• ePaper
Saturday, October 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MWIGULU ANUNUA TIKETI ZA SINGIDA BLACK STARS, TUSKER

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 24, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
MWIGULU ANUNUA TIKETI ZA SINGIDA BLACK STARS, TUSKER
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAZIRI Mkuu na mlezi wa timu ya Singida Black Stars, Dk. Mwigulu Nchemba, amenunua tiketi zote za mchezo wa marudiano ya raundi ya pili ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Tusker FC ya Kenya.

Pambano hilo, limepangwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mchezo huo wa marudiano utachezwa kuanzia saa 1:00 usiku, huku ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 katika mchezo wake wa kwanza uliopigwa nchini Kenya.

Mchezo huo ni muhimu kwa Singida BS ambayo inahitaji ushindi au sare ya aina yeyote ili kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Singinda BS, Hussein Massanza alisema mlezi wa timu hiyo, Dk. Mwigulu Nchemba amenunua tiketi zote hizo ili kuwezesha Watanzania kuingia bila kulipia.

“Habari njema ni kwamba Waziri Mkuu na mlezi wa timu yetu Dk. Mwigulu Nchemba amenunua tiketi zote za mchezo huo lengo ni kuwapa fursa Watanzania kuingia bure na kwenda kuishangilia timu yao ipate ushindi mnono,” alisema.

Massanza aliwaomba mashabiki na wapenzi wa soka kwa ujumla kujaaa kwa wingi ili kuwapa sapoti ya kutosha wachezaji wa timu hiyo wafanye vizuri.

Katika mechi sita za hatua ya makundi msimu wa 2025/26, Singida ilipata ushindi mmoja, sare mbili na kupoteza mechi tatu, ikifunga mabao matatu na kuruhusu sita. Ushindi wake pekee ulikuwa wa bao 1-0 dhidi ya AS Otoho ya Congo.


Msimu huu, timu hiyo imeanza kwa kasi tofauti katika hatua za awali, ikifunga mabao 10 dhidi ya El-Ghazal ya Sudan Kusini na kisha kupata ushindi muhimu wa ugenini dhidi ya Tusker, mechi lichezwa Oktoba 18,mwaka huu.

Previous Post

TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

Next Post

MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI

Next Post
MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI

MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WATOTO HAWASTAHILI KUCHOMWA VIGANJA KWA KUDOKOA NYAMA

WATOTO HAWASTAHILI KUCHOMWA VIGANJA KWA KUDOKOA NYAMA

9 months ago
TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

11 months ago

Popular News

  • MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI

    MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ANUNUA TIKETI ZA SINGIDA BLACK STARS, TUSKER

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KUWA KITOVU SOKO LA KABONI AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?