• ePaper
Friday, October 23, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA KUWA KITOVU SOKO LA KABONI AFRIKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 23, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA KUWA KITOVU SOKO LA KABONI AFRIKA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amesema Tanzania imejipanga kuwa kitovu cha soko la kaboni barani Afrika kwa kuendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi, uwazi na uwekezaji kuhakikisha biashara hiyo inachangia ukuaji uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Masauni amesema hayo, Oktoba 22, 2026 wakati akifungua Jukwaa la Soko la Kaboni na Uwekezaji Tanzania 2026, jijini Dar es Salaam, likiwa na kaulimbi: “Siku Moja. Soko Moja. Maono ya Pamoja.”

Amesema serikali inalenga kuhakikisha biashara ya kaboni inakuwa nyenzo muhimu ya maendeleo ya taifa kwa kuzalisha ajira, kuongeza mapato ya jamii, kuvutia uwekezaji, kuhifadhi misitu na kuendeleza matumizi ya nishati safi, sanjari na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Tanzania imeamua kuwa kitovu cha soko la kaboni lenye uadilifu barani Afrika, soko ambalo kila tani ya kaboni inayothibitishwa inatafsirika kuwa ajira kwa vijana wetu, mapato kwa vijiji vyetu, misitu iliyohifadhiwa, nishati safi majumbani mwetu na mtaji wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,” amesema.

Masauni ameeleza mafanikio ya soko la kaboni hayatategemea wingi wa miradi pekee, bali ubora wa matokeo, uhalali wa kisheria, uwekezaji unaotekelezwa na manufaa halisi yanayowafikia wananchi.

Amesema chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ajenda ya nishati safi ya kupikia ni mojawapo ya maeneo yenye fursa kubwa ya biashara ya kaboni, kutokana na uwezo wake wa kufikia mamilioni ya kaya na kuchangia kupunguza gesijoto.

Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC), Kathryn Kigaraba amebainisha kituo hicho kina jukumu muhimu la kusaidia maendeleo ya soko la kaboni nchini kwa kuzingatia utaalamu wa kisayansi, mbinu sahihi za kitaalamu, uwazi wa taarifa na mifumo ya ufuatiliaji na uthibitishaji.

Amesema lengo ni kujenga soko ambalo miradi yake inatambuliwa na kuendelezwa kwa utaratibu unaofaa, inafanyika kwa uwazi na manufaa yanayopatikana yanachangia maendeleo endelevu ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Kigaraba, utekelezaji wa azma hiyo unahitaji ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za serikali, waendelezaji wa miradi ya kaboni, wawekezaji, taasisi za fedha, jamii za wenyeji, taasisi za utafiti na washirika wa maendeleo.

Ameongeza mifumo ya kitaasisi inayohusu tathmini ya miradi, usajili wa miradi, ubadilishanaji wa taarifa na ulinzi wa haki na maslahi ya wadau ni muhimu katika kujenga imani ya soko.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Richard Muyungi, amesema jamii zinazohusika na usimamizi wa misitu, ardhioevu, mikoko na maeneo mengine yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi kaboni, zinapaswa kushirikishwa kikamilifu katika kubuni na kutekeleza miradi pamoja na kupanga namna ya kugawana manufaa.

Aidha, wanawake, vijana, wajasiriamali wa ndani na waendelezaji wa miradi midogo wanapaswa kupata nafasi katika uchumi unaochochewa na soko la kaboni.

Previous Post

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

Next Post

TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

Next Post
TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MIGIRO AWAPA MAAGIZO MAWAZIRI

DK. MIGIRO AWAPA MAAGIZO MAWAZIRI

9 months ago
DK. NCHIMBI ATOA  AHADI KWA  DK. SAMIA

DK. NCHIMBI ATOA AHADI KWA DK. SAMIA

1 year ago

Popular News

  • TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KUWA KITOVU SOKO LA KABONI AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKURASA MPYA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?