• ePaper
Friday, August 28, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NDEJEMBI KUMRITHI BALOZI DK. NCHIMBI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 26, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
NDEJEMBI KUMRITHI BALOZI DK. NCHIMBI
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

HALMASHAURI Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imempendekeza Deogratius Ndejembi (43), kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uamuzi huo ulitangazwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asha Rose-Migiro, katika ofisi ndogo za Chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Dk. Migiro alisema uamuzi wa Ndejembi kuwa Makamu wa Rais, utafanyika baada ya utaratibu wa kikatiba kukamilika.

“Uamuzi muhimu uliofanywa na Halmashaurui Kuu, ni kupokea na kupitisha jina katika hatua ya awali la mtu ambaye atapendekezwa kwa mujibu wa taratibu za Katiba kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na huyo ni Deogratius Ndejembi,”alisema Dk. Migiro.

Dk. Migiro alisema baada ya kupendekezwa jina hilo, litapelewa bungeni jijini Dodoma na taratibu za kumuapisha zitaanza.

Ndejembi ambaye ni Waziri wa Nishati, anachukua nafasi ya Dk. Emmanuel Nchimbi, ambaye alitangaza kujiuzulu Agosti 25, mwaka huu.

Nchimbi afutwa uanachama

Aidha, Dk. Migiro alisema CCM imemfuta uanachama Dk. Nchimbi kwa kukiuka katiba na kanuni za CCM.

Alifafanua Dk. Nchimbi, alikuwa akikabiliwa na makosa ya nidhamu na maadili.

“Leo tarehe 26 vilifanyika vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, vilikuwa na ajenda za jumla ambazo zilijadiliwa, kati ya ajenda zilizojadiliwa kulikuwa na suala la nidhamu na maadili, ambalo lilikuwa linamkabili mwanachama mwandamizi wa Chama chetu, Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu Balozi Emmanuel Nchimbi.

“Vikao vyote vilijadili kwa makini masuala yaliyohusu nidhamu na maadili, na baada ya kuzingatia taarifa zote zilizokuwepo ilithibitika kwamba Katiba ya CCM pamoja na kanuni zake zilikiukwa, kufuatia hayo Halmashauri Kuu ilipitisha uamuzi kutokana na mwenendo uliokiukwa ndugu Nchimbi afukuzwe uanachama,”alisema Dk. Migiro.

Previous Post

TUME YA MADINI YATOA SIKU 30 KWA WALIOKIUKA MIKATABA YA MSAADA WA KIUFUNDI

Next Post

MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

Next Post
MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAKONDA ASISITIZA KUTOVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE AFCON

MAKONDA ASISITIZA KUTOVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE AFCON

7 months ago
ABDULRAZAQ HAMIS BONDIA ANAYECHUKIZWA NA WAAMUZI WANAO PENDELEA WASIO NA UWEZO

ABDULRAZAQ HAMIS BONDIA ANAYECHUKIZWA NA WAAMUZI WANAO PENDELEA WASIO NA UWEZO

9 months ago

Popular News

  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI KUMRITHI BALOZI DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME YA MADINI YATOA SIKU 30 KWA WALIOKIUKA MIKATABA YA MSAADA WA KIUFUNDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ARIDHIA DK. NCHIMBI KUJIUZURU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?