• ePaper
Monday, June 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SIRI UTEUZI VIONGOZI CCM

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 11, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SIRI UTEUZI VIONGOZI CCM
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi, na Mafunzo,  Kenani Kihongosi, amesema heshima ya CCM ni kubwa kuliko fedha na umaarufu, hivyo maamuzi ya chama juu ya wagombea hufanywa kwa kuangalia uadilifu na maadili ya mgombea husika.

Kihongosi ameeleza hayo akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyehunge Halmashauri ya Buchosha Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, ikiwa ni muendeleo wa ziara yake Kanda ya Ziwa.

Kihongosi ameeleza hayo akijibu hoja ya moja wa wananchi, Leonard Methusela iliyeuliza kwanini ngazi za juu za chama zinawakata wagombea ambao wamepitishwa na wajumbe na kuleta majina ya watu wanao wataka wao, hatua ambayo inawagombanisha wananchi na wagombea wao.

Akijibu hoja hiyo Kihongosi amesema majina ya wagombea yanapochujwa huanza kutoka ngazi ya chini na kuendelea hadi Halmashauri Kuu ya Taifa,lakini kuna baadhi ya vitu wakiona si sawa huwa wanawakata ili kuweka wanaofaa.

Amesema chama hakimpi mtu nafasi kwa sababu wanaamini ana nguvu ya fedha au umarufu ndani ya CCM ,hawaangalii vitu hivyo bali wanaangalia heshima ya chama, na kuongeza kuwa wakiendekeza hela, rushwa au kujuana wengi wasingepata nafasi hata yeye asingekuwa mwenezi wa chama.

“Wale wanaotoa rushwa au kujaribu kuathiri mchakato wa uteuzi hawataweza kuleta maendeleo. Heshima ya Chama Cha Mapinduzi ni kubwa kuliko mali au umaarufu wa mtu,” amesema Kihongosi.

Ameongeza; “Tukiendekeza fedha, rushwa au uhusiano binafsi, hata mimi leo nisingekuwa Mwenezi wa CCM, hii ni kwa sababu heshima na nidhamu ya chama ndiyo msingi wa uteuzi wa viongozi”.

Amesisitiza uteuzi wa viongozi ndani ya chama hicho lazima uende sambamba na heshima, uadilifu na kupinga rushwa ili kuhakikisha maendeleo endelevu kwa wananchi, lakini wamekuwa wakibaini kuna wengi wamekuwa wakipita kwa njia zisizo halali.

Previous Post

MAELFU YA WAGONJWA KUTOKA NJE YA NCHI WAMIMINIKA KUPATA HUDUMA

Next Post

DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

Next Post
DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AIJAZA NOTI YANGA

RAIS DK. SAMIA AIJAZA NOTI YANGA

2 months ago
MSIGWA AELEZA MANUFAA UBORESHAJI RELI YA TAZARA

MSIGWA AELEZA MANUFAA UBORESHAJI RELI YA TAZARA

5 months ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA ZATOA MSIMAMO LIGI KUU BARA

    YANGA, SIMBA ZATOA MSIMAMO LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WFP KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA USIMAMIZI WA MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HESHIMA KUBWA KWA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU: MAMBO MAZURI YANAKUJA, AIPA TANO SERENGETI BOYS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?