• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. SAMIA AMEONESHA UMAHIRI KATIKA UONGOZI – DK. NCHIMBI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 26, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA AMEONESHA UMAHIRI KATIKA UONGOZI – DK. NCHIMBI

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi

0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA,

Iringa

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amebainisha kwa vitendo mwanamke wa Kitanzania anapopewa fursa ya kuongoza anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kuleta matokeo makubwa ya maendeleo.

Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo Isimani, alipohutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa kampeni za Chama kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Amesema hofu ilikuwepo kipindi Rais Dk. Samia anaingia madarakani miaka minne na nusu iliyopita, hivi sasa imefutwa na matendo yake makubwa, ambayo yamejidhihirisha katika kila sekta ya maendeleo ya taifa.

“Rais wetu ametuongoza kwa ufanisi. Ametimiza kiapo chake cha kuimarisha mshikamano, kuendeleza umoja wa taifa letu, kulinda mipaka na uhuru wa taifa letu na ameweka historia ya pekee ya mafanikio katika nyanja zote,” amesema.

Mgombea Mwenza wa Urais amesema mfano wa Rais Dk. Samia umekuwa kielelezo hadi kwa mataifa mengine na hivi sasa yanauliza kiongozi wa aina yake watampata wapi.

“Amedhihirisha kwa vitendo kwamba, wanawake wa Kitanzania wakipewa fursa wanaweza. Leo Samia amekuwa kiongozi wa mfano ndiyo maana nchi nyingine zimekuwa zikihoji zitampata wapi kiongozi kama Samia, tunawaambia tafuteni wenu,”amesema.

Balozi Dk. Nchimbi ameeleza mikakati ya CCM kwa miaka mitano ijayo kupitia ilani yake ya mwaka 2025-2030 ikiwemo kujenga vituo vipya vya afya saba, zahanati 15 na kupandisha hadhi ya hospitali ya wilaya.

Kuhusu sekta ya elimu, amesema itapewa kipaumbele kwa kuongeza shule 12 za msingi, sekondari nane na madarasa 395 katika shule zilizopo.

Amesema mradi mkubwa wa maji utaanzishwa Isimani na utawanufaisha wananchi katika zaidi ya maeneo manane, sanjari na uchimbaji wa visima virefu vitano na kukamilisha miradi mingine minne.

Kwa upande wa kilimo, Dk. Nchimbi amesema wamekusudia kuongeza ruzuku ya mbolea, kuboresha skimu za umwagiliaji, kujenga mifereji mipya na ghala la kuhifadhi mazao ya parachichi.

Akizungumzia sekta ya ufugaji, Balozi Dk. Nchimbi alisema wataimarisha ruzuku ya dawa na chanjo, kujenga majosho, malambo na mabwawa ya samaki vijana wapate fursa za ajira na kipato.

Vilevile, alisema mazingira ya biashara yataboreshwa kwa wajasiriamali na barabara zaidi ya tano zitajengwa kwa kiwango cha lami na zaidi ya 10 kwa kiwango cha changarawe.

Balozi Dk. Nchimbi alimwombea kura Rais Dk. Samia, wabunge na madiwani, wahakikishe Oktoba 29, mwaka huu, wanakipigia kura Chama.

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Isimani, William Lukuvi, alimshukuru Dk. Samia kwa kumuona Balozi Dk. Nchimbi.

Lukuvi alisema rekodi ya uongozi wa Dk. Nchimbi serikalini na ndani ya CCM inajulikana wazi, kuanzia Mwenyekiti wa Umoja wa  Vijana wa CCM (UVCCM), mkuu wa wilaya, naibu waziri hadi waziri na mjumbe wa vikao vikuu vya chama.

Lukuvi alisema rekodi hiyo inawapa wananchi imani kuwa ndiye mtu sahihi wa kumsaidia Rais Dk. Samia katika safari ya kuendeleza taifa.

 “Wananchi wa Isimani wanajua rekodi yako. Uadilifu wako, uzalendo wako na misimamo yako imara ndiyo sababu tunasema kwa dhati hatuna shaka na wewe. Hadi Oktoba 29 nitakuwa nikiwaambia wananchi wewe ni nani,”alisema.

Lukuvi aliwaomba wananchi wa Isimani Oktoba 29, mwaka huu, wajitokeze kwa wingi na kumpigia kura Dk. Samia katika urais, wabunge na madiwani wanaotokana na CCM.Awali, akiwahutubia mamia ya wananchi katika 

Uwanja wa Mpira wa Isere, Jimbo la Kilolo, katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Chama za kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mgombea mwenza huyo, Dk. Nchimbi, aliainisha baadhi ya vipaumbele vitakavyotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, huku sekta ya kilimo, afya, elimu, miundombinu na nishati vikitajwa kama nguzo kuu za maendeleo ya wananchi wa eneo hilo.

Alisema vipaumbele hivyo vitatekelezwa kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya mwaka 2025-2030, iwapo CCM itapewa ridhaa ya kuongoza nchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema dhamira ya Dk. Samia ni kuendeleza jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi kwa kasi zaidi katika miaka mitano ijayo.

Alibainisha kuwa,katika kipindi cha miaka mitano ijayo Chama kimekusudia kuboresha Hospitali ya Wilaya ya Kilolo kwa kuongeza majengo, vitendea kazi na rasilimali watu kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Pia, Balozi Nchimbi alisema wamedhamiria kujenga vituo vipya vya afya vitano na zahanati 10 kufanikisha upatikanaji wa huduma bora karibu na wananchi.

Previous Post

DK. SAMIA AAHIDI WAKULIMA DAWA YA KUPULIZIA MIKOROSHO BILA MALIPO

Next Post

WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

Next Post
WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA WABUNGE

RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA WABUNGE

3 weeks ago
SIKU 100 ZA RAIS DK. MWINYI:NI MAENDELEO, UWAJIBIKAJI

SIKU 100 ZA RAIS DK. MWINYI:NI MAENDELEO, UWAJIBIKAJI

3 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?