• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 16, 2025
in Burudani, Kimataifa, Michezo
0
OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

Azzedine Ounahi

0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RABAT, Morocco

KIUNGO wa kati wa Morocco, Azzedine Ounahi ametajwa kuwa miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kutazamwa zaidi katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.

Michuano hiyo imepangwa kuanza kufanyika Desemba 21, mwaka huu nchini Morocco.

Morocco imepangwa kundi A na timu za Mali, Zambia na Comoros katika michuano hiyo yenye kuvuta hisia kubwa kwa mashabiki wa soka Barani Afrika na hapa nchini.

Morocco maarufu  ‘Atlas Lions’ katika michuano hiyo hii, inasaka taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1976.

Tayari  Ounahi ameibuka kama mtu muhimu katika kampeni za wenyeji kuhakikisha safari hii taji hilo linabakia nchini Morocco.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, jukumu lake limekuwa na uzito zaidi huku kukiwa na sintofahamu juu ya utimamu wa nahodha Achraf Hakimi.

Kama Hakimi atakosa kushiriki michuano hiyo, Ounahi atakuwa na jukumu la kuongoza maeneo ya kati kuhakikisha Morocco inafanya vizuri katika mashindano hayo.

Hatua hiyo, inakuja baada ya Ounahi kupita kipindi kigumu huko Marseille, lakini hivi sasa Ounahi amejiimarisha tena kama mwanzilishi wa kawaida tangu ajiunge na timu ya Girona.

Baadhi ya mashabiki wa soka nchini Morocco wanamwona  mchezaji huyo kama nyota anayeweza kuunda bahati ya timu katika ardhi ya nyumbani kutwaa taji hilo.


Wachezaji wengine wanaotarajiwa kung’ara katika michuano hiyo ni Mohamed Salah wa Misri.

Victor Osimhen wa Nigeria, Riyad Mahrez wa Algeria na Sadio Mané wa nchi ya Senegal.

Pia, imeelezwa kuwa katika fainali hizo wapo chipukizi wa kuangaliwa ambao ni Ibrahim Mbaye wa Senegal na Rogers Mato wa Uganda.

Previous Post

KIPA NIGERIA ASHUSHA PRESHA

Next Post

KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

Next Post
KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

2 weeks ago
AMANI NGUZO KUU YA USTAWI – RAIS DK. SAMIA

AMANI NGUZO KUU YA USTAWI – RAIS DK. SAMIA

7 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?