• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 8, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WABUNGE kutoka Kundi la Kijiografia-Kisiasa la Bara la Afrika kupitia Umoja wa Mabunge ya Duniani (IPU) wameunga mkono ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ya kuimarisha afya ya uzazi, mama, mtoto na vijana barani Afrika.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Arusha katika mkutano wa pembezoni wa Mkutano wa 153 wa IPU, ambapo viongozi hao pamoja na wadau wa maendeleo ya Sekya ya Afya Duniani wamejadili umuhimu wa kuimarisha sera, mifumo ya utoaji huduma, uwekezaji na uwajibikaji katika sekta ya afya.

Kiongozi wa Kundi la Kijiografia-Kisiasa la Wabunge wa Bara la Afrika kupitia IPU na Spika wa Jamhuri ya Chad, Ali Kolotou Tchaïmi, amesema wakati umefika kwa nchi za Afrika kuunganisha nguvu, kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuwa na agenda ya pamoja ya kuboresha afya ya mama na mtoto.

Kwa upande wake Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Angela Didiza, amesema Afrika inaweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Tanzania katika kuendeleza afya ya wanawake, watoto wachanga, watoto na vijana, akisisitiza kuwa uongozi wa kisiasa una nafasi muhimu katika kuweka mazingira ya utekelezaji wa hatua za kibunge.

Spika wa Bunge la Botswana, Dithapelo Keorapetse, amesisitiza umuhimu wa kuunganisha uwekezaji katika sekta ya afya na ufuatiliaji wa matumizi na matokeo yake.

“Uwekezaji pekee hautoshi, bado tunakabiliwa na changamoto katika matokeo ya afya, hali hii inaonesha umuhimu wa kuangalia ufanisi wa matumizi ya rasilimali” amefafanua Keorapetse.

Akizungumza, Rais wa Umoja wa Mabunge ya Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema juhudi za Rais Samia katika kuimarisha afya ya uzazi zinapaswa kuungwa mkono, huku akisisitiza kuwa bila utashi wa kisiasa na uwajibikaji wa viongozi, wataalamu wa afya na na mifumo ya afya haitoshi kuimarisha Huduma za Afya ya uzazi, mama na mtoto.

“IPU inajidhatiti kuwa mshirika wa vitendo kwa mabunge katika kuhakikisha ahadi zinatafsiriwa kuwa hatua na matokeo chanya ya kuimarisha Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto” amesema Dk. Tulia.

Naye Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, amesema afya ya mama na mtoto ni kipaumbele cha Serikali ya Tanzania na kwamba Bunge kwa niaba ya wananchi lina wajibu wa kusimamia rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya huduma hizo.

Awali, Mshauri wa Rais kuhusu Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Mhe. Ummy Mwalimu, amesema vifo vitokanavyo na uzazi barani Afrika vimepungua kwa asilimia 42 kati ya mwaka 2000 na 2023, lakini Afrika bado inachangia asilimia 70 ya vifo vya kina mama duniani.

Amesema kupitia Mpango Kazi wa Rais Samia wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto Barani Afrika 2026–2030, ajenda ya Rais Samia inalenga kufikia Sifuri Tatu: sifuri ya kujifungulia nyumbani, sifuri ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto, na sifuri ya watoto wasiochanjwa.

Previous Post

BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AVUTIA MAELFU KILA KONA

DK. SAMIA AVUTIA MAELFU KILA KONA

12 months ago
DCEA YAKAMATA SHEHENA YA MIRUNGI KUTOKA KENYA, YAKAMATA BOTI BAGAMOYO

DCEA YAKAMATA SHEHENA YA MIRUNGI KUTOKA KENYA, YAKAMATA BOTI BAGAMOYO

6 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?