• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 8, 2026
in Habari, Kitaifa
0
BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya ndege ya British Airways imetangaza kurejesha safari za moja kwa moja kati ya Uingereza na Tanzania kuanzia Mei 2027, hatua inayolenga kuongeza usafiri wa watalii na wasafiri wa kibiashara kati ya mataifa hayo.

Tangazo hilo limetolewa Oktoba 7, 2026, na Mkuu wa Masoko wa British Airways kwa Bara la Afrika, Asia na Pasifiki, Moran Birger, katika Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza, katika ukumbi wa Mikutano wa Peninsula Hotel London Uingereza. Jukwaa hilo limefunguliwa na Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba

Birger amesema uamuzi huo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa idadi ya wasafiri na watalii wanaoitembelea Tanzania, sambamba na maendeleo ya kiuchumi na uwekezaji ambayo yameifanya Tanzania kuvutia watu wengi kufanya uwekezaji.

Kwa Upande wake Dk. Mwigulu amepongeza uamuzi huo akiutaja kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kuendelea kuifungua Tanzania na kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Kadhalika, Dk. Dkt Mwigulu amesema Tanzania ni kitovu  cha uwekezaji na ina masoko zaidi. “Kwa mwekezaji anayataka kuja kuwekeza  Tanzania,  asiangalie soko la ndani tu, bali aione Tanzania kama jukwaa la kuwafikia wadau wengi wa kikanda kwani inanknda nyingi inazojihusisha nazo,” amesema.

Amewaambia washiriki wa Kongamano hilo wapatao 300 kwamba amani, utulivu na uongozi imara usiotetereka ndiyo mtaji mkubwa wa kuifanya Tanzania kuwa jukwaa la uwekezaji.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu amesema uwepo wa umeme wa uhakika,  miundombinu ya barabara, reli ya kisasa ya SGR, bandari na viwanja vya ndege ni vichocheo vikubwa vya kuharakisha maendeleo  nchini.

Amesema mageuzi ya kiuchumi ambayo Tanzania imeyapanga kulingana na DIRA 2050, yanataka uwepo wa umeme wa uhakika na wa bei nafuu.

Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Kitila Mkumbo, amesema, Serikali ya Awamu ya Sita imeandaa Dira ambayo inafungua njia na muelekeo wa nchi.

“Nchi imeandaa sera, mipango na malengo thabiti kufanikisha malengo yake na kuwezesha ukuaji wa uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na ukuaji wa uchumi wa nchi kwa ujumla”

Previous Post

KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

Next Post

WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Next Post
WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AACHA GUMZO SONGEA AKIAHIDI NEEMA TELE

DK. SAMIA AACHA GUMZO SONGEA AKIAHIDI NEEMA TELE

1 year ago
GAMONDI AMPA MAJUKUMU KELVIN JOHN

GAMONDI AMPA MAJUKUMU KELVIN JOHN

11 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?