• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WADAIWA VIWANJA 6,560 DODOMA WAPEWA SIKU 21

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 30, 2025
in Habari, Kitaifa
0
WADAIWA VIWANJA 6,560 DODOMA WAPEWA SIKU 21
0
SHARES
20
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na FRED ALFRED, 
Dodoma

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma, imetoa siku 21 kwa wadaiwa wa viwanja 6,560 vyenye thamani ya sh. bilioni 55.4 vilivyopo maeneo ya Mtumba Zone II, Mtumba Zone III na Kikombo kujitokeza kufanya malipo.

Imesema watakaoshindwa kufanya hivyo, hatua zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa kisha kurejeshwa sokoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dennis Gondwe, alisema hatua hiyo, imekuja baada ya halmashauri kukamilisha zoezi la uhakiki wa malipo ya viwanja na kubaini kuwepo kwa wadaiwa wengi wakiwemo watu binafsi, taasisi na kampuni.

Alisema kwa Mtumba Zone II pekee kuna viwanja 1,915 vyenye thamani ya sh. bilioni 28.8 ambavyo bado havijalipiwa kikamilifu, hali inayokosesha mapato Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Aidha, Mtumba Zone III ina viwanja 2,594 vyenye thamani ya sh. bilioni 20.6, huku eneo la Kikombo likiwa na viwanja 2,051 vyenye thamani ya sh. bilioni 5.9 na kufanya jumla ya thamani ya viwanja vyote kufikia sh. bilioni 55.4.

Gondwe, alisema ucheleweshaji wa malipo hayo umeathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ukiwemo ujenzi na ukarabati wa barabara, upatikanaji wa maji safi na salama na usambazaji wa umeme.

“Mapato yatokanayo na mauzo ya viwanja ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa bajeti ya halmashauri, hususan kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi wa Jiji la Dodoma,” alisema.

Alisisitiza kuwa :”Wadaiwa wote wanapaswa kujitokeza ndani ya siku 21 kuanzia tarehe ya tangazo hilo ili kukamilisha malipo yao, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kurejeshwa kwa viwanja hivyo sokoni.

Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi waliokamilisha malipo lakini majina yao hayakuonekana katika orodha ya wadaiwa kufika katika ofisi za Jiji wakiwa na nyaraka halisi kwa ajili ya uhakiki.

Gondwe alibainisha kuwa lengo la zoezi hilo siyo kuwaadhibu wananchi, isipokuwa kuhakikisha uwazi, haki na upatikanaji wa rasilimali zitakazochochea maendeleo endelevu ya Jiji la Dodoma linalokuwa kwa kasi.

Previous Post

PM MWIGULU KUVALIA NJUGA MIGOGORO YA ARDHI

Next Post

MSIGWA AELEZA MANUFAA UBORESHAJI RELI YA TAZARA

Next Post
MSIGWA AELEZA MANUFAA UBORESHAJI RELI YA TAZARA

MSIGWA AELEZA MANUFAA UBORESHAJI RELI YA TAZARA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, USTAHIMILIVU

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, USTAHIMILIVU

4 months ago
SH. TRILIONI 3.5 ZIMETOLEWA KUWEZESHA VIJANA – MAJALIWA

SH. TRILIONI 3.5 ZIMETOLEWA KUWEZESHA VIJANA – MAJALIWA

5 months ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?