• ePaper
Sunday, October 25, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TRC YAMKOSHA PROF. MBARAWA UBUNIFU  KIWANDA CHA MATARUMA YA ZEGE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 25, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TRC YAMKOSHA PROF. MBARAWA UBUNIFU  KIWANDA CHA MATARUMA YA ZEGE
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amelipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa ubunifu wa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mataruma ya zege nchini, akisema hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama za ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya reli.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewekeza Shilingi bilioni 379 katika uboreshaji wa reli ya MGR kipande cha Kaliua–Mpanda (Km 210) hatua inayolenga kuboresha huduma za usafiri wa reli katika eneo hilo.

Profesa Mbarawa ametoa pongezi hizo Oktoba 25, 2026 wakati akizungumzia uwekezaji huo katika eneo la Uyumbu, Wilaya ya Kaliua, Mkoani Tabora, akiendelea na ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa SGR vipande vya Makutopor-Tabora, Tabora- Isaka, Isaka – Mwanza na Tabora- Kigoma, ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,  kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kimkakati  hususani sekta ndogo ya reli.

Akiwa katika kiwanda cha uzalishaji mataruma ya zege kwaajili ya MGR ikiwa ni sehemu ya maboresho ya MGR  Kaliua-Mpanda, mesema gharama ya kutengeneza taruma moja ya chuma ni takriban shilingi 360,000 ikilinganishwa na shilingi 130,000 kwa taruma moja ya zege inayotengenezwa hapa nchini, hali inayodhihirisha uwezekano wa kupunguza gharama kupitia matumizi ya teknolojia hiyo.

Ameongeza kwa kusema kuwa, uzalishaji wa mataruma hayo nchini utawajengea Watanzania uwezo wa kitaalamu na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na abiria, huku ukifungua fursa kwa nchi jirani kunufaika na miundombinu ya reli ya Tanzania.

“Tunaamini kabisa huko tunakokwenda reli hii ya MGR nayo itakuwa ya kisasa na itaweza kufanya kazi kwa bidii na kuchukua mzigo zaidi,” amesema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa, amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mataruma yanayotosha kujenga kilomita 50 za reli kwa mwezi, sawa na kilomita 510 kwa mwaka.

Vilevile amesema,  matumizi ya mataruma ya zege ni sehemu ya mkakati wa kuboresha miundombinu ya reli na kuongeza uimara wa njia, hatua inayotarajiwa kuimarisha ufanisi wa shughuli za usafirishaji.

“Tunaenda kuifanyia mapinduzi makubwa reli ya SGR kwa kubadilisha sasa kutoka kwenye sleeper (taruma) zile za chuma kuja kwenye hizi sleeper za zege,” amesema Mhandisi Shiwa.

Previous Post

DK. HOMERA AAGIZA UZINDUZI WA KAMPENI YA WASHA UMEME VITONGOJINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MWIGULU ASHUSHA PRESHA SAKATA KUPAA BEI MAFUTA

MWIGULU ASHUSHA PRESHA SAKATA KUPAA BEI MAFUTA

7 months ago
TANZANIA YATOA WITO WA KUIMARISHWA UMOJA WA MATAIFA

TANZANIA YATOA WITO WA KUIMARISHWA UMOJA WA MATAIFA

1 month ago

Popular News

  • TRC YAMKOSHA PROF. MBARAWA UBUNIFU  KIWANDA CHA MATARUMA YA ZEGE

    TRC YAMKOSHA PROF. MBARAWA UBUNIFU  KIWANDA CHA MATARUMA YA ZEGE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. HOMERA AAGIZA UZINDUZI WA KAMPENI YA WASHA UMEME VITONGOJINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA MAJI KUPWA, MAJI KUJAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AZAM FC NI REKODI AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?