• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 17, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amewataka viongozi wa wilaya na halmashauri nchini, kushughulikia changamoto za wananchi kwa wakati bila kusubiri ziara za viongozi wa kitaifa.

Dk. Mwigulu aliyasema hayo, alipohitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Katavi iliyoanza Machi 13, mwaka huu.

Akizungumza na viongozi katika kikao cha majumuisho kilichofanyika Ukumbi wa Katavi Social Hall, Manispaa ya Mpanda, Waziri Mkuu alisema mfumo wa ugatuaji madaraka, unalenga kuwapa viongozi wa maeneo uwezo wa kutatua changamoto za wananchi katika ngazi zao.

“Sio lengo la muundo wetu wa serikali ugatuaji wa madaraka kwamba mambo yatatuliwe panapokuwa na ziara za viongozi wa kitaifa.

“Hoja zote tulizosikiliza zimeandikwa, nendeni mkazifuatilie moja baada ya nyingine na mzifikishe mwisho,” alisema.

Sekta ya Elimu

Katika sekta ya elimu, Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwa viongozi wa Halmashauri ya Tanganyika, kutatua changamoto za wanafunzi, ikiwemo miundombinu ya shule na michango isiyo rasmi inayowakwamisha wanafunzi kupata elimu.

Dk. Mwigulu aliagiza kufanyika tathmini ya michango inayotozwa katika shule, kuhakikisha wanafunzi hawazuiwi masomo kwa sababu ya michango.

“Ni jambo lisilokubalika mwanafunzi kukosa masomo kwa sababu ya michango, ilhali serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 35 kila mwezi kugharimia elimu bila ada,” alisema Waziri Mkuu.

Aidha, aliwataka viongozi kufanya tathmini ya mahitaji ya elimu katika maeneo yao kwa kuzingatia kuanzia mwaka 2028, serikali itaanza kutekeleza mfumo wa elimu ya lazima hadi kidato cha nne.

“Kama elimu ya msingi ya lazima itakuwa hadi kidato cha nne, maana yake kila mtoto lazima afike kidato cha nne. Kwa lugha nyingine, kila kijiji kinapaswa kuwa na sekondari,” alisema.

Sekta ya Afya

Katika sekta ya afya, Waziri Mkuu aliagiza mkandarasi anayejenga jengo la huduma (Wing B) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, kuharakisha ujenzi wa mradi huo.

“Fedha za mradi zipo na vifaa vimeshafika, hivyo mkandarasi aharakishe ujenzi ili mradi ukamilike kwa wakati,” alisema.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha dawa zinazohitajika zinapatikana katika vituo vya afya na kuonya kuagiza dawa zisizohitajika.

“Uagizaji wa dawa lazima uzingatie mahitaji. Tusiagize dawa ambazo hazitumiki zikaharibika, huku fedha za serikali zikiwa zimepotea,” alisema.

Sekta ya Maji

Kwa upande wa maji, Waziri Mkuu aliagiza wizara na taasisi zinazohusika, kuhakikisha mradi wa maji uliokaguliwa unakamilika kwa wakati na wananchi wa maeneo yanayozunguka mradi huo wanapata huduma ya maji.

Miundombinu ya Barabara

Katika sekta ya ujenzi na miundombinu, Waziri Mkuu aliagiza barabara zilizoharibika kutokana na mvua, zishughulikiwe kwa dharura na kusisitiza kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Kagwira-Karema.

Pia, alielekeza barabara ya Kibaoni-Majimoto-Mlele kuingizwa katika mpango wa vipaumbele vya serikali ili kuanza ujenzi baada ya utaratibu wa usanifu utakapokamilika.

Nishati na Umeme

Katika sekta ya nishati, Dk. Mwigulu alisema serikali imepeleka umeme katika vijiji 172 na vitongoji 534 kati ya 912 mkoani Katavi na kazi ya kupeleka umeme katika maeneo yaliyosalia inaendelea.

Migogoro ya Ardhi

Waziri Mkuu pia aliagiza viongozi wa mkoa kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya watu wanaosababisha migogoro ya ardhi kwa kuuza viwanja mara nyingi kwa watu tofauti.

“Kuna watu wameuza kiwanja kimoja kwa watu watano. Hatuwezi kuangalia migogoro tu, lazima tujue chanzo chake na wahusika wachukuliwe hatua,” alisema.

Previous Post

ALAMA TATU KUMUENZI JPM

Next Post

SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

Next Post
SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAZIRI MKUU: WIZARA YA AFYA FUATILIENI UPATIKANAJI WA DAWA MAHSUSI

WAZIRI MKUU: WIZARA YA AFYA FUATILIENI UPATIKANAJI WA DAWA MAHSUSI

3 months ago
OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

3 months ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?