• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

GAMONDI MATUMAINI KIBAO AFCON 2027

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 2, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
GAMONDI MATUMAINI KIBAO AFCON 2027
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA, Kahama

KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Miguel Gamondi amewaomba Watanzania na wadau wa soka kutokuwa na wasiwasi na timu yao, kwani amejipanga kuboresha zaidi kikosi hicho kabla ya michuano ya Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza  mwezi Julai, mwakani ikishirikiana na nchi za Kenya na Uganda.

Akizungumza Kahama mkoani Shinyanga baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Gamondi alisema Watanzania wote wana matumaini kibao na kikosi chake, hivyo aliwatoa hofu kuwa wataenda kufanya vizuri.

“Niwaambie tu wadau wa soka nchini, hawatakiwa kuwa na hofu kwani nataka kufanya kazi ya kujenga kikosi imara ili kifanye vizuri katika michuano ya AFCON 2027,” alisema.

Hata hivyo,  Gamondi alisema anahitaji  kufanya kazi ya maandalizi ya mapema kuelekea katika mashindano hayo, lengo ni kuona wapi kuna upungufu.

Kocha huyo alisema kwamba anahitaji mechi nyingi za kirafiki ili kikosi chake kipate uzefu zaidi kabla ya kuanza mashindano hayo.

Aliongeza kuwa anajivunia kuwa na wachezaji wengi vijana ambao watajenga kikosi kizuri.

Aidha, baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF, wamewashauri wachezaji watakaoitwa katika kikosi waweka mbele uzalendo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajumbe hao, ambao waliudhuria mkutano mkuu wa 20 wa TFF uliofanyika Kahama, Shinyanga walisema wana imani timu hiyo itafanya vizuri.

Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga,  Alex Ngai alisema anapenda kuwashauri wachezaji wa Taifa Stars hasa kuelekea katika michuano ya AFCON wahakikishe wanaongeza juhudi na kujituma zaidi.

“Kuwa wenyeji wa AFCON ni heshima kubwa kwetu, hivyo wachezaji wa timu yetu wanatakiwa kuwa watulivu, kujituma na kuonyesha nia ya dhati ya kupambana ili tuweze kutwaa taji hilo,” alisema Ngai.

Mjumbe wa kamati ya utendaji TFF, Lameck Nyambaya alisema kwamba  wana imani kubwa na timu yao ya Taifa hivyo wachezaji wanatakiwa kupambana kwa jasho na damu ili kufanya vizuri na kupata matokeo chanya.

“Mimi sina wasiwasi na timu yetu ya Taifa, kwani tunahitaji kuona tunapata matokeo mazuri katika mashindano hayo, hivyo wachezaji wetu wanatakiwa kushirikiana ili kufanya vizuri,” alisema Nyambaya.

Naye mjumbe wa Mkutano mkuu, Murtaza Mangungu alisema imani yake ipo kwa wachezaji wa Stars hivyo wanatakiwa kuongeza nguvu zaidi ili kuwapa furaha Watanzania.

“Tunaingia katika mshindano hayo tukiwa tuna uhakika wa kufanya vizuri katika mashindano hayo, lakini wachezaji wetu wanatakiwa kujua umuhimu wa  kupambana  na kurekebisha upungufu wote tufanye vizuri,” alisema Mangungu.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi  mwezi Julai, mwakani huku wenyeji wakiwa ni Tanzania, Kenya na Uganda.

Previous Post

IMEISHA HIYO

Next Post

TANZANIA NA GHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA

Next Post
TANZANIA NA GHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA

TANZANIA NA GHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

PAPA LEO AAHIDI KUIOMBEA TANZANIA AMANI, UTULIVU

PAPA LEO AAHIDI KUIOMBEA TANZANIA AMANI, UTULIVU

2 months ago
MSIGWA : DK. SAMIA AMETHIBITISHA UWEZO WAKE WA UONGOZI

MSIGWA : DK. SAMIA AMETHIBITISHA UWEZO WAKE WA UONGOZI

6 months ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?