• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

DK. NCHIMBI AKAGUA UWANJA WA AFCON ARUSHA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 26, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
DK. NCHIMBI AKAGUA UWANJA WA AFCON ARUSHA
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Arusha, utakaotumika katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027), unaojengwa Jijini Arusha.

Makamu wa Rais amepongeza maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo, ambapo amesema ni faraja kuona ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa ili kuvutia michuano hiyo kufanyika nchini Tanzania, inatakelezwa kikamilifu.

Amemshukuru Rais Dk. Samia kwa kuendelea kutoa fedha ili kuhakikisha uwanja huo unakamilika kwa wakati.

Aidha, Makamu wa Rais ameishukuru Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na mkoa wa Arusha, Wakandarasi na Mshauri Elekezi kwa kazi kubwa waliyofanya katika Uwanja huo.

Makamu wa Rais amewataka Viongozi wa Wizara pamoja na Mkoa wa Arusha kusimamia vema agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha barabara zinazotumika katika kufika uwanjani hapo zinakamilika kwa wakati.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makala, amemueleza Makamu wa Rais, maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo ambao umefikia asilimia 88, ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Agosti, 2026.

Uwanja wa Arusha, utakapokamilika, mbali na michezo, unatarajiwa kuwa kivutio cha utalii ukiwa umebeba alama ya Mlima Kilimanjaro, Madini ya Tanzanite na Bendera ya Taifa.

Previous Post

KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA YAOMBA KUOMBEWA

YANGA YAOMBA KUOMBEWA

5 months ago
MEJA KUNTA AGEUKIA WASANII CHIPUKIZI

MEJA KUNTA AGEUKIA WASANII CHIPUKIZI

6 months ago

Popular News

  • DK. NCHIMBI AKAGUA UWANJA WA AFCON ARUSHA

    DK. NCHIMBI AKAGUA UWANJA WA AFCON ARUSHA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?