• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 25, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SUPERIUS ERNEST

MAKAMU wa Rais Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema Katiba ndiyo msingi mkubwa wa haki na maendeleo, hivyo inatakiwa kuwa ajenda ya watu wote kwani ndiyo utashi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Pia, alisisitiza upendo, umoja, mshikamano katika kujenga taifa lenye maridhiano, linalojengwa na haki kama msingi wa amani.

Dk. Nchimbi aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa 15 wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), uliofanyika Mlimani City, ambapo aliwapongeza kwa jitihada kubwa za kujiimarisha na mipango ya kujenga makao makuu.

“Ni muhimu sana, watetezi wa haki za binadamu, asasi za kiraia, vyama vya siasa na Watanzania kufahamu kuwa sheria kuu ya nchi ni katiba kwani ndiyo msingi wa maendeleo na haki.

Aliongeza:”Moja ya jambo muhimu sana ni utashi wa Rais aliyeko madarakani wa kupata katiba mpya,”alisema.

Alifafanua kwamba alipokuwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, walipounda kamati ya kukusanya maoni ya wananchi, ilimwambia asilimia kubwa wanataka katiba mpya, ambapo aliwasilisha kwa Rais kama Mwenyekiti wa Chama wakati huo, na kumweleza na kumuuliza juu ya hilo ambapo alikubali liwekwe katika ilani ya Chama.

Alisema katika utawa bora wa nchi, kitu kinachoweza kubeba mambo yote ni katiba, hakuna sheria inayoweza kutungwa kukinzana na katiba, lakini kilichopo ndani yake kinaweza kutengua sheria nyingine yoyote iliyopo na siku unapopitisha katiba mpya sheria zingine zote zinazokinzana zinakuwa zimekuwa.

“Ndiyo maana kama kuna kitu ningeambiwa Makamu wa Rais kama una jambo moja na hiyo ni nafasi ya mwisho waambie Watanzania, ningewaambia pambaneni mpate katiba mpya, mpate katiba ambayo ni ya makubalinao ya makundi yote, katiba yenye muafaka katika taifa.

“Tupate katiba itakayotupeleka mbele miaka 50 ijayo, ambayo kila mtanzania popote alipo atajisikia fahari kujitambulisa kutoka Tanzania, katiba inayojali maisha ya mtu, inayoheshimu haki za raia wake,” alisema.

“Ningekuwa namna ya kuwaambia Watanzania kwa namna ambayo Rais hawezi kusikia, ningefanya hivi, kwamba Rais analitaka sukumeni, lakini mazingira hayaruhusu lazima nisemee kwenye jukwaa, kwamba jamani hili Rais Dk. Samia analitaka sukumeni, anataka litekelezwe,” alisema.

Alisema ni vyema kupata katiba itakayolipeleka taifa katika maendeleo siyo ya mali tu na kuheshimu utu wa kila mtanzania.

“Majaribio ya kupata katiba mpya yamekuwepo kwa zaidi ya miaka 40, vuguvugu limedumu likiwa kubwa tangu mwaka 1992 baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa,” alisema.

Alieleza kuwa katika awamu ya nne ndipo walianza jitihada hizo na kupiga hatua kidogo na wakakwama mahali.

“Tunaweza tukawa na mambo 40 ya kupigania, katika mkakati wowote lazima uchague jambo kubwa ni lipi. Mfano sasa hivi ukisikiliza madai ya mengi ya watu mbalimbali, unabaini wanapanga mambo 10 kwa wakati mmoja. Hushindi vita ya mambo kumi, lazima uchague kubwa linaloweza kubeba mengine ni lipi,” alisema.

Alisisitiza ni vyema kutumia fursa hiyo, ambayo Rais anataka kusisitiza litekelezwe kama ambavyo tume ya haki jinai ilishauri kuwa litekelezwe kabla ya uchaguzi 2029 wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2030. Pia, Tume ya jaji Chande nayo imeshauri hadi 2028 iwe imepatikana na itumike katika chaguzi hizo.

“Komaeni hapo, tusisubiri hadi aje Rais asiyetaka katiba mpya, katiba uliyopo sasa Rais mbinafsi ataitaka tu kwa sababu inampa nguvu zisizo na maana, tusiruhusu tupate Rais ambaye hana hamu na katiba tutaitafuta miaka 50 mingine, kwa sababu Rais Dk. Samia ameonesha nia, komaeni hapo hapo, niwaambie nini muelewe,” alisema.

Alifafanua kwamba hata mapendekezo ya tume ya haki jinai yako zaidi ya 350, kama yakitekelezwa nchi haitabaki kama ilivyo sasa hivi, kuna mambo ya hovyo hovyo mengi yanafanyika hapa, Rais kasema tuyaondoe, habari ya watu kukaa mahabusu kwa kesi ndogo ndogo viko vingi tu, kukosa dhamana.

“Narudia kutumia maneno magumu tukomae hapo. Nazungumza na Watanzania wote, wanaccm, wapinzani na asasi za kiraia, waambie wanaccm katiba mpya ni kwa faida ya watoto, wajukuu na vizazi vijavyo, katiba mpya ni kwa faida ya taifa letu tupigane wote kupata katiba mpya, tukifika hapo kasi ya maendeleo ya taifa itakuwa kubwa kuliko mnavyofikiri,” alisema.

Alisema katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, ambayo imeanza kutekelezwa na Serikali, imeeleza kwa kina itakavyolinda na kuheshimu haki za binadamu.

Kuhusu dira mpya alisema:”Katika Dira ya 2050 ya Tanzania, moja ya mambo yaliyoelezwa kwa kirefu na kwa kina, ni kujenga jamii inayozingatia na kujali haki za binadamu,kati ya sasa na mwaka 2050,” alisema.

Alieleza inapozungumziwa haki za binadamu inamaanisha utawala bora, ushirikishwaji wa wananchi na usawa wa kijamii, ambapo wanashirikiana na watetezi wa haki za binadamu kujenga taifa lenye haki.

Alifafanua kuwa tafsiri halisi ya haki za binadamu, inaanzia kwa mtu akisema:” Tafsiri halisi ya haki za binadamu ni Mama anayetaka mtoto wake awe salama, Baba anayetaka kuilisha familia yake kwa heshima, kijana anayetaka kusikilizwa.

“Mwananchi anayetaka kutoa maono yake bila hofu, mtu anayetuhumiwa anayetaka kutendewa kwa mujibu wa sheria, polisi anayekwenda kazini na kutamani kurudi salama katika familia yake, mwandishi wa habari anayetaka kufanya kazi yake kwa usalama na haki, mwananchi ambaye hana cheo, fedha lakini kwa sababu ya utu wake athaminiwe,” alisema.  

Alisema katika hali hiyo, siyo lazima serikali au wananchi wakubaliane kila kitu, kwa sababu binadamu aliyekamilika lazima watofautiane kwa hoja na kuelewa katika ujenzi wa taifa.

“Serikali inaendelea kutambua na kuunga mkono kazi na jitihada kubwa inayofanywa na watetezi wa haki za binadamu nchini, ndiyo maana nimekuwepo hapa. Siyo lazima serikali ikubaliane na yote mnayotaka au kukubaliana na yote wanayotaka wananchi, lakini wote tukubaliane katika kuleta maendeleo,” alisema.

Alisema serikali haiwezi kupuuza jitihada zinazofanywa na asasi za haki za binadamu, kwani jitihada zake zimesaidia katika kujena uchumi wa taifa, ununuzi wa bidhaa, kushirikiana kuchangia kodi na mapato ya serikali, kushiriki kutoa elimu, kuvutia rasilimali fedha kutoka nje ya nchi.

“Kwa namna hiyo, nawashukuru wadau wetu wa kimataifa akiwemo Balozi wa Umoja wa Ulaya, tunaomba utufikishie salamu tunatambua mchango wao mkubwa, kwani fedha zilizotolewa ndizo zimesaidia kuongeza ajira, tunawasihi waendelee kutoa michango hiyo licha ya kusaidia maendeleo zinasaidia asasi hizi za kiraia,” alisema.

Alisisitiza kuwa serikali inaendelea kutengeneza mazingira wezeshi asasi hizo za kiraia, kuendelea kujenga taifa.

Alieleza takwimu zimeonesha kuwa katika kusaidia asasi za kiraia, asilimia 85 zilikuwa zakitegemea msaada kutoka nje ya nchi, huku taasisi zisizo na vyanzo mbadala ni asilimia 79 na asilimia 40 zimesitisha utekelezaji wa shughuli zake, ambapo alisema ombi lao la sera wezeshi linaeleweka na kuwahakikishia ushirikiano kwa kazi yao wanayoifanya kwa jamii.

Akieleza kuhusu jitihada zao za ujenzi wa makao makuu katika kiwanja walichopewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Mitumba jijini Dodoma, alisema, ombi hilo ataliwakilisha kwa Rais na mafanikio waliyofikia ya kukusanya sh. milioni 300.

Kuhusu haki na amani, alisema ni msisitizo wa Rais Dk. Samia kuwa haki ni msingi wa amani, jambo ambalo linawekwa katika vitendo.

Dk. Nchimbi alisema anatamani kuwe na Tanzania ambayo kila mwananchi anajisikia amani, anatamani kuchangia mafanikio yake, licha ya kutofautiana katika siasa, dini, makabila kutambuana katika utanzania wao, bila uhasama na uadui.

“Nimwombe kila mtanzania atumie kila nafasi aliyonayo kurudisha, umoja, mshikamano, kusimamia haki kama msingi wa amani,” alisema.

Awali akimkaribisha Dk. Nchimbi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba alisema serikali inathamini mchango na kazi kubwa inayofanywa na asasi za kiraia ikiwemo THRDC na itaendelea kushirikiana nao kwa karibu kuchochea maendeleo.

Alitaja mchango wa asasi hizo ni kutoa elimu kwa wananchi kusaidia katika kufanya tafiti mbalimbali na kusaidia jamii katika kulinda haki za binadamu, huku akiwapongeza kwa mkutano huo ambao umeendelea kuwaweka pamoja wadau wa haki za binadamu.

Kwa upande wake, Mratibu wa Taifa wa THRDC, Wakili Onesmo Ole Ngurumwa, alimshukuru Dk. Nchimbi kwa kukubali kuhudhuria katika mkutano huo mkuu wa 15 wa mwaka, ambapo aliwasilisha changamoto zao ni uhitaji wa fedha kufanikisha ujenzi wa Makao Mkuu jijini Dodoma ambapo kwa sasa wamefanikisha kukusanya sh. milioni 300 katika uhitaji wa milioni 500.

Aidha, alimshukuru Rais Dk. Samia kwa kutambua kazi kubwa wanayoifanya na kuwapa ushirikiano wakati wote ikiwemo kuwapatia kiwanja wapatako jenga jengo hilo.

Previous Post

MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA UWEKEZAJI AFYA AFRIKA

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA UWEKEZAJI AFYA AFRIKA

3 days ago
MWAKINYO AOMBA RADHI

MWAKINYO AOMBA RADHI

1 month ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?