• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

VIONGOZI SIMBASC WATAKIWA KUJITATHMINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 2, 2025
in Burudani, Michezo
0
VIONGOZI SIMBASC WATAKIWA KUJITATHMINI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

VIONGOZI wa Klabu ya Simba, wametakiwa kujitathmini kuhakikisha wanainusuru timu hiyo ili ifanye vizuri katika michuano mbalimbali.

Uongozi wa Klabu ya Simba, juzi ulifanya Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa Simba, walisema uongozi unatakiwa kujitathmini kuhakikisha wanainusuru timu ili ifanye vizuri.

Mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah  Kibadeni, alisema viongozi wa klabu hiyo wanatakiwa kujitathmini kuhakikisha wanainusuru timu yao.

Alisema ndani ya uongozi wa Simba kuna migogoro baina yao, hivyo wanachotakiwa ni kukaa pamoja na kuzungumza ili kujua chanzo cha matatizo na kuyapatia suluhusho kwa manufaa ya klabu kwa ujumla.

Alisisitiza hata kwa upande wake hakualikwa wala kushirikishwa kitu chochote kuhusu mkutano huo kitu ambacho siyo kizuri kwani wachezaji wakongwe wana mchango mkubwa ndani ya uongozi wa Simba na klabu kwa ujumla, hivyo wanatakiwa kushirikishwa vitu vinavyoendelea ili kutoa ushauri wao.

“Mimi mwenyewe nilishtushwa baada ya kupigiwa simu na watu waliokuwa wapo ndani ya mkutano kwani sikushirikishwa kwa kitu chochote japokuwa siyo kiongozi lakini nina mchango mkubwa ndani ya Simba.

“Sikwenda kwani sikualikwa na niliona viongozi waliopo inawezekana wanajiweza lakini wengi wamelalamika jinsi mwenyekiti alivyomaliza mkutano.

“Mimi ni mmoja wa watu nilioipa Simba mafanikio makubwa kipindi ninacheza na baadaye kocha, lakini bado nina mchango mkubwa kwa klabu kama wangekuwa wakiuhitaji.

“Watu hawataki kunitumia hivyo siwezi kuwalazimisha kwani kila mmoja anatambua uwezo wangu maana nimutumikia soka miaka 50 katika nyanja mbalimbali.

“Uongozi unatakiwa kujithmini kwani kuna tatizo ndani ya Simba, hakuna mtu anapenda kufungwa, watu wanalalamika wameshachoka kufungwa kila siku.

“Viongozi wajitazame wanakosea wapi na kurekebisha kasoro zao kuhakikisha timu inafanya vizuri kama ilivyokuwa awali, wachezaji wa zamani wanatakiwa kuhusishwa ili wasaidiwe kwa mambo mbalimbali,” alisema Kibadeni.

Kwa upande wa mchezaji wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella, alisema siku zote kama kuna uongozi una matatizo hata timu haiwezi kufanya vizuri kwa namna yoyote.

Alisema hata timu ilipokwenda nchini Mali kwa mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), dhidi ya Stade Malien, hakuna kiongozi mkubwa aliofuatana nao kwa ajili ya kuwapa sapoti, viongozi wote walijikitika katika mkutano kitu ambacho siyo sahihi.

Alisisitiza kwamba timu ilipata matokeo mabaya kwani chanzo kilianzia kwa viongozi kushindwa kwenda kuipa sapoti ya kutosha timu ilipokuwa ugenini.

“Shida ipo kwa uongozi unatakiwa kujifanyia tathmini kuhakikisha Simba inarudi katika makali yake kama zamani.

“Viongozi wanatakiwa kukaa pamoja na kuzunguza ikiwemo kujitafakari, watapata ufumbuzi na tutaanza kuiona timu ikifanya vizuri katika michuano mbalimbali,” alisema Mogella.

Naye Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema aliahirisha mkutano baada ya kumaliza ajenda zote na hakukuwa na hoja ya ziada.

“Niliongoza mkutano na baadaye niliuahirisha kutokana na ajenda zote kumalizika na hakukuwa na hoja ndiyo nilipoamua kuuahirisha,” alisema Mangungu.

Previous Post

PANTEV ATAJA SABABU KUPOTEZA CAFCL

Next Post

SIMULIZI YA RAIS DK. SAMIA ALIVYOWABEBA WANASIASA NJE 

Next Post
SIMULIZI YA RAIS DK. SAMIA ALIVYOWABEBA WANASIASA NJE 

SIMULIZI YA RAIS DK. SAMIA ALIVYOWABEBA WANASIASA NJE 

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIKU 100 ZA KAZI NA UTU

SIKU 100 ZA KAZI NA UTU

2 months ago
RAIS DK. MWINYI AONYA SIASA ZA CHUKI

RAIS DK. MWINYI AONYA SIASA ZA CHUKI

8 months ago

Popular News

  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?