• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KOCHA AIPA JEURI YANGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 23, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
KOCHA AIPA JEURI YANGA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

SAA chache mara baada ya Rais wa Yanga Mhandisi Hersi Said, kukutana na Kocha mpya wa timu hiyo, Manqoba Mngqithi na kufanya kikao cha kwanza na benchi zima la ufundi, uongozi wa timu hiyo umesema unajivunia kumpata kwani wana imani watabeba mataji mengi msimu ujao.

Julai 10, mwaka huu Yanga ilimtambulisha kocha huyo akirithi mikoba ya aliyekuwa kocha wao Pedro Goncalves waliyeachana naye Mei 6, mwaka huu.

Yanga waliachana na Pedro baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu kwa baadhi ya mechi na kikosi hicho alikabidhiwa Kocha wa Msaidizi, Abdihamid Moallin kumalizia mechi 10 zilizobakia msimu huu uliomalizika.

Moallin alisimamia vyema timu hiyo na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa tano mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kumalizia ikiwa na pointi 75 huku wapinzani wao Simba wakimaliza nafasi ya pili kwa pointi 73.

Akizungumza mara baada ya kocha huyo kukutana na uongozi wa Yanga jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa timu hiyo Ally Kamwe alisema tayari kocha na wasaidizi wake walishawasili na kuingia kambini moja kwa moja kuanza programu za msimu mpya utakaoanza mwezi ujao.

Alisema kuwa kocha huyo amekuja mapema nchini ili kuanza maandalizi ya haraka ya msimu ujao na kutimiza malengo ambayo amepewa na uongozi.

Alisema wanajivunia kumpata kocha huyo na kwamba wana imani atawasaidia kufanya vyema ikiwemo kubeba mataji mbalimbali kuanzia msimu ujao.

“Kocha ameshawasili na leo (jana), amekutana na Rais Hersi akiwa na benchi zima la ufundi.

“Walikaa kikao cha muda mchache na uongozi na uongozi kupanga mikakati mbalimbali ya msimu ujao.

“Baadaye alipelekwa moja kwa moja kambini kuonana na wachezaji na kuanza programu zake, tuna matumaini makubwa tutafanya vyema ikiwemo kubeba mataji mbalimbali chini yake,” alisema Kamwe.

Benchi jipya la timu hiyo linaundwa na Kocha Mngqithi akisaidiana na Simo Dladla.

Pia, Yanga imemtangaza Kocha wa Makipa, Greg Etafia kutoka Nigeria vilevile imefanikiwa kumchukua Mtaalamu wa Uchambuzi wa Viwango na Mifumo ya Soka, Yardaan Valodia.

Hadi hivi sasa, Yanga imewasajili nyota wapya wawili ambao ni Hussein Mihambo na Abdulnasir Mohamed wote kutoka Mashujaa FC ya Kigoma.

Previous Post

MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

Next Post

MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

Next Post
MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

STEVE NYERERE, WEMA SEPETU WAMLILIA LUKUVI

STEVE NYERERE, WEMA SEPETU WAMLILIA LUKUVI

4 months ago
‘MLIOGHUSHI AKAUNTI ZA JKT MITANDOANI ZIFUTENI HARAKA’

‘MLIOGHUSHI AKAUNTI ZA JKT MITANDOANI ZIFUTENI HARAKA’

9 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?