi cha timu hiyo kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi ya kirafiki kalenda ya FIFA dhidi ya Kuwait.

Pambano hilo, limepangwa kufanyika Novemba 14 jijini Cairo nchini Misri. 

Kelvin aliitwa mara ya mwisho na kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’, Machi 14, mwaka huu, wakati timu hiyo ikijiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco. 

Tangu hapo hakuitwa tena, licha ya kuanza vizuri msimu wa 2025/26 akiwa na kikosi cha Aalborg BK kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza huko Denmark ambapo ni msimu wake wa pili mfululizo. 

Chini ya Gamondi, mshambuliaji huyo ameitwa kwa mara nyingine tena akiwa mhimili mkubwa wa safu ya ushambuliaji ya Aalborg, akifunga mabao saba na kutoa  ‘asisti’ tatu katika mechi 15 alizocheza. 

Kelvin ameitwa huku nahodha wa Stars, Mbwana Samatta anayekipiga Le Havre ya Ligi Kuu Ufaransa na Simon Msuva wa Al Talaba wa Iraq wakitoswa kama ilivyokuwa katika kikosi cha mwisho kilichocheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Zambia. 

Katika kikosi kilichotangzwa mapema asubuhi ya jana, kocha Gamondi amewaita makipa, Yakoub Suleiman (Simba), Hussein Masalanga (Singida BS) na Zuberi Foba wa Azam FC. 

Wengine ni Bakari Mwamnyeto (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Mohamed Hussein (Yanga), Alphonce Mabula (Shamakhi, Azerbaijan), Feisal Salum (Azam FC), Morice Abraham (Simba), Abdul Suleiman (Azam FC) na Paul Peter wa JKT Tanzania. 

Wengine ni Mudathir Yahya (Yanga), Wilson Nangu (Simba), Novatus Dismas (Göztepe FC, Uturuki), Pascal Msindo (Azam FC) na Ibrahim Abdulla wa Yanga.

Haji Mnoga (Salford City, Uingereza), Dickson Job (Yanga), Habibu Idd (Singida BS), Tarryn Allarakhia (Rochdale AFC, England), Charles M’Mombwa (Floriana FC, Malta) na Seleman Mwalimu  kutoka Simba.

Gamondi ambaye ni Kocha Mkuu wa timu ya Singida Big Star, Novemba 4, mwaka huu, alitangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kukaimu nafasi iliyoachwa na Hemed Suleiman ‘Morocco’ aliyesitishiwa mkataba.

Kocha huyo atasaidiwa na Ahmad Ally ambaye anakinoa kikosi cha JKT Tanzania.

Previous Post

CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI CHAMPONGEZA JOHARI

Next Post

YANGA, SIMBA ZAANZA KUCHONGA 

Next Post
YANGA, SIMBA ZAANZA KUCHONGA 

YANGA, SIMBA ZAANZA KUCHONGA 

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KATIBUBMkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), BalozibDk. Asha-Rose Migiro

CCM IMEJIPANGA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU – BALOZI DK. MIGIRO

3 months ago
DK. SAMIA AMEONESHA UMAHIRI KATIKA UONGOZI – DK. NCHIMBI

DK. SAMIA AMEONESHA UMAHIRI KATIKA UONGOZI – DK. NCHIMBI

2 months ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KETE YA KWANZA KWA GAMONDI STARS LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAGIZO MATATU KWA DK. NCHEMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI MARIDHIANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.