• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MWIGULU ASHUSHA PRESHA SAKATA KUPAA BEI MAFUTA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 13, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MWIGULU ASHUSHA PRESHA SAKATA KUPAA BEI MAFUTA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WAANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Tanzania ina uzoefu mkubwa wa kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kuathiri shughuli za uzalishaji na usafirishaji nchini ikiwemo iliyopo hivi sasa ya upandaji bei ya mafuta.

Amewataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu, huku serikali inafuatilia kwa umakini suala la mafuta, itahakikisha mafuta yanaendelea kupatikana nchini na kwamba, shughuli za uzalishaji na usafirishaji zisiathirike.

Dk. Mwigulu alitoa kauli hiyo jijini Dodoma, alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mvumi Mission, akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Chamwino.

Waziri Mkuu, alisema kufuatia kuwepo kwa changamoto ya upandaji wa bei za mafuta ambazo zinazikumba nchi mbalimbali hivi sasa baada ya kuwepo kwa mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati, serikali inaendelea kufanya tathmini ya kina kwa kufuatilia mwenendo wa jambo hilo.

“Serikali inatambua na kufuatilia kwa ukaribu masuala ya uchumi na maisha yanayoendelea kote duniani na hapa nchini kwetu na hata juzi, mlisikia kauli ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhusu mafuta,”alisema

Alisema serikali inafuatilia kwa ukaribu hatua kwa hatua na kwamba, inakutana kila wakati na wadau mbalimbali wakiwemo wa sekta binafsi na kwamba, leo anatarajia kukutana nao.

“Hawa ni wadau muhimu katika kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele hasa hasa katika masuala haya ambayo yanahusisha ushirikiano wa hali ya juu wa wadau mbalimbali,”alisema

Alisema jambo la mafuta haliamriwi na nchi husika pekee yake na kwamba, nchi nyingi duniani siyo waamuzi wa hatima ya mafuta.

“Mnakumbuka ilipotokea COVID 19 dunia nzima ilitikisika katika masuala haya ya usafirishaji na masuala ya mafuta sababu ni moja tu, siyo kila nchi inazalisha mafuta na siyo kila nchi inajitegemea kwenye suala la mafuta,”alisema

Dk. Mwigulu alisema ilipotokea COVID 19 Tanzania iliendelea kufuatilia kwa ukaribu kufanya tathmini na kuchukua hatua kuhakikisha shughuli za uzalishaji ndani ya nchi haziathiriki.

“Pamoja na kuwa ilikuwa jambo la dunia nzima, lakini tulilifuatilia kwa ukaribu, utaratibu na kuchukua hatua stahiki bila ya taharuki na Tanzania chini ya Rais Dk.Samia tukavuka salama bila uhaba wa bidhaa zote muhimu ikiwemo mafuta yenyewe ambayo ni injini ya uendeshaji wa uchumi,”alisema

Alisema baada ya COVID 19, likajitokeza jambo lingine la mzozo wa Mashariki mwa Ulaya kati ya Urusi dhidi ya Ukraine, nchi hizo ndizo wazalishaji wakubwa wa mafuta ya kula na mafuta ya nishati.

“Nchi nyingi za Afrika ukiwemo ukanda wa Afrika Mashariki, zikakumbwa na upungufu wa mafuta ya kula, mafuta ya nishati, ngano pamoja na bidhaa zingine ambazo wazalishaji wakubwa ni nchi hizo kama ilivyokuwa COVID 19.

“Rais Dk. Samia akasema twendeni tufanye tathmini kwa kina kwa uangalifu na tuchukue hatua kwa uangalifu bila ya kuwa na taharuki Dk.Samia alituagiza kushirikishwa kwa sekta za umma, serikali na sekta binafsi,”alisema

Aliongeza: “Kwa nchi zingine, ilikuwa jambo la kawaida tu mtu anafuatilia vituo vya mafuta kwa ajili ya kuweka mafuta katika vituo 10 hadi 15 na hatimaye yanaisha yale yaliyokuwa yanasaidia kuzunguka na hatimaye unatafuta vijana wa kusukuma gari likae pembeni unatafuta mafuta mwezi mzima ili kuiondoe hilo gari,”alisema.

Alisema Rais Dk.Samia alisema jambo la kwanza ni kuhakikisha bidhaa hizo zipo bila ya upungufu kutokana na kuwa, hiyo ndiyo injini ya uzalishaji.

“Akasema jambo la pili ni tushughulike na bei zake sababu bei ikipanda kila kitu kitapanda ambapo gharama za uzalishaji zitapanda, gharama za usafirishaji pia zitapanda, gharama za maisha zitapanda na bahati nzuri, wakati ule nilikuwa Waziri wa Fedha, tulifanya vikao usiku na mchana kuhakikisha tunatekeleza maagizo hayo ya Rais Dk.Samia,”alisema.   

Waziri Mkuu alisema miongoni mwa mambo ambayo waliyatekeleza ni kuhakikisha uupatikanaji wa bidhaa yenyewe na kusiwe na uhaba wa bidhaa hiyo na kushughulikia bei yake.

“Tukavuka salama, hatukukaa sawa likajitokeza suala la upungufu wa fedha za kigeni kule ughaibuni mafuta huwezi kununua bila fedha za kigeni, sasa ukajitokeza uhaba wa fedha hizo mafuta yapo, fedha hakuna,”alisema

Alisema katika nchi nyingi za Afrika hususan Ukanda wa Afrika Mashariki, zilikuwa zinaacha mafuta yao bandarini kipindi cha mwezi mzima hawana fedha za kigeni ya kulipia hayo mafuta.

“Rais Dk.Samia katika hilo akasema wala tusiwe na taharuki tufanye tathmini kwa kina tutekeleze majukumu haya kwa kuzingatia kipaumbele sehemu kubwa fedha za kigeni tupeleke katika kununua dawa ambazo zinatumika na watanzania ununuzi wake unatumika na fedha za kigeni watanzania wasije kufa kwa kukosa dawa,”alisema.

Alisema Rais Dk.Samia aliagiza sehemu ya pili ya fedha hizo ziende katika nishati ya mafuta kusiwepo na uhaba wa bidhaa hiyo.

“Baadhi ya nchi zikachukua hatua za mkato na dili kibao mpaka leo hawajamaliza madeni yale, sisi tukavuka salama bila uhaba wa bidhaa hiyo wala kutengeneza madeni yanayohusiana na mafuta,”alisema   

Dk. Mwigulu, alisema hivi sasa limejitokeza suala hilo la mzozo unaohusisha Mashariki ya Kati na mataifa mengine ambao unaathiri pia Tanzania kwa kiasi fulani.

“Kabla ya mathara kuja Tanzania, Rais Dk.Samia alishatuelekeza ndani ya serikali kuwa, kuna madhara yanakuja tumeendelea kufuata utaratibu ule ule jinsi tulivyovuka matatizo mengine yalivyokuja bila ya taharuki,bila ya ugomvi kati ya serikali na watoa huduma,”alisema.

Alisema serikali inafanya tathmini kwa kina kujua hatua stahiki zinazotakiwa kuchukuliwa kwa muda mwafaka.

Alisema Tanzania ina uzoefu na kwamba jambo hilo siyo la kwanza kutokea, hivyo aliwataka Watanzania kutokuwa na taharuki wala kuwepo kwa ugomvi kati ya wananchi na watoa huduma.     

“Hili siyo la kwanza na tena hayo tuliyovuka wala siyo siku nyingi, juzi juzi COVID 19 ilikuwa 2020/2021 na hilo la Mashariki ya Ulaya ni la mwaka 2021/2023 na la upungufu wa fedha za kigeni ni la mwaka 2024/2025 na tukavuka salama,”alisema.

Dk. Mwigulu alisema Tanzania ilivuka salama kupitia miongozo hiyo ya Rais Dk.Samia na kwamba,  kama siyo hilo la sasa Watanzania wangeshasahau kulikuwepo na uhaba wa fedha za kigeni.

“Kama kuna muda ulitokea mabadiliko ya sera kukawa na shida upatikanaji wa dola yaani mafuta yapo alikwishaagiza lakini kuyalipia anazunguka mabenki anapewa dola za kimarekani 200 hivyo ndivyo ilivyokuwa lakini utulivu wa Rais Dk.Samia stahili yake ya kutokuwa na taharuki tukavuka salama,”alisema

Alisema hata jambo la upandaji wa bei za mafuta serikali inafuatilia kwa ukaribu, umakini na kwamba kila siku watendaji wanafanya vikao vya sekta mbalimbali kuhakikisha bidhaa za mafuta za aina zote hazihadimiki.

“Na jambo la pili serikali inashughulika na bei za bidhaa hizo,bei za huduma shughuli za uzalishaji zisiathirike na shughuli za usafirishaji zisiathirike pia kwa kiwango ambacho Watanzania wanaweza kushindwa kukimudu,”alisema.  

ASISITIZA MATUMIZI FEDHA ZA UMMA

Dk. Mwigulu alisisitiza fedha za umma zitumike vizuri na kuleta tija iliyokusudiwa pasipo ubadhirifu.


Alisema Rais Dk. Samia, ametoa fedha kugharimia miundombinu, hivyo ni wajibu zikatumika vizuri.


“Fedha hizo zinatakiwa zionekane katika huduma za wananchi wanazopata. Haikubaliki mwananchi anakweenda hospitali anaambiwa akanunue dawa nje wakati tunaambiwa tuna utoshelevu wa asilimia 90. Tunataka serikali inapotoa fedha wananchi wanufaike nazo,”alisema.


KUHUSU BARABARA

Akizungumza kuhusu ujenzi wa barabara ya Ntyuka, Mvumi hadi Kikombo, Dk.  Mwigulu alisema ni muhimu kwa sababu inaunganisha maeneo ya uzalishaji na Mji wa Dodoma.

Waziri Mkuu alisema barabara hiyo inarahisha kufika katika hospitali ya macho ambapo wananchi wanatoka maeneo mbalimbali kufuata huduma.


“Nimepata maelezo kuwa, mkandarasi amelipwa malipo yake, hivyo hakikisheni barabara hii inakamilika kwa wakati. Kama mnataka kuendelea kupata miradi nchini hakikisheni kazi zote katika barabara hii zinakamilika kwa wakati,


”Serikali inapomlipa mkandarasi lazima asimamiwekuhakikisha analipa wafanyakazi wake kwa wakati. Inaudhi kukuta serikali imelipa malipo yote,unakuta kuna watu wanadai hatutaki kuona,”alisema.


Alisisitizas kuwa,  serikali ikigundua kuna wandarasi wa nje wanaondoka na madeni ya Watanzania hawapati kazi  yoyote.

ABDALLAH ULEGA

Akizungumza kuhusu mradi huo wa barabara ya Ntyuka, Mvumi hadi Kikombo, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, alisema barabara hiyo inajengwa kwa hatua tatu ambapo hatua ya kwanza imekamilika kwa asilimia 90.

Alisema barabara hiyo itasaidia kwa Mji wa dodoma kutokana na kukua kwake kila siku.

“Barabara hii inatanua mji wetu na kusaidia wananchi kufika kwa urahisi katika hospitali teule ya macho ya Mvumi. Barabara hii pia itasaidia kusafirisha vyakula ambavyo vinazalishwa katika maeneo ya pembezoni ya mkoa,”alisema.

MBUNGE

Mbunge wa Jimbo Mvumi, Livingstone Lusinde, alisema Rais Dk.Samia ametoa sh. bilioni 98 kwa ujenzi wa barabara hiyo.

Previous Post

SERIKALI YAFUNGUA MILANGO KWA WADAU AFCON 2027

Next Post

WACHUMI WATAKA RAIS DK. SAMIA AUNGWE MKONO

Next Post
WACHUMI WATAKA RAIS DK. SAMIA AUNGWE MKONO

WACHUMI WATAKA RAIS DK. SAMIA AUNGWE MKONO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UBINGWA LIGI KUU WAWATEGA BARKER, PEDRO 

UBINGWA LIGI KUU WAWATEGA BARKER, PEDRO 

1 month ago
WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS

WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS

3 weeks ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?